We have 447 guests and no members online

Matangazo Mapya

We provide the full IT solutions including web design, web development ...

uboyo

 Kamanda Muroto akiingia ndani ya nyumba wanayoishi wana JKT katika Kambi yao ya Lugwadu.

 Kamanda Muroto (wa tatu kushoto) na Makamanda wezake wakiwa katika nyumba wanayohishi  wana JKT.

 Mwenyekiti wa wana JKT,Palale Kiwango (kushoto) akizungumza na Makamanda eneo la shamba la Mahindi, Mbaazi na Karanga.

 Wana JKT kazini.

 Mwenyekiti wa wana JKT,Palale Kiwango (kushoto) akizungumza na Kamanda Muroto.

 Mwenyekiti wa wana JKT,Palale Kiwango (kushoto) akizungumza na Makamanda waliowatembelea.

 Kamanda Muroto na wezake wakikagua bustani ya mboga.(P.T)

Read more...

Rais Bush na mkewe walazwa hospitalini

Published in Jamii

Rais wa zamani wa Marekani George Bush na mkewe Barbara

Rais wa zamani wa Marekani George Bush na mkewe Barbara

Rais mstaafu wa Marekani George HW Bush aliyekuwa amelazwa hospitalini huko mjini Texas tangu Jumamosi, amepelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Baada ya kutibiwa ugonjwa wa homa ya mapafu, Bush mwenye umri wa miaka 92 sasa anaendelea vizuri.

Mke wake Barbara, amelazwa katiaka hospitali hiyo hiyo kama tahadhari kwa sababu ya uchovu.BBC

kabwe

Mkurugenzi wa Internews Bw.Wence Stanslaus akiongea na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali katika mjadala wa sheria ya Mtandao na Takwimu

Mmoja wa wadau wa habari (kulia) akiwasilisha mada katika mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania.

Mmoja wa wadau wa habari (kulia) akiwasilisha mada katika mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania.

Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania.

Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania.

Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania.

Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi ya Internews Tanzania.

Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Wamiliki na Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (TBN-Bloga ) akiwa katika mjadala huo.

Sehemu ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Wamiliki na Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (TBN-Bloga ) akiwa katika mjadala huo.

Mmoja wa wadau wa habari (katikati) akiwasilisha mada katika mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi wa Internews Tanzania, Wenceslaus Mushi.

Mmoja wa wadau wa habari (katikati) akiwasilisha mada katika mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi wa Internews Tanzania, Wenceslaus Mushi.

Mwanasheria na Mwanahabari, James Marenga akiwasilisha mada kwa washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika majadiliano ya Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria na Mwanahabari, James Marenga akiwasilisha mada kwa washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika majadiliano ya Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu katika vikundi leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mjadala wa pamoja kati ya wanahabari na wawakilishi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakijadili Sheria ya Mtandao na ile ya Takwimu leo jijini Dar es Salaam.(P.T)

 

JAJI1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman. 

JAJI2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha  Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman. 

JAJI3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi  baada ya kumuapisha  Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 

JAJI4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha   Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 

JAJI5

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju  wakiwa katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa, Majaji wa Mahakama kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 

JAJI6

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa na Majaji wa Mahakama  kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 

JAJI7

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na watendaji wa Mahakama baada ya  kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. PICHA NA IKULU

jaji juma

 

MAJALIWA ATATUA MGOGORO WA MPAKA WA KILINDI NA KITETO

Published in Jamii

LIW1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia  mkutanao wa hadhaa katika kijiji cha  Lembapuli kilichopo mpakani mwa wilaya za Kilindi na Kiteto alikokwenda kutatua mgogoro wa  mpaka  Januari 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

LIW5

LIW3

Waziri   Mkuu, Kassim Majaliwa  akielekea kwenye moja ya  jiwe la mpaka wa  wilaya ya Kilindi na Kiteto wakati alipokwenda  kwenye kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka wa Kiteto na Kilindi kutatua  mgogoro wa mpa Januari 18, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na kulia kwake ni  Mkuu wa wilaya na Tanga na Kaimu  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

LIW2

Baadhi ya wananchi wa  wilaya za Kilindi na Kiteto wakimshangilia  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji  cha  Lembapuli kilichopo  mpakani mwa wilaya za Kiteto na Kilindi alikokwenda kutatua mgogoro wa mpaka Januari 18, 2017. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

LIW6

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Kiteto na Kilindi  wakati  alipokwenda kwenye kijiji  cha Lembapuli  kilichopo kwenye mpaka wa wilaya hizo  kutatua mgogoro wa mpaka Januari  18, 2017.  Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na wapili kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

LIW8

Waziri Muu, Kassim Majaliwa  akizugumza na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi   (kushoto)  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel wakiwa katika kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka  wa wilaya ya Kiteto na Kilindi  Januari 18, 2017.  Mheshimiwa Majaliwa alikwenda Kiteto na Kilindi kutatua mgogoro wa mpaka unaovikabili vijiji vya  Mafisa na Kijungu. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Muu wa Wilaya ya Tanga mjini , Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

LIW9

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata  maelezo kuhusu ramani inayoonyesha mpaka  wa wilaya  ya Kilindi na Kiteto katika kijiji cha mpakani cha Lembapuli wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa mpaka kati ya wialya hizo Januari 18, 2017.  Mheshimiwa  Majaliwa apia alifuatana na Mawaziri , William Lukuvi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi na George Simbachawene  wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

LIW7

 

Waziri Muu, Kassim Majaliwa  akizugumza na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi   (kushoto)  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel wakiwa katika kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka  wa wilaya ya Kiteto na Kilindi  Januari 18, 2017.  Mheshimiwa Majaliwa alikwenda Kiteto na Kilindi kutatua mgogoro wa mpaka unaovikabili vijiji vya  Mafisa na Kijungu. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Muu wa Wilaya ya Tanga mjini , Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(P.T)

 

BEL1

Mwenyekiti wa  Kamati ya  Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)  Mhe. Albert Obama (Mb) akizungumza wakati Kamati yake ilipokwenda kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba katika eneo la Kawe na Morroco Jijini Dar es Salaam.

BEL2

Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya PIC kuhusu mradi wa ujenzi wa Nyumba katika eneo la Kawe.

BEL3

Mwenyekiti wa  Kamati ya  Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)  Mhe. Albert Obama (Mb) akielezea jambo wakati Kamati yake ikikagua ujenzi wa nyumba unaofaywa na NHC katika eneo la Kawe

BEL4

Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya PIC wakati wakikagua ujenzi wa Nyumba katika eneo hilo la Kawe.(Picha na Ofisi ya Bunge)(P.T)

MB1

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisindikizwa na kiongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe  baada ya kuwasili  jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MB2

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akisalimiana na viongozi wa Idara za wizara yake hiyo jijini Mbeya  baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe  kwa ziara ya kikazi.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MB3

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.Wengine ni viongozi wa idara za wizara yake  jijini hapo( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MB4

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akizungumza na aliyewahi kuwa kiongozi  katika Serikali zilizopita,Profesa David Mwakyusa (kushoto), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)(P.T)

Picha ya Fred Matuja

Kwa mara nyingine tena, Watanzania tunapitia katika hali ya sintofamu kati ya mgongano wa mawazo kuhusu uhakika wa chakula baada ya bei za baadhi ya vyakula hususani kupanda bei baadhi ya mikoa hapa nchini. Tamko la serikali kupitia kauli ya Mhe. Rais Magufuli iko wazi kuwa hakuna baa la njaa Tanzania. Kauli ya Rais Magufuli imefafanuliwa vyema na Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambae chini yake anasimamia idara inayohusika na usimamizi wa ghala la taifa la chakula.

Kwa upande mwingine, Waziri wa kilimo Mhe. Charles Tizeba nae ameonesha kwa kina kuhusu upungufu wa chakula kati ya sehemu moja na nyingine, hali kadhalika uhakika wa chakula katika mikoa mingine na mkakati wa kupeleka chakula kutoka ghala ya serikali kule kwenye upungufu.

Kwangu mimi naona kuna upungufu mkubwa wa moyo wa kizalendo kati ya waandishi wa habari Tanzania. Aidha wengi wao hawajui tafsiri rasmi ya baa la njaa au kuna watu wameweka maneno ya baa la njaa katika fahamu zao, nao kwa kujua au kutojua wanaingiza hofu katika akili za wasomaji wao.

Pamoja na changamoto za kutokuwa na uhakika wa mvua kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, bado kuna uwezekano wa kulima kwa mfumo wa kumwagilia na tukawa na uhakika wa kila aina ya chakula tunachokihitaji.

Ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi umezikumba nchi nyingi kusini mwa jangwa la Sahara ambazo ni Zambia, Malawi, Afrika Kusini na Zimbabwe.

Ni wakati muafaka kwetu Watanzania kuingia katika mfumo wa uzalishaji endelevu kwa kulimo cha umwagiliaji, kwani sote tunakumbuka kuwa ili mbegu iweze kuota inahitaji unyevunyevu, hali joto na hewa ya oxygen. Tukidadavua kisayansi, hali joto ipo, hewa ya oxygen ipo tunachokihitaji na uhakika wa unyevu unaotokana na maji.

Dk. A. R. Bernard katika mafunzo yake ya sanaa ya kutatua matatizo (art of problem solving) aliwahi kusema, “tatizo ni tofauti ya nini tunacho na nini tunahitaji” (Problem is a mis-match between what we have and what we want). Ili kupata tunachokitaka tunahitaji kujenga daraja la kututoa hapa tulipo kwenda pale tunapopataka. Mahali tulipo ni hali ya kutokuwa na uhakika wa mvua inayoleta unyevunyevu ili kuotesha mbegu na kuzikuza.

Tunachotaka ni uhakika wa maji ili tukilima tuweze kupata maji kama chanzo cha unyevunyevu muda wote mazao yakiwa shambani. Lengo likiwa ni kupate mazao ya chakula kama mahindi, mpunga, ndizi, maharage hali kadhalika mbogamboga na matunda.

Kwa upande mwingine, tunaweza kulima mazao ghafi kwa ajili ya viwanda. Mazao kama alizeti, karanga, pamba, ufuta na chochote kile kinachotakiwa kama mali-ghafi viwandani.

Kwa mfumo huu huu wa kumwagilia tunaweza kumwagilia nyasi kwa ajili ya chakula cha wanyama (kama vile ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda n.k) tunaofuga. Uhakika wa vyakula vya wanyama vitatupa uhakika wa nyama, maziwa na mazao mengine ya mifugo
Ushauri wangu kwa serikali na taasisi za kifedha kama vile mabenki ni kuja na mfumo mbadala wa kukopesha wakulima wenye akili za kulima kwa mfumo wa umwagiliaji ili kutengeneza mfumo endelevu wa uzalishaji wa mazao ya chakula na mazao mali ghafi za viwanda.

Watanzania hatutakiwi kulia kwa changamoto ya kukosa mvua katika maeneo ambapo hainyeshi vya kutosha, huu ni wakati sahihi zaidi kusimama kuikabili changamoto hii kwa akili mbadala. 
Nchi hii ina vyanzo vya maji ya uhakika kutoka katika maziwa, mito, maji yaliyo chini ya ardhi. Tukishirikiana na wataalamu wa mazingira, tunaweza kutumia vyanzo hivi vya maji ili kumwagilia mashamba yetu. Kwa upande mwingine, nyakati ambapo mvua huwa zinanyesha vya kutosha, kuna fursa ya kutengeneza mifumo ya kukinga na kuhifadhi maji ya mvua yanayotiririka (storm water) ili yatumike kumwagilia wakati mvua hazinyeshi.

Tukizalisha chakula kwa teknolojia ya kumwagilia, tutakuwa na uhakika kuzalisha mpaka ya mara 3 kwa mwaka kwa mazao ya muda mfupi kama mahindi, maharage na aina za mazao ya chini ya miezi mitatu.

Kwa adadi ya wingi wetu hapa Tanzania, tukitumia akili zetu vyema kwa kushirikiana na lengo kuja na mfumo wa uzalishaji endelevu kutoka shambani wakati huu wa mabadiliko ya tabia nchi.
Kilimo pasi kutegemea mvua kinawezekana. Tuamkeni, tujadiliane na wataalamu kwa ili tukuze uchumi wetu kwa mfumo wa kilimo cha umwagiliaji.

Tanzania ya viwanda itawezekana na inawezekana pia kwa kilimo endelevu cha mfumo wa umwagiliaji wa mazao yetu ya shambani. 
Nihitimishe kwa kumnukuu mfalme Suleiman kwa methali aliyoiacha kwa jamii ya wanadamu; … Pale pasipo na mashauriano, mipango hushindikana, ila kwa wingi wa mashauriano (yenye kusudi la kujenga) mipango hufanikiwa… (Where there is no counsel, plans fail; but in a multitude of counselors they are established.)

Kumbe sisi tunaojua kuandika, kuzungumza, tuna nafasi ya kushauri mipango yenye lengo la kuwa sehemu ya suluhisho juu ya changamoto zinazolipitia taifa hili. Tuna wajibu wa kufanya vyovyote vile kuijenga nchi hii isonge mbele ikiwemo mpango mkakati unaotekelezeka wa kuwa na kilimo endelevu chenye kutumia mfumo wa umwagilaji kwa ajili ya chakula na mazao ghafi kwa ajili ya viwanda.

Tanzania ikipiga hatua ya kimaendeleo, kila mmoja atafaidi. Kuna misingi ya usawa na utaifa ilijengwa na akina Mwalimu Nyerere, leo hii kila mmoja anafaidi. Huu ni wakati wetu wa kuweka jiwe, tofali, mbao, bati, dari na chochote kinachohitajika kuimarisha ujenzi wa nyumba yetu inayoitwa Tanzania.

Fredrick Mauja
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.(P.T)

Wananchi wa kijiji cha Madege kata ya Idete wakiwa katika mkutano wa uhamasishaji wa kilimo cha zao la Pareto 

Wananchi wa Madege wakisikiliza elimu ya kilimo cha zao la Pareto .

Wananchi wakitawanyika katika mkutano wa uhamasishaji wa kilimo cha pareto uliofanyika ofisi ya kijiji Madege Kilolo 

Vitalu vya miche ya Pareto kwa ajili ya kupewa bure wananchi 

mwakilishi wa kiwanda cha Pareto Mafinga Bw Godfrey Mbeyela akiwaeleza wananchi wa Bomalang'ombe Kilolo faida ya kilimo cha zao la Pareto 

Mwamasishaji wa zao la Pareto nchini Gerald Chuwa akiwapa maelezo wananchi wa Madege kata ya Idete juu ya faida ya kilimo cha Pareto 

Wananchi wa Bomalang'ombe wakimsikiliza diwani wa viti maalum

Na MatukiodaimaBlog 

WAKULIMA wa wilaya ya Kilolo na Mufindi mkoani Iringa kuanza kunufaika na kilimo cha zao la pareto baada ya kiwanda cha Pyrethrum company Tanzania Ltd (PCT) Mafinga kuanza kugawa bure ya zao la Pareto .
Akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji wa kilimo cha zao La Pareto mwakilishi wa kiwanda cha PCT Bw. Godfrey Mbeyela jana wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Bomalang'ombe na Idete , alisema kuwa kampuni hiyo imeamua kutoa miche bure ili kuwaondolea usumbufu wananchi wa kupata mbegu.

Alisema pamoja na kugawa bure kwa wananchi waliotayari kulima zao hilo la biashara pia kwa wale watakaojiunga vikundi watapewa ajira ya kuotesha miche ya Pareto na kuiuza kwa kampuni ili kuigawa bure kwa wakulima zoezi ambalo litakuwa kwa mwakani

"Kwa mwaka huu miche ipo ya kutosha ya kuwawezesha wananchi zaidi ya 40,000 kulima Pareto ila kwa kuwa idadi ya wakulima inaweza ongezeka zaidi mwakani vikundi vitapewa kazi ya kuotesha miche na kuuza kwa kampuni….. kampuni haitaki mkulima wa zao la Pareto kununua miche"

Juu ya soko la zao hilo ambalo miaka ya nyuma Wilaya ya Kilolo ilikuwa akiongoza kwa uzalishaji alisema kwa sasa soko ni uhakika kwani kampuni imekuja kwa kasi ya kuwakomboa wakulima na sasa fedha za mazao zitatolewa papo kwa papo shambani baada ya mavuno na hakuna mpango wa kumkopa mkulima .

Pia alisema bei ya zao hilo kwa kilo kwa wananchi wa Kilolo kwa ajili ya kuhamasisha kilo itanunuliwa kati ya Tsh 20000 hadi Tsh 30000.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wananchi kujiunga na kilimo hicho kwani ni moja kati ya mazao ambayo hayahitaji gharama kubwa ya kuhudumia zaidi ya palizi pekee.

Hivyo alishauri kila mwananchi kulima japo hekari moja ya Pareto japo mazao mengine waliyozoea yakiwemo mahindi kwa ajili ya Chakula kulima hekari nyingi zaidi. Mkuu huyo wa wilaya ya Kilolo alisema kilimo hicho cha Pareto ni fursa kubwa kwa wananchi ambao watachangamkia kuanza kilimo hicho.

Awali wananchi walisema kuwa waliacha kilimo hicho na mashamba ya Pareto kufyeka na kupanda viazi baada ya kuyumba kwa soko la Pareto ila kwa sasa kwa utaratibu huu mpya wapo tayari kuchangamkia kilimo hicho.(P.T)

Waziri Profesa Mbarwa (kushoto), akimweleza jambo Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi (katikati), wakati akitembelea Posta Kuu, maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ziara hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Dk. Harun Kondo (katikati), akimweleza jambo Waziri Profesa Mbarawa, akitembelea vitengo mbalimbali vya Ofisi za Posta Kuu jijijini katika ziara hiyo.

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza wakati Waziri Profesa Mbarawa alipokutana na wafanyakazi na kuzungumza nao Makao Makuu ya shirika hilo, wakati akimaliza ziara yake hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Dk. Harun Kondo (kulia), akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Profesa Mbarawa, kuzungumza na wafanyakazi, Makao Makuu ya shirika hilo, wakati wa kumaliza ziara yake hiyo.

Waziri Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta, Makao Makuu ya shirika hilo, wakati wa ziara yake hiyo.

Ofisa Mwandamizi wa Shirika la Posta, Makao Makuu, David Hango, akizungumza wakati akimweleza Waziri Profesa Mbarawa baadhi ya changamoto zinazolikabili na kukwamisha shirika hilo katika kupiga hatua za kimaendeleo.

Mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo kutoka Chama cha Wafanyakazi cha Tewuta, Ahmed Kaumo, akimweleza Waziri Profesa Mbarawa baadhi ya changamoto ambazo angependa kuwa na kikao cha pamoja cha Viongozi wa shirika hilo na wa chama hicho cha wafanyakazi katika kukabiliana nazo ili kulikwamua shirika hilo.

Mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo, upande wa Masoko, Joyce Kagose, akimweleza Waziri Profesa Mbarawa changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika hilo.

Mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa shirika hilo, akimweleza kwa uchungu Waziri Profesa Mbarawa jinsi changamoto wanazozipata kutoka kwa baadhi ya watendaji wa shirika hilo, ambao hujifanya wasomi na kuwazarau wale wa zamani kutokana na elimu zao.

Waziri Profesa Makame Mbarawa (katikati), akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na wafanyakazi hao.

Waziri Profesa Makame Mbarawa, akijibu baadhi ya hoja na ushauri wa wafanyakazi wa shirika hilo, wakati wa ziara yake hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akiwasili Ofisi za Posta Kuu ya Shirika la Posta maeneo ya Posta Mpya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Dar es Salaam leo. Kulia ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi (katikati), wakati alipofika katika ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Shirika la Posta, Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo kuangalia shughili mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo.

Mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (kushoto), akimpatia maelezo Waziri Profesa Mbarwa kuhusu mambo ya usalama kwenye mtandao wa shirika hilo. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Posta, shughuli za biashara, Janeth Msofe.

Waziri Profesa Mbarwa, akimsikiliza mteja wa shirika hilo, Mhandisi Nungu Allanus kutoka DIT, kuhusu ubora wa utoaji huduma wa shirika.  

Waziri Profesa Mbarwa (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Msaidizi Meneja wa Fedha na Huduma wa shirika hilo, wakati alipotembelea kitengo kipya cha kutolea huduma mbambali za kifedha cha Jamii Centre. Katika Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Dk. Harun Kondo. (P.T)

Oh! Oh! Mwenyekiti Leo Amekumbuka Marimba Ya Bukoba..!

Published in Jamii

Ndugu zangu,

Mwaka 2012 nilikuwa Bukoba. Nilipata bahati ya kutembezwa sehemu tofauti. Pichani ni mojawapo ambapo nilikuta wana marimba pia!
Maggid(P.T).

WVU

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na  baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya IPP Media yenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WVU 1

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass(kushoto) akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa IPP Media upande wa Televisheni wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  alipotembelea Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WVU 7

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza mara baada ya kuwasili katika kampuni ya IPP media kwa ajili ziara yake ya kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya Kampuni hiyo jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WVU 10

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipata maelekezo kutoka kwa mmoja ya wafanyakazi wa Ipp Media kuhusuana na ufanyaji kazi wa vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WVU 3

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia studio ya kutangazia habari katika kituo cha Televisheni cha ITV alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya IPP Media jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WVU 6

Mkuu wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam kujionea utendaji wake wa kazi jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WVU 11

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Sahara Media alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa vituo chini ya kampuni hiyo jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WVU 12

Mkurugenzi wa Masuala ya Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)  Frederick Ntobi akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa Sahara Media wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  alipowatembelea jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WVU 13

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na uongozi na wafanyakazi wa Sahara Media kwa tawi la Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake kwa vituo vilivyo chini ya kampuni hiyo jana January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.

Na Raymond Mushumbusi WHUSM

Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari nchini katika kutoa habari kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo Serikali katika kutekeleza majukumu yake.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv pamoja na Sahara Media kwa tawi la Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye amehaidi kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali na vyombo vya habari katika utoaji wa habari ambazo ni muhimu kwa wananchi kujua zikiwemo hatua ambalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kutekeleza majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Niseme kwa kipindi cha nyuma kumekuwa na urasimu wa utoaji wa taarifa muhimu kutoka kwetu kuja kwenu vyombo vya habari lakini niwahakikishe kuwa sasa Serikali imefungua milango kwenu na tuendelee kushirikiana katika kuhabarisha umma wa watanzania” Alisistizia Mhe. Nnauye.

Kawa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass amevihakikishia vyombo vya habari nchini ushirikiano mzuri katika kupata habari za Serikali kutoka katika vitengo vyote vya Mawasiliano Serikalini.

Dkt Abass ameeleza kuwa kwa sasa wako katika mpango wa kuboresha vitengo vya Mawasiliano serikali ili kuboresha upatikanaji wa habari zinazohusu Serikali.

“Niwahakikishieni ndugu zangu wanahabari kuwa suala la upatikanaji wa habari kutoka Serikali litakuwa si la kusumbuana tena na tunatengeneza mfumo katika vitengo vyote vya Mawasilaino Serikalini ili iwe rahisi kupata taarifa kutoka kwetu” alisisitiza Dkt Abass.

Aidha Mkurugenzi wa ITV/Radio One Bibi. Joyce Mhavile ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari vya binafsi nchini katika kutoa taarifa kwa umma ambazo zimesaidia kuelimisha, kuburudisha na kutengenza mazingira ya watu kuamini yale yanayotolewa na vyombo vyao.

Naye Mkuu wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari nchini  na kuahidi kuongeza ushirikiano baina yao na Serikali katika upashanaji habari.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye yupo katika ziara ya siku sita kutembelea vituo vya Televisheni kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo ikiwa pamoja na changamoto zilizopo ili kupata namna bora ya kuiendeleza sekta ya habari kwa manufaa ya taifa.(P.T)

MAJALIWA CU ELIMU MTWARA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi Wazara wa Elimu Sayansi na Telnolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda mkoani Mtwara kufanya uchunguzi ili kubaini sababu zilizosababisha shule tisa za mwisho katika matokeo ya kidato cha pili kutoka mkoani humo.

Pia ameziagiza halmashauri nchini kushirikiana na Idara ya Ukaguzi ili kuhakikisha wanawasimamia vizuri walimu jambo litakalowezesha kuboresha ufundishaji na hatimaye kupata matokeo mazuri.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Januari 17, 2017) wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo ya Mpanda kwa ajili ya kufungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.

Kwa mujibu wa matokeo hayo kati ya shule 10 za sekondari zilizofanya vibaya kwenye mtihani huo, tisa zinatoka katika Mkoa wa Mtwara na moja Tanga. Shule za Mtwara zilizofanya vibaya ni Chingungwe, Malocho, Naputa, Chanikanguo, Mtiniko, Michiga, Msimbati, Salama na Lukodoka huku ya Tanga ikiwa ni Nywelo.

“Viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) waende Mtwara wakafuatilie kwa kina wajue kuna nini hadi shule tisa kati ya 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke huko,” amesisitiza.

Mbali na kuuagiza huongozi wa wizara hizo kwenda mkoani Mtwara pia Waziri Mkuu amewataka wasimamie vizuri mikoa ambayo awali ilikuwa na matokeo mabaya na sasa inafanya vizuri na wahakikishe shule za mikoa hiyo hazishuki na badala yake ziendelee kupata matokeo mazuri zaidi.

Awali, akisoma taarifa ya mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga alisema katika matokeo ya mtihani kidato cha pili ya mwaka jana mkoa wake ulishika nafasi ya pili kitaifa ukiongozwa na mkoa wa Geita.

Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha katika mitihani ya mwaka huu wanashika nafasi ya kwanza kitaifa, hivyo alitoa wito kwa watendaji wa Idara ya Elimu, wakuu wa shule, wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMANNE, JANUARI 17, 2017.(P.T)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School kushoto ni Meneja Mradi Dkt Charles Sokile.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania uliomtembelea ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.                              

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameuhimiza uongozi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania kuharakisha mchakato wa kuanzisha Chuo cha Joseph Business School hapa nchini chuo ambacho kitatoa mafunzo mbalimbali ya biashara, maadili ya uongozi na ugunduzi wa mawazo ya biashara ili kusaidia mamia ya Watanzania kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

Makamu wa Rais ametoa kauli ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa  Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania ambao walimtembelea Makamu wa Rais kumweleza hatua ambazo wamefikia katika uanzishaji wa Chuo hicho.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema wazo la uanzishaji wa Chuo hicho ulitolewa na Dkt Bill Winston ambaye ni Mwanzilishi wa Winston Ministries mwaka jana katika Maombezi ya Taifa ambaye yeye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo, anasema aliupokea kwa furaha mpango huo kwa sababu chuo hicho kitasaidia watanzania wengi kupata elimu na ujuzi wa kuimarisha biashara zao wakati taifa likielekea kwenye uchumi wa Viwanda.

Amesema hatua za uanzishwaji wa Chuo hicho hapa nchini ni fursa pekee na nzuri kwa Watanzania kujifunza ubunifu na ugunduzi katika biashara, maadili ya uongozi katika biashara ili kuongeza ufanisi katika biashara zao kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla hasa katika ulipaji wa kodi.

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma na Meneja Mradi Dkt Charles Sokile wamemhakikishia Makamu wa Rais kuwa hatua ambazo wamefikia kwa sasa katika uanzishaji wa Chuo hicho ni nzuri ambapo mpaka sasa wamepata majengo kwa ajili ya ofisi na maeneo ya kufundishia na hatua za usajili wa chuo hicho zipo katika hatua za mwisho.

Wamesisitiza kuwa wanataka kushirikiana ipasavyo na Serikali katika uanzishaji wa chuo hicho ambacho kitatoa elimu ya biashara hasa ugunduzi wa mawazo ya biashara nchini kama hatua ya kutekeleza kwa vitendo dhana ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda nchini.(P.T)

KATAEE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la Dawa la Bohari ya Dawa (MSD), Mpanda mkoani Katavi. Kutoka shoto mwenye shati la kijani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa  Katavi, Peter Mselemu, Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kanali mstaafu Raphael Muhuga. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

Jiwe la Msingi.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu wakifurahi wakiwa ndani ya duka hilo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi wa duka hilo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa MSD.

Mwonekano wa duka hilo la MSD, mkoani Katavi.

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema utaratibu wa MSD wa kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji litaboresha upatikanaji wa dawa na kupunguza gharama za kununua dawa kutoka nje ya nchi.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa duka la dawa la MSD,  Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi, ambalo linaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka 7 ya dawa nchini.

Waziri Mkuu pia amesema kwa mwaka huu wa fedha shilingi Bilioni 251 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba ili kupunguza changamoto za uhaba wa dawa na kueleza kuwa shabaha ya serikali ni kufikia asilimia 95-100 ya upatikanaji wa dawa hadi itakapofika mwezi Juni, 2017.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa duka hilo wataliendesha kwa mwaka mmoja tu,na kisha kulikabidhi kwa Halmashauri ili iliendeshe na kuongeza mapatao yao.

Kwa upande wa upatikanaji wa dawa, Bwanakunu amesema kuwa kwa sasa fedha sio tatizo,na dawa zinaendelea kuagizwa kulingana na mahitaji. 

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)(P.T)

Shujaa Alphonce Simbu atua nchini

Published in Jamii

asimbu1

Wawakilishi wa Tanzania katika mbio za 14 za Standard Chartered Mumbai Marathon Alphonce Simbu na mwanadada Magdalena Krispin, wakiwasili nchini kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere  ambapo alichukua nafasi ya kwanza akimtimulia vumbi mpinzani wake wa karibu Mkenya Joshua Kipkorir katika kundi la wakimbiaji wa nje wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Multchoice Tanzania Johnson Mshana na kushoto ni Kocha wa Alphonce Simbu Bw.Francis

asimbu2

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Multchoice Bw. Johnson Mshana akizungumza na waandishi wa habari wakati Wawakilishi wa Tanzania katika mbio za 14 za Standard Chartered Mumbai Marathon Alphonce Simbu kulia alipowasili usiku wa kuamkia leo.

asimbu3

Wawakilishi wa Tanzania katika mbio za 14 za Standard Chartered Mumbai Marathon Alphonce Simbu na mwanadada Magdalena Krispin wakishuka kwenye ndege wa Shirika la Ndee la Precission Air mara baada ya kuwasili nchini wakitokea Mumbai nchini India.

 

  • Asema kazi ndio imeanza.
  • Atoboa siri ya ushindi wake…. Wingi wa wenzetu unawabeba!

Wawakilishi wa Tanzania katika mbio za 14 za Standard Chartered Mumbai Marathon Alphonce Simbu na mwanadada Magdalena Krispin, wamewasili nchini huku mshindi wa mbio hizo Alphonce Simbu  akitoboa siri nzito kuhusu ushindi wake ambapo alichukua nafasi ya kwanza akimtimulia vumbi mpinzani wake wa karibu Mkenya Joshua Kipkorir katika kundi la wakimbiaji wa nje. Mtanzania huyo aliongoza huku akifuatiwa na Wakenya 7 and Waethiopia 2 katika 10 bora.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, Simbu alilakiwa na kocha wake Francis John na Afisa muandamizi kutoka Multichoice Tanzania Johnson Mshana, muwakilishi wa Chama cha Riadha Tanzania Tulo Chambo. Pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kuwasili, Simbu alianza kwa kutoa shukrani kubwa kwa Watanzania wote ambao wamekuwa wakimuombea na kumtakia kila la heri. Aliipongeza kipekee kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kukubali kumdhamini kwa muda wa mwaka mzima kitendo ambacho kimempa muda mrefu wa kufanya mazoezi na hivyo kuweza kushinda mbio hizo.

“Kwa kweli nimefurahi sana kwa ushindi huu na siri kubwa ya ushindi wangu ni kujituma, mafunzo na mazoezi” alisema Simbu na kuongeza “Baada ya kupata udhamini kutoka Multichoice Tanzania, niliweza kutulia kwani sasa kazi yangu ilibaki moja tu, mazoezi, na kwakweli mwalimu wangu amefanya kazi ya ziada ya kunifundisha na kuniongoza pamoja na kusimamia kila kitu ikiwemo kufanya mawasiliano na waandaaji wa mashindani niliyoshiriki”

Mkuu wa mawasiliano wa Multichoice Tanznaia Johnson Mshana ambaye alikuwepo uwanjani hapo kumpokea Simbu, amesema Multichoice Tanzania imejizatiti kuinua na kuimarisha sekta ya michezo na burudani hapa nchini ikiwemo kuongeza chanel nyingi zenye maudhui ya kitanzania katika sanaa, burudani na michezo na pia katika kushiriki moja kwa moja kama ilivyofanya kumdhamini Simbu.

“Bila kuvipalilia vipaji tulivyonavyo, itakuwa vigumu sana kufikia malengo, ndiyo sababu sisi Multichoice Tanzania tumeamua kutia nguvu katika kukuza vipaji vya watanzani” alisema Mshana na kuahidi kuwa wataendelea kumuunga mkono simbu ili wafanikiwe katika lengo la kushinda katika michuano ijayo ya kimataifa.

Mwalimu wa mafunzo wa Mkimbiaji huyo Francis Alimtaja Simbu kuwa ni mwanariadha mwenye kipaji kikubwa na nidhamu ya hali ya juu, mbali na jitihada kubwa anazofanya kila siku kuhakikisha kuwa anatimiza ndoto zake. “Alphonse ni kijana mwenye bidii, juhudi na maarifa, na zaid ya yote ni kipaji chake na nidhamu yake ya hali ya juu” alisema Francis na kuongeza kuwa  sisi multichoice tumeTulichukua jukumu la kumdhamini simbu katika mazoezi na maandalizi yake kwa kipindi cha mwaka mzima, kwani tunafahamu fika kuwa mazoezi na maandalizi ndiyo siri kubwa ya mafanikio katika mchezo wowote. Alisema Mshana na kuongeza “dhamira yetu kubwa ni kuinua vipaji na kulirejesha taifa letu kwenye ramani ya dunia katika ulingo wa michezo na burudani”

Katika mbio hizo, aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa 2:09:28 muda ambao ni mzuri sana kwa mbio za aina hiyo. Mwezi April mwaka huu, Alphonce anatarajiwa kushiriki mashindano mengine makubwa Ulimwenguni ya London Marathon.(P.T)

pol1

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari leo, Januari 17, 2017, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Picha na Bashir Nkoromo)

pol2

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari leo, Januari 17, 2017, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Picha na Bashir Nkoromo)

*AWASIHI WANASIASA KUJIKITA KATIKA SIASA SAFI NA UONGOZI BORA

Na Bashir Nkoromo

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewasihi viongozi wa vyama vya wapinzani kujikita katika siasa safi na uongozi bora, kwa kuachana na matamko ya uongo yanayosababisha taharuki katika nchi na kuchonganisha wananchi na serikali yao, kwa kuwa vitendo hivyo havina manufaa kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Huphrey Polepole, wakati akizungumza na waandishi wa habari, leo Januari 17, 2017, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Kichama.

Polepole amsema, wapinzania wamekuwa wakitumia matatizo ya wananchi na kutoa matamko ya uongo ili kutia nchi katika taharuki kwa lengo la kujitafufia umaarufu wa siasa vitendo ambavyo alisema, havisaidii wananchi wala wanasiasa  wa vyama hivyo katika kuleta maendeleo ya nchi.

Alisema, mbali na matamko ya viongozi wa vyama hivyo kutosaidia, katika ujenzi wa maendeleo yamaendeleo ya nchijambo ambalo alisema za kueneza maneno ya yasiyofanyiwa utafiti kwa lengo la kusababisha taharuki kwa wananchi, jambo ambalo alisema, si miongoni mwa siasa safi wala uongozi bora.

Polepole alisema, wapinzani wamekuwa wakifanya siasa za aina hiyo wakiwa wanajua ubaya wake, kwa kuwa wao lengo lao ni kujaribu kuchonganisha wananchi na serikali hata pale ambapo serikali inaonyesha juhudi za dhali za kuijenga Nchi yenye uchumi imara wa viwanda.

“Nawaonba Watanzania tuwapuuze wanasiasa wa vyama hivi,  tuendelee kuiunga mkono serikali, ili itimize mipango na malengo iliyoweka, ikiwemo kuhakikisha Tanzania inakuwa kiuchumi kwa kuwa nchi ya viwanda, hali ambayo itasaidia sana kutukwamua Watanzania kutoka katika umasikini”, alisema Polepole.

Polepole alitaja kuwa miongozi mwa mambo ambayo katika kipindi hiki wanayatumia kupotosha ili kujaribu kuletea taharuki wananchi ni pamoja na kueneza propaganda kuwa Tanzania imekumbwa na baa la njaa na pia kutumia matatizo waliyopata wananchi wakati wa janga la tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera kama mtaji wao kisiasa.

“Kwanza mjue, kutungaza taarifa ambazo zitaleta taharuki katika jamii ni kosa la jinai, lakini pia inajulikana na wenyewe wanajua, kwamba Duniani kote zipo taratibu ya utangazaji wa majanga katika nchi yoyote. Baa la njaa ni janga kubwa linapofikia kiwango kibaya, mwenye mamlaka ya kutangaza ni Mkuu wa nchi”, alisema Polepole na kuongeza;

Alisema, Tanzania haijawahi kupata  njaa yenye kiwango cha kuitwa baa la njaa, katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, hivyo wanaojaribu kutangaza kuwa Nchi ipo katika baa la njaa ni kushindwa kufanya siasa safi na kukosa uongozi bora kama ilivyo CCM ambayo mambo hayo inayo.

“Ingawa tumekuwa na tatizo la njaa katika sehemu chache za na kuwepo upungufu wa mvua katika maeneo kadhaa ya nchi hali ambayo inaweza kusababisha upungufu wa chakula katika maeneo husika, bado hili siyo baa la njaa. Na kwa kuwa hili serikali inalijua inaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuweza kupelekwa vyakula maeneo yote kuondoa uhaba, na kipindi hiki hatujafikia huko”, alisema Polepole.

“Baada ya kuona hali ipo hivi nilitarajia viongozi wote bila kujali vyama , tuhimize wananchi kutumia chakula vizuri wasikitumie katika mambo ya anasa au kukiuza hovyo, lakini wao wanakimbilia kutangaza baa la njaa wakati njaa yenyewe haijatokea, hawa watu wa ajabu sana’, alisema Polepole.

Alisema, kila kiongozi anayeongozwa na misingi ya uongozi bora na mzalendo kwa nchi yake, analo jukumu la kuwahamasisha wananchi kutunza vyakula walivyonavyo.

Kuhusu tetemeko lilitokea Bukoba  na kusababisha uharibifu na vyumba za watu na miundombinu mbalimbali alisema kama ilivyo ulimwenguni kote, inapotokea mambo haya ya majanga serikali hujenga uwezo wake kwanza ili kusaidia wananchi wake.

“Baada ya tetemeko lile, Serikali ilichofanya ni kujengea uwezo wa wananchi wasiwe mbali na huduma  ndiyo maana ikaimarisha miundombinu ya elimu, afya na barabara, kwa sababu watu waendelee kupata huduma”. alimalizia Polepole.(P.T)

POLISI YANG’OA TAA 665 ZA MAGARI ZISIZO SAHIHI

Published in Jamii

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Jeshi la Polisi Tanzania limeondoa taa za ziada (spot light) 665 zilizokuwa zimewekwa kwenye baadhi ya magari bila kupata kibali na utaratibu wa mtengenezaji wa chombo husika.

Hatua hiyo inalenga kupunguza ajali za barabarani zinazosababishwa na matumizi ya taa hizo zisizo sahihi.

Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matumizi ya taa za gari.

DCP Mpinga alisema kuwa marekebisho yoyote katika gari yanahitaji kibali cha mtengenezaji , kinyume cha hapo ni uvunjaji wa sheria.

Aliongeza kuwa taa hizo hutumika vibaya hasa nyakati za usiku na kuwa chanzo cha ajali kwa sababu zinapotumika hupoteza uwezo wa mtumiaji kuzitawala kwa maana ya kubadilisha uwakaji wake.

Kamanda Mpinga aliwashukuru baadhi ya watumiaji wa barabara kwa kuunga mkono usimamizi wa sheria kwa kuziondoa taa hizo kwa hiari na kuwasisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo waendelee kuzitoa taa hizo wenyewe.

Aidha, Kamanda huyo alitaja ajali za barabarani zilizotokana na matumizi mabaya ya taa kwa mwaka 2015 zilikuwa 104 na mwaka 2016 zilikuwa 123.(P.T)

Mkuu wa Zana za Kidijitali wa Kampuni ya Simu ya Tigo,  Tawonga Mpore (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuzindua Twende APP kwa ajili ya kusaidia huduma ya usafiri wa teksi nchini. Kulia ni Mkuu wa Utawala na Fedha wa DTBi ambao ni wawezeshaji wa mradi huo, Mramba Makange na Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu wa Costech,  Dk.Digushilu Mafunda.

Ofisa Mtendaji na Muasisi wa Twende App, Justin Kashaigili, akielezea jinsi ya kutumia mfumo huo kupitia simu ya mkononi.

 Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu wa Costech,  Dk.Digushilu Mafunda (katikati), akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Hassan Mshinda.

 Wadau mbalimbali na waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Wapiga picha wakichukua tukio hilo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI inayoongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imezindua huduma mpya ya kidijitali inayoitwa Twende App ambayo ni suluhisho la kuita teksi na hivyo kuwapatia wateja wake huduma sahihi na  wanayoimudu ya usafiri wa teksi nchini Tanzania.

Kwa kuunganishwa moja kwa moja na madereva wa teksi, huduma hiyo inawawezesha watumiaji kufurahia kiwango cha chini kuliko ambavyo wangetumia njia nyingine mbadala za mitaani. Twende App itakuwa na mawasiliano ya madereva teksi, bajaj na boda boda ambao wamehalalishwa na vyama husika vya madereva.

Akitangaza huduma hiyo mpya katika mkutano wa wanahabari jijini Dar es Salaam leo asubuhi , Mkuu wa Zana za Kidijitali wa Tigo Tawonga Mpore  alisema, “Huduma hii ni kielelezo cha Tigo kujikita katika mageuzi ya mtindo wa maisha ya kidijitali kwa kutoa suluhisho kwa changamoto zinazowakabili wateja wake. Tunaamini kwamba Twende App itatoa huduma nzuri kwa abiria kwa kuwaunganisha na madereva ambapo watapata huduma bora zilizo na gharama nafuu na zenye ufanisi wa hali ya juu.”

Mpore aliongeza: “Tunaamini kwa kutoa njia mbadala kwa usafiri uliopo wa teksi,  tunaweza kusaidia kuboresha  usafiri kwa ujumla nchini Tanzania. Tunafahamu msongamano wa vyombo vya usafiri  uliopo jijini kwa sasa; hivyo tunalenga kuwa sehemu ya suluhisho katika kutatua adha hiyo. 

Kimsingi tunaamini  kupunguza usumbufu  katika barabara za jijini  na kupunguza athari za kimazingira zinazotokana na  msongamano wa magari  ikiwa ni sehemu ya kukua kwa uchumi.”

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),  Dk. Hassan Mshinda ambaye alisema: “Napenda kumshukuru mbia wetu Tigo ambaye kila mara  amekuwa mstari wa mbele  katika kuhakikisha wajasiriamali  wetu vijana katika teknolojia ya kisasa wanapata msaada muhimu katika kufikia malengo yao na kwa huduma  hii naamini itawapatia fursa mpya zenye manufaa  kwa madereva kote jijini.”

Akizungumza  wakati wa uzinduzi, Ofisa Mtendaji na muasisi wa Twende App, Justin Kashaigili alisema: “Nimesukumwa na kasi ya maendeleo ya miundo mbinu  na nguvu ya ujasiriamali hapa nchini. Ninategemea kuwapatia wakaazi wa jiji la Dar es Salaam chaguo wanalolimudu, rahisi na linalofaa kwa ajili ya  usafiri  salama.”

Akielezea jinsi ya kujiunga na huduma hiyo, Kashaigili alisema, “abiria analotakiwa kufanya ni kupakua Twende App katika simu yake  ambayo itamuunganisha na dereva moja kwa moja  badala ya kuhangaika kwenda mwenyewe kufuata  sehemu ilipo teksi. Huduma hii pia inatumia muda sahihi wa taarifa za dereva, mfumo hai wa satelaiti unaowezesha ramani  ya kufahamu sehemu alipo abiria  na kumuunganisha abiria mwenyewe na dereva aliyepo karibu na wakati huo huo kumwezesha dereva kutoa majibu.”

Twende App  hivi sasa  inatoa mbadala sahihi wa malipo  kupitia Tigo Pesa kwa namba binafsi za Tigo Pesa kwa madereva na inapatikana  katika mfumo wa Android na hivi karibuni itapatikana kwa watumiaji wa simu zilizo na mfumo wa iOs.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)(P.T)

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA