Abdallah Mtolea, aliyepitishwa na CCM kuwania Ubunge wa Temeke, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 amepita bila kupingwa baada ya wagombea waliokuwa wamechukua fomu kuwania nafasi hiyo kukosa sifa.
Mtolea aliyekuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF hadi Novemba 2018 alipojiunga na CCM na kupitishwa kuwania ubunge, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Lusubilo Mwakabibi kuwa mshindi.



