habari

Abdel Fattah al Sisi Aibuka Mshindi Kwa 97%.

on

Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo baada ya kushinda uchaguzi wa rais kwa asilimia 97 ya kura, idadi sawa ya kura aliyopata katika uchaguzi uliopita miaka minne iliyopita. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa mwezi Machi hata hivyo yanaonesha kuwa idadi ya wapiga kura waliojitokeza kushiriki ilikuwa asilimia 41 licha ya juhudi za kuwashawishi Wamisri wengi kujitokeza.

Ushindi huo wa Al Sisi unaompa muhula wa pili madarakani, ulitarajiwa kwani hakuwa na ushindani wa maana.Mgombea pekee aliyeruhusiwa kuwania dhidi yake ni Moussa Mostafa Moussa, mwanasiasa asiyekuwa na ushawishi anayeonekana kutumika kuhalalisha ushindi wa Al Sisi. Upinzani ulisusia uchaguzi huo ulioutaja kuwa ni kichekesho. Tume ya uchaguzi imesema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *