Kuna watembeleaji 209  wapo online

Magazeti ya Leo

Kwa habari na mambo ya kijamii, siasa, biashara, uchumi, michezo nk, sikiliza LIVE kwanza Radio.

 

 

Matangazo Mapya

Azania Bank Limited is the first indigenous private bank, formerly kno ...

Shambulizi jengine lawauwa watu 13 kenya

Published in Jamii

Mashambulizi katika eneo la Mpeketoni kenya

Takriban watu 13 wanahofiwa kuuawa katika mashambulizi mawili katika pwani ya Kenya karibu na mpaka wa Kenya na Somali.

Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu tisa wameuawa katika shambulizi lililotekelezwa katika eneo la Gamba kaunty ya Tanariver ,huku wengine wanne wakifariki katika shambulizi kali la ufyatulianaji wa risasi karibu na kituo cha kibiashara cha Kaunty ya Lamu.

Shambulizi la pili lilitekelezwa karibu na eneo la Mpeketoniambapo zaidi ya watu sitini waliuawa mwezi uliopita.

Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi hilo bila ya kutoa maelezo zaidi.

Mwandishi wa BBC nchini kenya amesema kuwa kuna polisi wengi katika maeneo ya pwani kufuatia shambulizi hilo la mwezi uliopita.(P.T)

UHOLANZI YAING'OA KWA MATUTA COSTA RICA

Published in Michezo

UHOLANZI imetinga Nusu Fainali kwa ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana na Costa Rica ndani ya dakika 120 usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Dunia nchini Brazil.

Baada ya timu yake kupelekeshwa kwa dakika 120 na Costa Rica na kushindwa kupata bao, kocha Louis van Gaal alimuingiza kipa wa Newcastle, Tim Krul kwa ajili ya penalti.

Krul alipasha misuli yake moto haraka na kwenda kumbadili Jasper Cillessen dakika ya 118, kisha akaedna kuokoa penalti mbili kuipelekea nchi yake Nusu Fainali ya michuano hiyo.

Super sub: Holland's Tim Krul makes the decisive save to deny Costa Rica's Michael Umana in the shoot-out

Kipa wa Uholanzi, Tim Krul akipangua penalti ya nne ya Costa Rica iliyopigwa na Michael Umana na kuipeleka Uholanzi Nusu Fainali

Krul aliokoa penalti ya pili ya Costa Rica  iliyopigwa na mchezaji wa Fulham, Bryan Ruiz na ya nne iliyopigwa na Michael Umana.

Raha zaidi ni kwamba, Nahodha Robin van Persie, Wesley Sneijder, Arjen Robben na Dirk Kuyt wote wakafunga penalti zao na sasa Uholanzi itakutana na Argentina katika Nusu Fainali.

Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen/Krul, dk120, De Vrij, Vlaar, Martins/Huntelaar dk105, Kuyt, Wijnaldum, Sneijder, Blind, Robben na van Persie, Depay/Lens dk76. 

Costa Rica: Navas, Gamboa/Myrie dk78, Acosta, Diaz, Gonzalez, Ruiz, Borges, Tejeda/Cubero dk97, Bolanos, Campbell/Urena dk66 na Umana. (P.T)

Neymar amesafirishwa kwa helikopta kupelekwa Sao Paulo kuanza mapumziko

NYOTA wa Brazil, Neymar anaamini timu yake itashinda Kombe la Dunia bila ya kuwa na yeye.
Mchezaji huyo wa Barcelona aliaga mashineano hayo juzi usiku baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Colombia, Juan Zuniga.

Mchezaji huyo ameelezea maumivu yake baada ya pigo hilo linalomuondoa Kombe la Dunia mapema akiiacha timu yake imetinga Nusu Fainali na zaidi amewatakia heri wachezaji wenzake wabakize kombe hilo nyumbani.

Neymar amesafirishwa kwa helikopta baada ya tiba ya awali na kupelekwa Sao Paulo kuanza mapumziko. Tayari FIFA imesema inalifanyia uchunguzi tukio hilo kabla ya kumchukulia hatua Zuniga.

Safe journey: Neymar with the president of the Brazilian Football Condederation Jose Maria Marin

Neymar akipewa pole na Rais wa Shirikisho la Soka Brazil, Jose Maria Marin(P.T)

Ni timu ya taifa ya Zaire, sasa DR Congo. Ni world cup ya 1974 Ujerumani. Pichani mabeki Mwepu Ilunga na Boba Lobilo wakimkabili mshambuliaji Edu wa Brazil. Ukiiangalia jezi ya Edu utaona ina nyota tatu. Kwenys jezi ya Brazili nyota huwa na maana ya idadi ya makombe ya dunia waliyotwaa. Kwa sasa jezi ya Brazil zinasomeka nyota tano...! ( Picha ya maktaba ya Mjengwablog.com)
Maggid
Iringa.(P.T)

JE WAJUA?

Published in Michezo

JEZI_af8dc.jpg

Unajua kwa nini baadhi ya timu zinazoshiriki ama zilizoshiriki Kombe la Dunia la FIFA huwa na nyota kadhaa kwenye nembo za vyama vyao vya kabumbu?

Timu hizo huweka idadi ya nyota sawasawa na idadi ya mataji ya ubingwa wa dunia wanayoyashikilia. Hivyo, nyota hizo, huwa nishani ama heshima kwa kutambua ubingwa wa nchi husika.

Brazil huweka nyota tano kwa kuwa ndiyo idadi ya mataji ya kombe la dunia inayoyashikilia. Timu za Ujerumani, Ufaransa, Argentina na Uingereza nazo huweka nyota sawasawa na idadi ya mataji yao.

Wadadisi wengine wanaweza kustaajabishwa na jezi ya Uruguay yenye nyota nne ilhali ni wazi wameshinda kombe la dunia mara mbili tu, 1930 na 1950. Jibu ni kuwa, nyota mbili zingine zinawakilisha ubingwa wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 1924 na 1928 ambayo FIFA inautambua ubingwa wake kama ubingwa wa dunia.

Kuvaa huko kwa jezi zenye nyota hakujatokea tu. Kunatokana na Kifungu cha 18.2 cha Kanuni za Vifaa za FIFA. Kifungu hicho kinaruhusu wanachama wa FIFA waliowahi kushinda kombe la dunia kuweka alama kwenye jezi zao kama kielelezo cha ushindi huo.

Si hivyo tu, vilabu kadhaa vya soka ulimwenguni pia huweka nyota kama kielelezo cha mafanikio yao katika kabumbu. Nottingham Forest ya Uingereza huweka nyota mbili kutokana na mafanikio yao makubwa ya kushinda ubingwa wa Ulaya (sasa UEFA Champions League) mara mbili mfululizo, 1979 na 1980. Klabu ya Aston Villa yenyewe imeweka nyota moja ya rangi ya fedha kama kielelezo cha mafanikio waliyoyapata mwaka 1982.

Vile vile, Juventus ya Italia huweka nyota. Nyota yao moja huwakilisha mataji 10. Hivyo kwa mataji yao 30 wanazo nyota tatu.

Kwa Afrika, timu za taifa zilizowahi kushinda michuano ya Mataifa ya Afrika huweka nyota pia. Misri huweka nyota saba idadi sawa na mataji yao.Ghana na Cameroon huweka nyota nne kila mmoja huku Zambia wakiweka nyota moja baada ya ushindi wao wa mwaka 2012. Lakini nyota hizi hazivaliwi timu hizi zinaposhiriki michuano ya Kombe la Dunia la FIFA.

Huko Asia, Japan huweka nyota nne kielelezo cha ushindi wao mara nne wa michuano ya Asia.

Haya ndiyo yahusuyo nyota tuzionazo katika jezi za timu za taifa.

Nakutakia utazamaji mzuri wa kandanda dakika chache zijazo.(E.L) SOURCE FADHY MTANGA

FIFA yaipa Nigeria siku tatu

Published in Michezo

 

Victor Moses wa NIgeria katika Kombe la Dunia akivutana na Yohan Cabaye wa Ufaransa
 

Shirikisho la Kandanda la Dunia, FIFA, limeionya Nigeria kwamba itatolewa katika kandanda ya kimataifa iwapo serikali haitalirejesha tena shirika la kandanda la Nigeria, Nigerian Football Federation, ifikapo Jumaane juma lijalo.

Siku ya Alkhamisi serikali iliifuta Nigerian Football Federation na Ijumaa rais wa shirika hilo alikamatwa baada ya kurudi kutoka Kombe la Dunia.

 

Nigeria ilishindwa kwenye mechi na Ufaransa na hivo kukosa kuingia katika robo-fainali.

FIFA imesema imetiwa wasi-wasi na hatua ya serikali ya Nigeria dhidi ya chama cha kandanda cha nchi hiyo.

Kanuni za FIFA zinaeleza wazi kuwa wanachama wake lazima waruhusiwe kufanya kazi yao bila ya kuingiliwa kati na serikali.

Wakuu wa Nigeria wamekifuta chama cha kandanda cha taifa na piya kumkamata rais wa chama; na waziri wa michezo amemteua mkurugenzi wake kuongoza chama hicho.

Haijulikani sababu ya serikali ya Nigeria kufanya hivyo.

Lakini iwapo serikali haitabadili uamuzi wake basi Nigeria haitaweza kushiriki katika mechi za kimataifa, mazoezi na kadhalika.(A.I).

argentina_d445b.jpg

Goli la Gonzalo Higuain laipeleka Agrentina nusu fainali Kombe la Dunia 2014
Argentina 1-0 Ubelgiji (E.L)

MLIPUKO WAUA WANNE MOGADISHU

Published in Jamii

mlipuko_9db99.jpg

Mlipuaji wa kujitoa mhanga ameua watu wasiopungua wanne karibu na bunge la Somalia, kwa mujibu wa polisi na vyombo vya habari nchini humo.
Taarifa zinasema bomu hilo lililipuka nje ya lango kuu la kuingilia bungeni baada ya walinzi kumpiga risasi mlipuaji huyo.
Taarifa moja imekariri kundi la al-Shabab ikipongeza "shambulio la kafara".
Al-Shabab walipoteza udhibiti wa Mogadishu mwaka 2011, na tangu wakati huo wamekuwa wakifanya mashambulio kadha wa kadha.(E.L)

Kiongozi wa Brotherhood afungwa maisha

Published in Jamii

Mohammed Badie pamoja na mahabusu wenzake wa Muslim Brotherhood

Mahakama moja nchini Misri imempatia kifungo cha maisha jela kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie na wanachama wengine 36.

Watu hao walipewa hukumu hiyo kwa kuchochea ghasia na kufunga barabara wakati wa maandamano baada ya jeshi kumpindua aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi mwaka uliopita.

Mohammed Badie

Bwana Badie tayari anakabiliwa na hukumu nyengine ya kifo kutoka kesi nyengine .

Mahakama hiyo ya mjini Cairo pia iliwahukumu vifo wanachama wengine kumi wa kundi la Muslim brotherhood.

Makundi ya haki za kibinaadamu yamekosoa misururu ya hukumu za kifo nchini Misri yakisema zilishinikizwa kisiasa.

CHANZO BBC Swahili.(MC)

Bomu laua wanne nje ya Bunge Somalia

Published in Jamii

 

Wapiganaji wa Al Shabaab

Bomu lililotegwa kwenye gari limelipuka na kuua watu wanne karibu na Bunge la Somalia na wengine kujeruhiwa, maafisa wa Polisi wamesema.

Habari zanasema bomu hilo lilipiga nje ya lango kuu la kuingia katika majengo ya Bunge la Somalia baada ya askari kumrushia risasi mtu anayedaiwa kulipua bomu hilo.

Mshambuliaji aliyejitolea mhanga pia alikufa, alipolipua gari lake, baada ya kukataliwa kuingia kwenye eneo la bunge.

Kabla ya hapo, mshambuliaji huyo alijaribu kuingia katika wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, lakini alizuiliwa.

Majeshi ya AMISOM yakionyesha silaha walizopokonya kutoka kundi la Al Shabaab

Taarifa zilizonukuliwa kutoka kundi la kigaidi la Al Shabaab zinasema wapiganaji hao walifanya shambulio la kujitoa sadaka.

Wapiganaji hao Waislamu wamelaumiwa kwa shambulio hilo. Al-Shabaab ilisema itazidisha mashambulio wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Mlipuko mwingine uliofanywa na waasi hao katika majengo ya bunge mwezi Mei uliua watu 10.

Kundi la Al shabaab lilipoteza udhibithi katika mji mkuu wa Mogadishu tangu mwaka 2011 na tangu wakati huo limekuwa likiendesha mashambulizi ya mabomu na kufanya mauaji.

Mapema wiki hii Mbunge maarufu Ahmed Mohamud Hayd, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mji huo, katika shambulio linalodaiwa kufanywa na Al Shabaab.

CHANZO; BBC Swahili..(MC)

Kijana wa Kipalestina alichomwa

Published in Jamii

 

Wapalestina wakaa nje ya nyumba yao huku askari wa Israel wanapiga doria mjini Hebron, Ufukwe wa Magharibi
Ripoti kutoka Ufukwe wa Magharibi unaokaliwa na Israel zinasema kuwa ukaguzi wa awali wa mwili wa kijana wa Kipalestina aliyeuwawa juma hili mitaa ya mashariki ya Jeusalem, unaonesha kuwa kijana huyo alichomwa moto akiwa hai.

Wakuu wa Israel wanasema hawajui hasa vipi kijana huyo wa miaka 16 aliuwawa.

Familia yake inaamini aliuliwa kulipiza kisasi mauaji ya vijana watatu wa Israel mwezi uliopita.

Shirika la habari rasmi la Palestina (Wafa) lilimnukuu mkuu wa sheria akisema kuwa 90% ya mwili wa Mohammad Abu Khdair ulikuwa umeteketea.

Shirika hilo linaripoti kuwa afisa wa Palestina alikuwako kwenye ukaguzi huo wa matabibu, na jivu lilikutikana ndani ya kifua cha Abu Khdair ambayo inamaanisha alivuta moshi wakati akiuungua, yungali hai.

CHANZO; BBC Swahili.(MC)

DEREVA ASIYE NA MIKONO AKATAZWA KUENDESHA GARI

Published in Jamii

nbnb_95ad9.jpg

Polisi nchini China wamemkamata mtu asiyekuwa na mikono akiendesha gari. Bwana huyo Wo Guo (45) si tu kwamba hakuwa na leseni bali alikuwa akitumia mguu wake wa kulia kubadili gia huku mguu wa kushoto ukikanyaga mafuta na breki.
Msemaji wa polisi amesema: "Ni jambo la ajabu, lakini ni hatari sana kwake kuendesha gari." Polisi huyo amesema itakuwa vyema kama ataajiri dereva wa kumuendesha. Gari la bwana Wo linashikiliwa na polisi ili kumzuia asiendelee kuendesha.
Picha na taarifa kutoka Metro na CEN. (E.L)

(MC)

(MC)

Ruaha nitarudi tena...!

Published in Jamii

Nimekuwa na wakati mzuri sana wa mapumziko nikiwa na team yangu hapa Ruaha na hususan Ruaha Hilltop Lodge. Muda huu naianza safari kurudi Iringa. Ni mwendo wa saa 2 na nusu kutoka Ruaha.
Asanteni sana kwa kuwa nami...(MC)

Maggid.
Ruaha.

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

Maoni ya Wanakijiji

Zilizosomwa Zaidi

BLOG SHABIHANA