habari

Ajali Mbeya, Watu 8 Wafariki Papo hapo.

on

Watu wanane wamefariki dunia papo hapo baada ya gari dogo aina ya Noah yenye namba za usajili T 649 DEA kugongana uso kwa uso na basi la Igembesabo katika Barabara ya Chunya Mbeya huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa hakijulikani.

Taarifa zinasema kuwa waliofariki ni ndugu wa familia moja waliokuwa wakisafiri kwenye gari hiyo aina ya Noah kutoka Chunya kwenda Jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mussa Tahib, ajali hiyo imetokea saa 5:00 asubuhi nakusema na kwamba wanafamilia hao waliofariki walikuwa wanawahi mazishi ya ndugu yao jijini Mbeya.

Amesema wanafamilia hao walikuwa tisa na kwamba ni mmoja pekee ambaye alisalimika japo alijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya kwaajili ya matibabu na hakuna majeruhi wala kifo chochote kwenye basi.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Aprili 9, 2018 mchana ikihusisha Noah yenye namba za usajili T 649 DEA na basi la Igembesabo katika Barabara ya Chunya Mbeya huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa hakijulikani.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *