siasa

Katibu mkuu CUF alia na wanaofanya siasa kwenye nyumba za ibada

on

 

Muhamed Khamis

Unguja.Katibu mkuu wa Chama cha wananchi CUF Khalifa Suleiman amesema hawatawavumilia wale wote wanaotumia nyumba za ibada kufanya vikao kwa lengo la kukihujumu chama hicho kisiwani Pemba.

Khalifa aliyasema hayo juzi kisiwani Unguja wakati alipokua akizungumza na wanachama wa chama hicho kisiwani hapa katika mkutano uliofanyika Amani mjini Unguja.

Alisema kwa sababu siasa si uadui anashangazwa kuwa wapo baadhi ya watu kisiwani Pemba wamekua wakipanga uadui dhidi yao kwa lengo la kutaka kurejesha nyuma harakati za ujenzi wa chama  hicho.

‘’Tunawajua na tayari tumeshatoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama juu ya watu wanaofanya hivyo na tunaamini kuwa watachukuliwa hatua’’aliongezea Khalifa.

Aidha alisema hawatakubali tena kuchokozeka na watajibu kila aina ya uchokozi kwa njia wanazozijua wao hivyo wasijaribiwe.

Huku hayo yakijiri Makamo Mwneyekiti wa chama hicho Abas Juma Muhunzi aliwataka wanachama wao kuendeleza siasa safi na kuhubiri miakakati mipya ya ujenzi wa chama.

Muhunzi alisema kuzoroka kwa chama hicho kwa kipindi chote kulitokana  na udhaifu kwa viongozi waliokua na nafasi za juu kiutendaji na kwa sasa hali huo hawawezi kuiruhusu tena.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *