habari

Ajali Ya Basi Ujerumani: Wanne Wapoteza Maisha, 20 Wajeruhiwa.

on

Takribani Watu wanne wameuawa baada ya basi dogo kuligonga kundi la watu waliokuwa wakitembea kwa miguu katika mji wa Muenster, Ujerumani Jumamosi mchana ambapo watu wengine 20 walijerihiwa.

Aidha imeelezwa kuwa kati ya watu waliokufa katika tukio hilo ni dereva mshukiwa, aliyejipiga risasi akiwa ndani ya gari hilo kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la polisi. Gazeti la Sueddeutsche Zeitung limesema maafisa wanaamini hapakuwa na lengo la ugaidi katika tukio hilo.

Gazeti la Sueddeutsche pia limeripoti nyumba ya mshukiwa ilikuwa ikakaguliwa kutafuta uwezekano wa kuwepo na vilipuzi, ingawa maafisa wa serikali ya Ujerumani walikuwa bado hawajasema ni nini wanadhani lilikuwa lengo la tukio hilo.

Msemaji wa Polisi Andreas Bode amesema mashuhuda walioshuhudia tukio hilo wamesema watu wengine waliondoka kwenye gari baada ya kugonga.

Shirika la habari la Ujeurmani DPA, liliripoti kwamba mashuhuda walizungumzia juu ya watu wawili waliokuwemo ndani ya basi hilo mbali na dereva na kwamba uchunguzi bado unaendelea.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *