habari

Agnes Gelard (Masogange) Aachiliwa Baada Ya Kulipa Faini.

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachilia huru Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye ni ‘video queen’ baada ya kulipa faini ya shilingi milioni 1.5.
Awali mahakama hiyo ilikuwa imemhukumu Masogange kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitatu au kulipa faini ya Shilingi Milioni 1.5, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, ambapo Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko alisema kuwa watalipa faini.
Hukumu hiyo ilikuwa imetolewa na Hakimu Wilbard Mashauri ambaye alisema kuwa ameridhishwa pasi na kuacha shaka juu ya ushahidi wa upande wa mashtaka hasa kwa uthibitisho uliotolewa na Mkemia Mkuu wa serikali kwamba mkojo wa mshtakiwa ulikutwa na chembe chembe za dawa za kulevya.
Baada ya Masogange kutoa utetezi wake, Hakimu Mashauri alisema kuwa ameusikia utetezi wa mshtakiwa kwamba apewe adhabu ndogo, huku upande wa mashtaka ukitaka apewe adhabu kali.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *