We have 449 guests and no members online

Matangazo Mapya

We provide the full IT solutions including web design, web development ...

10

Na: Frank Shija – MAELEZO

Rais wa Jmamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kumfutia usajili mwekezaji wa Kiwanda cha Nyama, Kampuni ya Triple S na badala yake watafute mwekezaji mwingine.

Agizo hilo limetolewa leo Mjini Shinyanga wakati akiwahutubia wananchi wa mji wa huo ambapo yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi iliyoambatana na sherehe ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

“Futeni usajili wa mradi wa Triple S, haiwezekani mwekezaji hakashindwa kuendesha kiwanda kwa zaidi ya miaka 10 sasa afu tuendelee kumkumbatia, tafuteni mwekezaji mwingine, mkishindwa semeni Serikali iweke hela, ili uzalishaji uendelee,” alisisitiza Rais Magufuli.

Aliongeza kuwa mwekezaji huyo amekuwa mbabaishaji kwani tangu kipindi yeye (Rais Magufuli) alipokuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo alimfahamu na alimpa maelekezo cha kusikitisha hakuna jambo aliloendeleza ikiwemo kuanza kwa uzalishaji.

Akizungumzia sababu ya kufanya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar katika upande huu wa Bara Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni moja, na kuongeza kuwa chimbuko halisi la uwepo wa Taifa la Tanzania ni Mapinduzi ya Zanzibara mabapo miezi michache tu baada ya kufanyika kwa mapinduzi hayo Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaliwa kwa Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake Waziri wa TAMISEMI na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri amesema wao kama Wazanzibar wamefarijika sana kwa kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuamua kushiriki maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu kwa kusherehekea katika upande wa Bara kitu ambacho akijawahi kufanyika kabla.

Aliongeza kuwa ujio wake umetokana na ukweli kwamba Tanzania ni nchi moja hivyo Rais Magufuli alivyoeleza nia yake ya kuadhimisha Maapinduzi huku Bara, Rais Dkt. Shein alimteua aje kumwakilisha na kueleza kuwa maefarijika sana na kusema Tanzania ni yetu sote na tutaendelea kuwa wamoja.

Rais Dkt. Magufuli yuko ziarani Mkoani Shinyanga ambapo kesho anatarajiwa kufungua viwanda kadhaa vilivyopo mkoani hapo, baadhi ya viwanda hivyo ni pamoja na Kiwanda cha Vinywaji Baridi (maji) cha Jambo, Kiwanda cha Mafuta na vingene.(P.T)

WEN

Sehemu ya wodi za wagonjwa katika hospitali  ya wilaya ya Nyamagana iliyofungwa umeme jua.

WEN 1

Mratibu wa Mradi wa  Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya   wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah, (kulia) akielezea maendeleo ya mradi huo kwa Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE), Paul Kiwele ( wa pili kutoka kulia). Wengine ni wataalam kutoka  Sehemu ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati na Madini.

WEN 2

Mratibu wa Mradi wa  Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya   wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kulia) akieleza jambo kwa Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (katikati). Kushoto ni  Nasra Mohamed kutoka  Wizara hiyo.

ENEO 3

Mratibu wa Mradi wa  Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya   wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kushoto mbele) akimwongoza  Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE), Paul Kiwele (kulia mbele) pamoja na wataalam kutoka Wizara ya  Nishati na Madini katika ziara kwenye mradi huo.

WEN 4

Mratibu wa Mradi wa  Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya   wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kulia) akielezea mfumo wa kuongozea vifaa vya umeme jua katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana.

WEN 5

Mratibu wa Mradi wa  Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya   wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kushoto) akionesha mita maalum ya kuruhusu umeme kuingia na kutoka kwenye  Gridi ya  Taifa.

WEN 6

Mratibu wa Mradi wa  Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya   wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah ( wa pili kutoka kulia) akionesha karabai zinazotumia umeme jua zilizotolewa na mradi  huo kwa wavuvi wa soko la samaki  la Mwaloni jijini Mwanza.

WEN 7

Mmoja wa wavuvi katika soko la samaki la Mwaloni jijini Mwanza, Joseph Athony (kushoto) akielezea manufaa ya karabai zinazotumia umeme jua zilizotolewa na Mradi wa  Umeme Jua wa Majaribio.(P.T)

PINDU 1

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea na wananchi wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisema mbali za jitihada zilizofanywa na serikali hiyo katika kuinua maisha ya wazanzibar ameahidi kuendelea kusimamia rasilimali ili zitumike kwa maslahi ya wananchi wote.

PINDU 2

2-Makamo wa Pili wa Rais Zaznzibar Balozi Seif Ali Idd akiongea na wananchi wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka jitihada ili kuendelea kujenga uchumi za Zanzibar kwa maslahi ya wananchi.

PINDU 3

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasalimia wananchi walijitokeza katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 5

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiimba wimbo wa Taifa katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 6

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 7

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 8

Vikundi mbalimbali, Asasi za Kiraia,Vyama vya Siasa,Mikoa,Wizara na Taasisi za Serikali wakipita mbele Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 13

Vikosi mablimbali vya Jeshi la Polisi vikipita mbele Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 14

Vijana vya halaiki wakiwa katika umbo linaloonesha miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 16

Kikosi cha Kwata la KimyaKimya wakionesha onesho wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 18

Komando wa Jeshi la Wananchi Tanzania akishuka katika kamba katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 19

Kikosi cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakionesha onesho wa namna ya kuakibiana na vikwazo mbalimbali wawapo kazini katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

PINDU 20

Askari wa Kikosi cha Mbwa, akionesha namna mbwa anavyoweza kuruka vikwazo mbalimbali katika kukabiliana na wahalifu katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

………..

Na: Frank Shija – MAELEZO

 

ZANZIBAR imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali za kimaendeleo na utoaji wa huduma bora za kijamii.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya Mapinduzi leo katika uwanja wa Amani, Unguja, Zanzibar.

Dkt. Sein amesema kuwa siku ya Mapinduzi ni muhimu sana katika historia ya Zanzibar kwani ndiyo siku ambayo Wazanzibar walipokuwa huru katika nchi yao na kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kujiletea maaendeleo.

“Tukiwa tunasherehekea miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni vyema tukajivunia maendeleo yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana.”Alisema Dkt. Shein.

Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu Mapinduzi Matukufu yatokee tarehe 12 Januari 1961, Dkt. Shein amesema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta za elimu kwa kuwa na ongezeko la shule kutoka shule 752 mwaka 2015 hadi kufikia 843 mwaka 2016.

Ongezeko hilo limeenda sambamba na ongezeko la udahili wa wananfunzi ambapo umeongezeka kutoka wanafunzi 384,000 hadi kufikia 424,000 mwaka 2016.

Katika sekta ya afya kumekuwa na mafanikio ya kuongezeka kwa vituo vya afya kwa asilimia 13.4 ambapo mwaka 2015 kulikuwa na Vituo vya Afya 134 hadi kufikia sasa jumla ya Vituo 152 vimepatikana.

Mafanikio mengine ni pamoja na upatikanaji wa ajira 2658 zilizotokana na miradi mbalimbali iliyozindulia katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya Mapinduzi, kukua kwa Sekta ya Utalii kwa ongezeko la watalii kwa asilimia 13 huku ikichangia pato la taifa kwa asilimia 27.

Huduma za kijamii zimezidi kuboreshwa huku upatikanaji wa maji safi na salama umeendelea kutatuliwa ambapo miradi ya maji imeekuwa ikitekelezwa ikiwemo kuchimba visima vipya 9 na kuvifanyia ukarabati visima vya zamani.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema kuwa Mapinduzi haya yamekuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa kuwa yamewaweka Wazanzibar kuwa huru katika kutekeleza shughuli zao za kujiletea maendeleo.

Zanzibar imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar huku ikiwa imepiga hatua kubwa za kimaendeleo ambapo katika shamra shamra za maadhimisho haya jumla ya miradi 32 ya maendeleo imezinduliwa huku mingine 16 ikiwekwa jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji wake, hayo yote ni matunda yatokanayo na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo baadaye yalizaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.(P.T)

1

ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka watatu kutoka kulia Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa wakwanza kulia pamoja na viongozi wengine.

unnamed

2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengiene  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3).

3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS  Mhandisi Cristianus Ako kabla ya kuweka jiwe la msingi.

4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3), mkoani Simiyu.

6

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.

55

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.(P.T)

Read more...

Barack Obama famously said “Africans must build Africa for Africa!”. A nice message, but what do you do, when Africans themselves fight each other while building the same house?
In Africa, those on the roof of the house under construction are receiving building stones from the ground, but .. Read Morehttp://www.africablogging.org/…/obamas-sour-story-on-gover…/(P.T)

Ukistaajabu Ya Mussa Utayaona Ya Firauni..

Published in Jamii

Happy Mapinduzi Day!

Published in Jamii

Image may contain: one or more people, car and outdoor


-Kwanini Mapinduzi, Kwanini Muungano?
Ndugu zangu,
Ningelipenda kuwa Zanzibar katika siku kama ya leo. Ningelipenda kuwa Zanzibar siku kama ya leo miaka 53 iliyopita.
Ndio, usiku wa kuamkia leo, miaka 53 iliyopita, yaani, Januari 12 , 1964, siku ya Jumapili, ndio ilikuwa Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mapinduzi ya Zanzibar ni sura ya kipekee katika kitabu cha historia ya Bara hili. Nimepata kuandika, kuwa kwetu sisi wa Bara, jambo la Zanzibar ni letu, imani hiyo pia iko visiwani, kuwa jambo la Bara ni lao.Tuko jirani mno na tuna historia ya pamoja. Ni ndugu wa damu.
Wengi wa wajumbe wa Baraza la kwanza la Mapinduzi ni wenye asili ya Bara. Ni watu wa aina ya Edington Kisasi, Hassan Nassoro Moyo, Abdalah Natepe na wengine.
Nimepata kuwa Zanzibar mara nyingi. Nimepata nafasi ya kuongea na WaZanzibar. Nimedadisi Mapinduzi yale ya 1964, nimedadisi Muungano wetu.
Na tujifunze kupitia historia. Nimeamini siku zote, kuwa historia ni Mwalimu Mzuri sana. Maana, hatuwezi kuyajua ya leo kama hatuyajui ya jana. Na hivyo, hatutoweza kupata mwanga kwa yatakayotokea kesho.
Shuleni nilipenda sana kusoma habari za Wanamapinduzi wa dunia hii. Kusoma habari za mapinduzi ya umma katika sehemu za dunia. Habari za Mapinduzi ya Zanzibar zilinivutia sana. Nilipata kusoma kitabu cha John Okello kilichonivutia sana kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar. Kiliitwa ' Zanzibar Revolution'.
Kupitia historia hiyo nilifahamu habari za wanamapinduzi; ni watu wa aina ya Abdurahman Babu, Edington Kissasy, Kassim Hanga na wengineo. Nilipomaliza Form Four pale Tambaza Secondary nilifanya safari ya kwanza maishani mwangu kuvuka bahari. Safari ya kwenda Unguja.
Huko nilikuwapo wakati wa sherehe za Mapinduzi Januari 12, 1989. Ni wakati wa utawala wa Dr Salmin Amour. Nilifurahia kuwapo mahala palipokuwa na vuguvugu la Mapinduzi ya mwaka 1964. Kuviona kwa macho na kutembea kwenye vitongoji vya Zanzibar; Mkunazini, Ziwani, Fuoni, Mji Mkongwe na kwengineko.
Mwandishi Ryszard Kapuchinski alikuwapo Dar es Salaam na Zanzibar wakati wa mapinduzi. Kapuchinski anaandika; kuwa Karume alikuwa Dar es Salaam wakati mapinduzi yale yakiendelea kule visiwani. Kapuchinski anamzungumzia Karume kama mtu aliyekuwa akiongea kwa sauti ya juu sana hata ukikaa nae karibu. Mara nyingi Karume alikuwapo pale New Africa Hotel, mahali walipokutana wanamapinduzi wengi wa bara hili.
Ninapotafakari mitazamo tofauti juu ya dhana ya Mapinduzi ya Zanzibar, na kwa vile nimepata bahati ya kufika visiwani na kuongea na WaZazibar na wa Mji Mkongwe na wa mashambani, kuna uhalisia ninaouona, kuwa suala la Zanzibar na hususan Muungano si jepesi kama wengine wanavyofikiri, au wanavyotutaka tufikiri.
Maana, Muungano ni zao la Mapinduzi ya 1964. Yale ya 1964 yalikuwa ni Mapinduzi ya Umma. Ni Mapinduzi ya Wajamaa wa Kiafrika. Ni muhimu watu wakajua historia sahihi ya Mapinduzi, lakini, yumkini swali muhimu leo si nani aliyewaongoza wakulima, wavuvi na wakwezi wale kufanya mapinduzi, bali, kuyafahamu malengo ya mapinduzi yale na kama yamefikiwa.
Naamini, kuwa kuuvunja Muungano leo ni kuvunja misingi ya uwepo wa Tanganyika kama dola. Kuna hasara kidogo sana kubaki kwenye muungano, na hasara na madhara makubwa zaidi kuwa nje ya Muungano.
Zanzibar ya jana, leo na kesho, itabaki kuwa ni mkusanyiko wa wenyeji wa asili mbali mbali. Na wengi ni Waafrika wa kutokea Tanganyika. Mathalan, Zanzibar ina WaZanzibar wenye asili ya Unyamwezi, Usukuma, Umakonde, Uluguru, Uzaramo, Undengereko, Urabau, Ushiraz na kadhalika. Hivyo basi, swali gumu ni je, Mzanzibar ni nani nje ya Muungano? Unafikiri haya unapokutana na Wazanzibar wenye kuongea Kinyamwezi lakini hawajawahi kukanyaga Sikonge wala Urambo, Tabora.
Bila shaka, Mwalimu Nyerere aliposema kama ingewezekana Zanzibar isogezwe na upepo iwe mbali na Tanganyika huenda ingekuwa nafuu, naye alikuwa akisumbuliwa na ukweli huo. Kuwa ni vigumu kwa Tanganyika kuondokana na Zanzibar katika uhalisia uliopo. Tulivyo sasa, suala la Zanzibar ni letu Tanganyika, na la Tanganyika ni la Zanzibar pia.
Yalikuwa malengo sahihi, ya waasisi wa Muungano kuwa uanze na Serikali MBILI kwa lengo la kwenda kwenye Serikali MOJA. Na kuunganisha vyama; Afro Shiraz na TANU ulikuwa ni mwanzo wa safari ya kuelekea kwenye kuyafikia malengo hayo. Maana, Serikali kibaraka wa Sultan iliyopinduliwa 1964 haikuwa na malengo ya kuukomboa umma wa Zanzibar ulio na mchanganyiko wa hata wenye asili ya Bara. Serikali iliyoundwa na ZNP na ZPPP ilikuwa ni mabaki ya Usultani ambao wanyonge walio wengi visiwani hawakuwa na faida nao.
Huu ni wakati wa kujitafakari. Ni wakati wa kujisahihisha pia. Kuyaacha malengo ya waasisi ya kuufikia Muungano Kamili wa Serikali MOJA kutoka kwenye Serikali MBILI, na kubadili mwelekeo kwenda kwenye Serikali TATU, kimsingi itakuwa ni kuianza safari ya kurudi Tanganyika na Zanzibar pasipo MUUNGANO.
Zanzibar inatokaje kwenye mkwamo huu wa kisiasa?
Tumesema, historia ni mwalimu mzuri. Itakumbukwa, kuwa baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 Maalim Seif alikaririwa akitamka kuwa; 'Hakuna tena mufaka wa tatu". Rais Karume naye akakaririwa akitamka; "Sitaki kusikia habari ya Serikali ya mseto".
Katika karne hii, tukubaliane, kuwa hakuna tena masuala ya ndani ya Tanzania , Zimbabwe, Uganda au Ushelisheli. Dunia imebadilika. Yanayotokea Mji Mkongwe Unguja na Micheweni Pemba yanaihusu Idara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, Shirika lake la ujasusi CIA na hata FBI. Tuiangalie dunia ya sasa kwa miwani hiyo.
Itakumbukwa baada ya Vita Kuu ya Pili, dunia ilipitia kipindi cha vita baridi . Miaka ile ya 60 dunia iligawanyika katika kambi mbili kubwa kiitikadi; zilijulikana kama Warsaw Pact na Nato Pact. Kambi ya Warsaw iliongozwa na Urusi ya zamani na ile ya NATO iliongozwa na Marekani. Kulikuwepo pia na kundi la nchi zisizofungamana na upande wowote. Tanzania ilikuwa mwanachama wa kundi hili. Hata hivyo, nyingi ya nchi hizi kimsingi zilikuwa na upande zilizoegemea kati ya makundi mawili niliyoyataja.
Tunasoma kuwa Marekani na hususan kupitia Shirika lake la ujasusi la CIA ilijiingiza kwa mara ya kwanza katika siasa za Zanzibar mara baada ya mapinduzi ya 1964 kwa lengo la kupunguza kasi ya kuenea kwa Ukomunisti. Marekani iliingiwa na hofu ya Zanzibar kama kisiwa kutumiwa na Wakomunisti. Katika Zanzibar bado kuna kumbukumbu ya historia hii kwa kuyaangalia majina kama Uwanja wa Mao Tse Tung, hospital ya V.I Lenin, shule za Fidel Castro, Patrick Lumumba na mengineyo. Yote haya yalikuwa na mwelekeo wa kambi ya Warsaw; Ukomunisti.
Mvutano wa kiitikadi kati ya Warsaw na NATO uliendelea kuwepo hadi pale ukuta wa Berlin uliopoangushwa Agosti 23, 1989. Huo ndio ulikuwa mwisho wa vita baridi ya dunia. Marekani ikabaki bila mpinzani wa kiitikadi. Kuanzia hapo upepo wa kisiasa uligeuka ghafla, wimbi la demokrasia ya vyama vingi likaanzia Ulaya Mashariki na kuikumba Afrika.
Kati ya mwaka 1990 hadi 1998 tulishuhudia kuwepo kwa ombwe la kiitikadi. Uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 1995 ulifanyika kukiwa na ombwe hilo la kiitikadi duniani. Miaka mitatu baadae, Agosti 7, 1998, sura ya dunia ilianza kubadilika. Ni mara ile balozi za Marekani Nairobi na Dar Es Salaam zilipolipuliwa. Septemba 11, 2001 sura ya dunia ilibadilika ghafla, pale kikundi cha kigaidi cha Alqaida kilipofanya maangamizi makubwa katika miji ya Washington na New York. Hii ni tafakuri endelevu..
Happy Mapinduzi Day!
Maggid Mjengwa,
Iringa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama) akifungua Kikao cha walimu alichokiitisha ili kuskiliza changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wakati wa ziara yake Wilayani Karatu.

Walimu wa shule za msingi na Sekondari wanaofanya kazi katika Halmashauri ya Karatu wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya kikazi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akiongea na walimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Karatu. 

Na Nteghenjwa Hoseah, Karatu 

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo kuhakikisha fedha za walimu wa shule za sekondari na msingi zilizokatwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwaajili ya vitambulisho vya kazi zinarudishwa. 

 Mhe. Gambo alitoa agizo hilo jana wilayani Karatu wakati alipokuwa akizungumza na walimu hao kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Karatu Boys ili kujua changamoto wanazokutana nazo na jinsi ya kuzitatua ikiwemo madeni ya likizo, upandaji wa madaraja. 

 Alihoji ni kwanini walimu hao wakatwe Sh. 6000 kwa ajili ya kutengenezewa vitambulisho vya kazi wakati ni haki yao kama watumishi na waajiriwa wa halmashauri hiyo na ni haki yao kupata vitambulisho vya kazi bure; Mwajiri anao wajibu wa kumtengenezea kila mtumishi Kitambulisho cha kazi.  Alimwagiza DC Mahongo kuhakikisha anafuatilia na kumchukulia hatua watumishi wa halmashauri hiyo waliowakata walimu hao wa msingi na sekondari kiasi hicho cha fedha kwa ajili kuwachukulia hatua.

Kwa habari kamili BOFYA HAPA(P.T)

media

Rais mteule wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano na vyombo vya habari, mjini New York, Januari 11, 2017.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump atakayechukua hatamu ya uongozi wa nchi Januari 20 amekutana kwa mara yake ya kwanza Jumatano hii na waandishi wa habari tangu achaguliwe Novemba 8.

Akionekana ni mwenye hasira dhidi ya vyombo vya habari, rais mteule wa Marekani amezungumzia masuala mbalimbali kama vile mahusiano yake na Urusi, kurejelea upya sera ya Obamacare, na mpango wake wa kujenga ukuta na Mexico.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameshutumu tangu mwanzo wa mkutano wake na waandishi wa habari, taarifa za uongo zilizosambazwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini Marekani kuhusu mahusiano yake na Urusi.

Mahusiano na Putin

Rais mteule wa Marekani pia amesema hakujua kama angeweza kuelewana na Putin lakini ana matumaini kuwa itakuwa hivyo. Bilionea huyo kutoka chama cha Republican anasema ni "jambo muhimu" kuona rais wa Urusi anakuwa upande wake. "Kama Putin anampenda Trump, ni vizuri, si tatizo lolote," amesema Bw Trump.

Trump aachana na kazi ya biashara

Rais mteule wa Marekani Donald Trump pia ametangaza kukata mahusiano na shughuli zake nyingi za kibiashara na kifedha kwa kuhamisha mali yake yote katika kampuni ya "Trust" inayosimamiwa na wanawe wawili.RFI

dstv-nape

Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na sanaa Kushoto,Diamond Platnumz katika pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania bw.Salum Salum.

dstv-nape-6

Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania Shumbana Walwa akiwa anaongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kumkabidhi Diamond Platnumz bendera ya Tanzania kuelekea katika ufunguzi wa Afcon nchini Gabon.

dstv-nape-3

Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bw.Alpha Joseph akimkalibisha Kaimu Mkurugenzi Salum Salum katika hafla ya utoaji wa Bendera kwa msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz.

salum

Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Bw.Salum Salum akimkaribisha mgeni wa tukio ambaye ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa Mh.Nape Nnauye hayupo pichani.

dstv-nape-1

Waziri wa Habri,Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh.Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari wakati wa kumkabidhi Bendera Diamond Platnumz anayekwenda kwenye shoo ya Ufunguzi wa Afcon nchini Gabon.

dstv-nape-8

Msanii Diamond Platnumz akitoa shukruni kwa Serikali na DStv pamoja na waandishi wa habari kwa mchango wao pamoja na kuendelea kumsapoti kupitia kazi zake.

dstv-nape-5

Mh.Nape Nnauye akisalimiana na Msanii Diamond Platinum.

dstv-nape-7

Msanii wa vichekesho nchini Tanzania JOTI ambaye pia ni balozi wa Kifurushi cha DStv Bomba ambacho kitarusha moja kwa moja Michuano ya Afcon akitoa pongezi kwa Kampuni ya Multichoice Tanzania.

dstv-nape-4

Waziri wa Habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa Mh.Nape Nnauye katika akiwa na balozi wa kifurushi cha Bomba Joti kulia pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Bw.Salum Salum kushoto wakiteta jambo.

dstv-nape-11

Baadhi ya Waandishi waliohudhuria tukio hilo wakiwa katika majukumu yao ya kuchukua picha.

dstv-nape-13

Msanii Diamond Platinum akiwa na bendera baada ya kukabidhiwa na Serikali tayari kuelekea kwenye ufunguzi wa Michuano ya Afcon inayoanza Jumamosi ya Januari 14.

dstv-nape-12

Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Nape Nnauye pamoja na Msanii Diamond Platinum.

PICHA NA MO DEWJIBLOG.

Kuelekea katika Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika ‘AFCON’ Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia Kifurushi cha DStv Bomba imetoa tiketi sita kwa vijana wa Msanii wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum kwenda kushuhudia ufunguzi huo.

Ufunguzi huo wa michuano hiyo mikubwa Afrika, inatarajiwa kufanyika Januari 14, mwaka nchini huko ambako Dimaond amealikwa kwenda kutuimbuza.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alimkabidhi bendera ya taifa, Diamond kwa ajili ya kwenda kuipeperusha vyema Tanzania katika ufunguzi huo.

“Kikuweli nimpongeze Diamond kwa mwaliko alioupata wa kwenda kutumbuiza kwenye michuano mikubwa Afrika ya Afcon, siyo kitu kidogo kwake, ni nafasi ya yeye kujitangaza zaidi kimataifa, ninaamini wapo wasanii wengi wazuri Afrika, lakini kachaguliwa yeye hivyo anastaili pongezi,” alisema Nape.

Nape ndiye aliwaomba DStv kujitokeza na kudhamini safari ya wachezaji shoo wa Diamond na baadhi ya watu wa timu yake kwenda Afcon ili kuhakikisha anafanya shoo ya uhakika zaidi.Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DStv, Salum Salum alisema wametoa tiketi hizo kwa Diamond kwa lengo kukuza na kuendeleza vema tasnia ya filamu.“Tunathamini tasnia ya sanaa nchini kwa kupitia muziki na filamu, hivyo basi katika kutambua hilo tumetoa tiketi sita kwa kundi la WCB chini ya msanii Dimaond kwa ajili ya kwenda kwenye uzunduzi wa Afcon huko Gabon.

“Tumempatia tiketi hizo, baada ya kuomba udhamini wa tiketi hizo kwa ajili ya vijana wake sita atakaombatana nao kwenye shoo hiyo na kikubwa tunataka kuona Diamond anafunika ili atauwakirishe vema,” alisema Salum.DStv, ndiyo itaonyesha michuano hiyo mikubwa ya kimataifa kwa kifurushi chake cha bei cha chini kabisa kitakachopatikana kwa Shilingi 19, 975 tu.(P.T)

Mfumo wa Uhifadhi Data, Nishati Jadidifu kuanzishwa

Published in Jamii

JADI 1

Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kushoto) akizungumza na mtaalam  kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Mobisol, Devis Mtete (kulia) mjini Kahama mkoani Shinyanga tarehe 11 Januari, 2017

JADI 2

Mtaalam kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Zola, Omary Raymond (katikati) akielezea shughuli za kampuni yake kwa Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kulia). Kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE) chini ya  Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele

Na Greyson Mwase, Kahama.

Wizara ya Nishati na Madini kupitia Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE: Capacity  Development  in the Energy Sector  and Extractive Industries), inatarajia kuanzisha mfumo wa uhifadhi data  kwa ajili ya nishati  jadidifu  ujulikanao kama  Tanzania  Renewable Energy Management  Information System (TREMIS)  utakaowezesha wawekezaji ndani na nje ya nchi  kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika  sekta ya nishati jadidifu.

Hayo yameelezwa na  Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE), Paul Kiwele katika ziara ya maandalizi ya mfumo huo jana, Kahama mkoani Shinyanga

 Kiwele alisema katika mfumo huo kutawekwa  taarifa mbalimbali kuhusu,  tafiti mbalimbali  na fursa za uwekezaji katika nishati jadidifu , sera, sheria na taratibu ili kuvutia wawekezaji kutoka  ndani na nje ya nchi.

“ Kupitia mfumo huu kutakuwa hakuna haja ya mwekezaji kutoka nje ya nchi kufunga safari  hadi  Tanzania kwa ajili ya kupata  taarifa,  taarifa zote zitakuwepo katika mfumo huu utakaounganishwa na tovuti ya  Wizara ya Nishati na Madini.

Akielezea maandalizi ya mfumo huo, Kiwele alisema kazi ya  maandalizi ya  taarifa kwa ajili kuwekwa kwenye mfumo huo imeshaanza kwa kushirikiana na Kitengo cha Teknolojia  ya Habari na Mawasiliano kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na kuzungumza na wauzaji na waendelezaji wa vifaa vya nishati mbadala katika  wilaya  ya Kahama, Shinyanga kwa ajili ya kupata taarifa zao.

Aliongeza kuwa kutakuwa na warsha itakayokutanisha  wadau mbalimbali wa nishati mbadala ili kupata maoni  yao kuhusu  taarifa zitakazojumuishwa katika mfumo huo.

Mradi wa CADESE unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Maendeleo (UNDP) ulianzishwa mwaka 2014 na unatekelezwa na  Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana n a  wadau wengine kama Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Taasisi ya Uongozi na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).(P.T)

CD

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) Seleman Jafo akipokea taarifa za maendeleo ya ujenzi wa madarasa shule ya msingi Chang’ombe ‘’A ‘’kutoka kwa Afisa mteule daraja la -I-  ambaye ni Fundi mkuu kutoka (JKT) Aluleyani Mapunda wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa shule ya msingi  hiyo unaofanywa katika kata ya Chang’ombe mjini Dodoma.

CD 1

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) Seleman Jafo akitoa shukrani zake za dhati baada ya kuridhishwa na utendaji wa kazi ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Chang’ombe A na ukarabati wa majengo ya shule wakati wa ziara aliyoifanya katika shule hiyo

CD 2

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)  Selemani Jafo akiwa na mwanafunzi George John wa darasa la saba ambaye ni mlemavu  na kutoa agizo kwa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma  Godwin Kunambi,kuhakikisha mradi wa ujenzi wa vyoo vya wanafunzi Shule ya Msingi Chang’ombe A unazingatia miundombinu rafiki kwa ajili ya watu wa ulemavu wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe.

CD 4

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo akipokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma  Godwin  Kunambi juu ya ukamilifu wa ujenzi wa choo cha walimu shule ya msingi Chang’ombe ‘B’ pia uendelevu wa ujenzi wa vyoo vya wanafunzi  katika ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe.

CD 3

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo akitoka kukagua ujenzi wa choo cha walimu katika shule ya msingi Chang’ombe ‘B’ wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe

CD 5

Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR-TAMISEMI) Selemani Jafo  akimalizia ziara yake kwa kukagua miundo mbinu ya majitaka katika shule ya msingi Chadulu.

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa wilaya nchini kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wanakwenda kuanza shule huku akiwasisitiza wazazi watakaoshindwa kuwapeleka shule watoto hao wachukuliwe hatua za kisheria.

Jafo ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara ya kukagua miundombinu mbalimbali katika shule za msingi, Chadulu, Chang’ombe A na B, Manispaa ya Dodoma.

Katika ziara yake ya kukagua maagizo aliyoyatoa kwenye shule hizo kuhusu masuala ya miundombinu, Jafo amesema  “Sisi kama serikali hatutaki mtoto akose elimu hasa katika kipindi hichi ambacho serikali imeamua kuelekeza nguvu za kutosha kwenye elimu kwa ajili ya watanzania.”

Ameongeza “Kwa mzazi ambaye mtoto wake atabainika hajaenda shule na kupewa kazi zingine kama kuendesha bodaboda hatua za kisheria zichukuliwe mara moja,”.

 Pamoja na hayo, Jafo amekemea tabia ya wazazi kutotilia mkazo masuala ya elimu na kuwakabidhi watoto wao kuendesha bodaboda kama ajira yao badala ya kuwapeleka shule na kuwataka kuhakikisha wanawanunulia mahitaji yote ya shule.

Aidha amesema serikali haitarajii kuna vijana waliochaguliwa wakishawishiwa na wazazi kufanya vibaya kwenye mitihani kutokana na elimu kuwa ni bure.

Akizungumzia kuhusu watoto walioandikishwa kuanza kusoma elimu ya awali na msingi, Jafo amesema kumekuwepo na mwitikio mkubwa katika suala la uandikishaji watoto hao na linatokana na uwepo wa elimu bure.

Hata hivyo, amesema shule nyingi idadi ya wanafunzi imeongezeka zaidi na kwa serikali ni faraja kuona watanzania wengi sasa wanapata elimu huku akiwataka wazazi wahakikishe watoto walioandikishwa wanahudhuria shule ipasavyo  na wakurugenzi kuendelea kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.

Kadhalika, Jafo ameridhishwa na ukarabati wa miundombinu mbalimbali kwenye shule hizo huku akiwaahidi walimu kuwa serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufundishia ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi, amesema kwasasa Manispaa hiyo inaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja ujenzi wa shule za msingi na sekondari na kuongeza madarasa kwenye baadhi ya shule ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi hasa wanaohamia Dodoma.

 Kwa upande wake, Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo, Scholastika Kapinga, amesema hadi sasa watoto zaidi ya 8,000 wameandikishwa kwenye manispaa hiyo kuanza kusoma elimu ya awali na msingi.(P.T)

Taarifa kwa Umma Kuhusu Siku ya Kufanya Mazoezi

Published in Jamii

Displaying Taarifa kwa umma.jpegDisplaying Taarifa 2.jpeg

Sabodo: Ukaribu wangu na Mwl. Nyerere uliokoa Taifa

Published in Jamii

 Mfanyabiashara maarufu, Mustafa Jaffar Sabodo

 Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere

Aliyekuwa Kiongozi wa Taifa la Iran, Ayatolah Khomein 

Mwandishi Wetu

HAKIKA ukitaja jina la Mustafa Jaffer Sabodo, siyo geni masikioni mwa Watazania wengi.

Hii ni kutokana na mchango wake kwa jamii katika kuliondoa taifa kutoka sehemu moja ya chini kwenda juu, yaani maendeleo.

Sabodo mfanyabiashara maarufu ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Asia amekuwa akitoa mchango kwa maendeleo ya Taifa katika nyanja mbalimbali kuanzia za uchumi, siasa, elimu, afya na maji.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni mzaliwa wa mkoani Lindi takriban miaka 73 iliyopita amejitolea kujenga shule mbalimbali nchini, hospitali, visima vya maji hata kufadhili shughuli za kisiasa na kiuchumi.

Michango yake hiyo kwa jamii ya Watanzania, imefanya jina lake kuandikwa katika mioyo ya wananchi wengi kwani alidhirisha tabia yake isiyojificha ya uzalendo kwa Taifa lake Tanzania.

Sabodo anatajwa kuwahi kuvifadhili vyama vya siasa vya CCM na Chadema kwa nyakati tofauti.

Pia anatajwa kwamba alikuwa rafiki wa karibu wa Mwalimu Julius Nyerere na wanasiasa mbalimbali nchini hata kuwahi kutumwa kwenda nchini Iran kukutana na kuomba mafuta kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo la Kiislamu, Ayatolah Khomein katika miaka ya 1970 baada ya taifa kukumbwa na uhaba wa mafuta uliochagizwa na sababu mbalimbali ikiwamo ukosefu wa fedha za kigeni.

Hali hiyo ilitokea kipindi hicho wakati dunia ilikuwa bado ikishuhudia mgawanyiko kwa baadhi ya nchi kuegemea Marekani kisiasa na kimfumo, nyingine zikifuata mfumo wa iliyokuwa Muungano wa nchi za Kisovieti za Urusi (USSR).

Si hivyo tu kwa kusoma alama za nyakati, baadhi ya nchi zilikaa kando na utengano huo na kuanzisha Jumuia ya Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote.

Miungoni mwa mataifa yaliyofuata siasa za kutofungamana na upande wowote, Tanzania wakati huo chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa mojawapo.

Tofauti hizo za kisiasa hata kidini kati ya mataifa zilisababisha athari zilizozaa tofauti ya hali hasa kiuchumi na kisiasa hata baadhi ya nchi kuingia kwenye mahangaiko ikiwamo Tanzania iliyokumbwa na uhaba wa mafuta ya Petroli na fedha za kigeni.

Sabodo anasimulia kwamba kufuatia hali hiyo iliyoilazimu Serikali kuzuia magari yake kutembea Jumapili huku Jumamosi yakitembea hadi saa nane mchana, alipata nafasi ya kukutana na Rais Nyerere.

Anasimulia kwamba katika mazungumzo hayo alimwabia Rais Nyerere haja yake ya kutaka kwenda Iran kuomba mafuta.

“Nikamwambia wacha niende Iran. Nilifanya hivyo nikiamini Khomein atanisikiliza. Nakumbuka nilikwenda na Chifu Adam Sapi Mkwawa,” anasema.

Anasimulia: “Mimi ni Khoja, Mwislamu wa dhehebu la Shia na Khomein pia, nilipokutana naye, nikamwambia wanaoteseka Tanzania kwa shida ya mafuta wamo piaWaislamu wa Shia wengi tu.”

“Nilimwambia Tanzania ni nchi nzuri haina ubaguzi na Rais Nyerere ni mtu mwema, hata Waziri Mkuu wake ni Rashid Kawawa na Waziri wa Madini na Mafuta ni Anoor Kassam, nikamwangukia miguuni nikiliaa kuomba aipe nchi yetu mafuta, akakubali” anakumbuka Sabodo.

Hata hivyo, anasema licha ya kukubali, Khomein  akasema hawezi kumpa mafuta yeye Sabodo hadi watu wa Serikali ya Tanzania watakapofika Iran kuthibitisha ombi hilo.

“Nikarudi Tanzania na kumpa taarifa baba wa Taifa naye alimwambia Kawawa na John Malicela ikakubalika tukaenda tena Iran safari hii nikiwa na mawaziri wa Fedha, Cleopa Msuya, Anoor Kassam wa Mafuta na Usafirishaji pia alikuwepo Peter Noni kwa niaba ya Benki Kuu na Adam Sapi Mkwawa,” anasema.

Sabodo anakumbuka kuwa safari hiyo ilizaa matunda kwani Khomein aliipa Tanzania mafuta yenye thamani ya Dola za Kimarekani 80,000.

“Nakumbuka hapo urafiki wangu na Nyerere uliniwezesha kuliokoa Taifa kwa kupata mafuta baada ya kunituma kwenda Iran nilipomshauri,” anasema Sabodo ambaye wazazi wake alizaliwa Lindi.

Anakumbuka kuwa pia katika safari hiyo alimshauri Khomein kufungua ofisi ya Ubalozi wa Iran nchini naye alikubali na alifanya hiyo pia kwa Zambia, Tanzania nayo ikafungua ubalozi Iran.

Don’t forget to read my book; CORRUPTION IS CRUCIFICATION OF TANZANIA, which is in process(P.T)

The Obama`s are getting ready to pack their bags to move out of the White House as Barack Obama is near the end of his journey as President of America. He has been in the White House for seven years and has made four state visits to the continent of Africa. The question is, will Africa be disappointed that there will not be a fifth?
2009 was the year that Barack Obama moved in to the White House, but also the year when China surpassed USA in trade relations with Africa. That did not hamper Obama from.. Read more..http://www.africablogging.org/…/will-africa-miss-the-obamas/(P.T)

Mama Na Mwana!

Published in Jamii

Furaha ya mzazi ni kuwa karibu na mtoto au watoto wake.
Ni zawadi kubwa kwetu kila wakati tunapoungana na wana wetu. Na tuamini pia, mzazi ni mwalimu, na mtoto pia. Binafsi, hujifunza mambo mengi kutoka kwa wanangu. Hutokea pia fikra zangu kuzijaribu kwa wanangu kutaka ushauri wao. Ni hawa pia, kwa urafiki wetu wa kweli, kama nimefikiri jambo la kijinga , najua wataniambia; " Baba hapa umechemsha!". 
Maggid.(P.T)

Na Judith Mhina – MAELEZO

“Wakati umefika wa kujenga makumbusho ya Taifa ya Mapinduzi ya Zanzibar, ili kizazi cha sasa na kijacho waweze kujifunza na kuipitia historia muhimu kwa Watanzania na wageni kutoka nje.

Hayo ni maneno ya msingi ambayo yamesemwa na Dkt Mohammed Seif Khatibu wakati wa mahojianno yake na Idara ya Habari MAELEZO mapema mwishoni mwa wiki.

Dkt Khatib alisisitiza “Ni vema kuonesha katika picha, maandishi na sura halisi za historia ya Zanzibar kabla yaani wakati wa Waajemi, Wareno, Waarabu, Waingereza na sasa Serikali ya Mapinduzi”.

Dhamira ya makumbusho hayo, Dkt. Khatib amesema “Vijana wengi ukiwaambia nchi hii kulikuwa na unyanyasaji wa Waafrika hawakubali maana hawajui historia, waelezwe kwa nini tuko huru, kuna wasioitakia mema Zanzibar wanapotosha historia hiyo”.

Kumbe kwa kuweka makumbusho na usahihi wa historia ya nyuma kabla, wakati, baada ya Mapinduzi na yanayotokea sasa, hayo yote yakiwa katika makumbusho yatakuwa msingi wa historia ya Zanzibar hatua ambayo itasaidia kuwekwa wazi mambo yaliyowahi kutokea, hivyo sio rahisi kwa mtu yoyote ambaye ana agenda ya kupotosha umma kufanya hivyo.

Lakini kwa sasa ni kweli kabisa mtu yoyote anaweza akasema vyovyote atakavyo kwa kuwa hawajui historia na wala hawana mahali pa kurejea historia ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Watu walitoka Kongo, Malawi, Kigoma na Tabora wakibebeshwa pembe za Ndovu na kusafiri kwa mguu, wakifuata njia ya reli ya kati, mpaka Bagamoyo na kusafirishwa na boti mpaka Unguja na kuwekwa sokoni kuuzwa kama samaki katika soko la watumwa. Huu ndio ukweli” alisema Dkt Khatib.

Tuchukulie mfano wa jirani zetu Rwanda walikubwa na mauaji yakimbari mwaka 1994, kwa kutambua kuwa hicho siyo kitu kizuri kutokea tena hapa duniani wameona waweke makumbusho ya kitaifa. Inahuzunisha lakini ndio ukweli, unapoona yale mafuvu ya vichwa yalivyopangwa huwezi kuamini kama hiyo ni hali halisi iliyotokea hapa duniani.

Kwa Wanyarwanda na watu wengine duniani, makumbusho kimbari ni sehemu ya Utalii ikizingatia msemo wa waswahili wanasema kuona ni kuamini.

Siyo hiyo, tu hata kule Namibia kuna jumba la makumbusho la mauaji yaliyofanywa na wajerumani kwa kabila la Waherero waliuwawa katika vita ya kwanza ya dunia. Takribani Waherero nusu ya milioni waliuwawa na hivi karibuni Waherero wa Namibia walikuwa wanaomba fidia kwa Serikali ya Ujerumani, ingawa Ujerumani wameomba msamaha kwa mauaji hayo ya kimbari.

Uingereza ni nchi inayoongoza duniani kwa kuweka kumbukumbu zake katika makumbusho za Kifalme, Kimataifa, Kitaifa, Vita, Silaha, Bahari, Mtu Binafsi, Jiji au Mji husika. Uingereza ina zaidi ya makumbusho 55 ambayo yanafahamika duniani. Mfano “British Museum London, Natural History Museum London, National Gallery London, Science Museum London, Victoria and Albert Museum, National Maritime Museum, Museum of London City, National Portrait Gallery, National Army Museum, Sir Johns Soanes Museum, Wallace Collection London, National War Museum nk”

Hivyo, tuunge mkono wazo hilo na tushirikiane wote kama Watanzania kuhakikisha kituo hicho cha makumbusho kinajengwa na kuhifadhi kila kinachohitajika ili kukamilisha historia husika.

Kujengwa kwa kituo cha makumbusho Zanzibar kitasaidia kuingizia fedha kama sehemu ya Utalii wa historia ambapo mtu anayehitaji kuijua historia hiyo atapata kila kitu mahala pamoja bila kusumbuka. Mungu ibariki Tanzania “MAPINDUZI DAIMA”.(P.T)

UTEUZI WA MKURUGENZI WA MAENDELEO YA MICHEZO

Published in Jamii

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo Omari

kawa1

MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo,Dk.Shukuru Kawambwa akizungumza na wanachama wa vikundi vya ujasiriamali vya jipe moyo na kiroho safi,vilivyopo Mwavi kata ya Fukayose,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)

kawa2

MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo,dk.Shukuru Kawambwa akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mkenge kata ya Fukayose,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo,
.(Picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo

MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo,dk.Shukuru Kawambwa ameelekeza nguvu zake katika ujenzi wa madarasa katika shule mbalimbali jimboni humo ambapo amechangia zaidi ya mifuko 1,000 ya saruji.

Aidha ametoa zaidi ya sh.mil.10 kuchangia vikundi viwili vya ujasiriamali kwenye kila kata kwa ajili ya kukopeshana ambapo kati ya vikundi hivyo vimewezeshwa sh.mil.1 hadi mil.1.5.

Hayo aliyasema kijiji cha Mwavi,Mkenge na Fukayose wakati wa ziara yake inayolenga kupeleka mrejesho kwa wananchi kuhusiana na hatua anazozichukua kufuatilia kero zao zinazowakabili.

Dk.Kawambwa alisema jimbo hilo lina jumla ya kata 11 na kila kata ameichangia kati ya mifuko 100-150 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa .

Alieleza kuwa amehakikisha mfuko wake wa jimbo unajikita kuunga mkono juhudi za wananchi kwenye ujenzi huo na kuwezesha wajasiriamali.

Mbunge huyo alisema,ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona bado shule nyingi zinapambana na changamoto ya uhaba wa madarasa na vikundi kukosa mitaji.

Hata hivyo,dk.Kawambwa aliahidi kutoa matofali 1,000 katika kitongoji cha Kalimeni na kwa kijiji cha Kitopeni ameshawapa ardhi yenye heka 6 na fedha kwa ajili ya kujenga shule na tayari wameanza .

“Nimeona suala la madawati limemalizika vizuri kwa ushirikiano wa wadau,halmashauri na ofisi ya wilaya ya Bagamoyo,tumevuka kwa hili lakini tatizo ni majengo “

“Nitaelekeza nguvu zangu katika ujenzi huu kulingana na uwezo uliopo pamoja na kusupport akina mama na vijana kwenye vikundi vyao”alisema dk.Kawambwa.

Aliiomba jamii washirikiane kwa pamoja kwenye ujenzi wa madarasa ili kufanikisha lengo lao la kuondokana na upungufu wa madarasa.

Akizungumzia jambo la ujasiriamali aliwaomba wananchi wajishughulishe na kutumia fursa zilizopo ikiwemo mikopo kutoka kwa mbunge,halmashauri ili kujiendesha kimaisha.

Nae diwani wa kata ya Fukayose,ambae pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo,Ally Ally Issa,alivitaka vikundi vya ujasiriamali kurejesha mikopo kwa wakati.

Alisema kwasasa vikundi ambavyo havina uaminifu havitofumbiwa macho na vitachukuliwa hatua za kisheria.

Ally alisema mitaji haitoshi lakini halmashauri hiyo imeshawezesha vikundi mbalimbali kuanzia sh.mil.2 hadi mil.4 kulingana na vigezo vilivyopo na namna kikundi kinavyorejesha .

Alisema inakabiliwa na tatizo kubwa la maji,migogoro ya wakulima na wafugaji,miundombinu ya barabara kuwa korofi ikiwemo barabara ya kuelekea Mkenge na zahanati ya kijiji cha Fukayose kukosa gari la wagonjwa /maabara na upungufu wa nyumba za walimu .(P.T)

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Nyamikoma Wilayani Busega wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kisesa mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Magu mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.

. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU.(P.T)

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA