habari

Ajali Ya Ndege Algeria, Abiria 247 Na Wafanyakazi 10 Wapoteza Maisha.

on

Mara tu baada ya kuondoka kutoka uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufarik, Ndege ya kijeshi ya usafiri ya Algeria imeanguka  kilomita 30 kusini mwa Algiers. Kwa mujibu wa ripoti rasmi ya kwanza  iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi, Katika ajali hiyo, jumla ya watu 257 wamepoteza maisha, ambao ni Abiria 247 na wafanyakazi wote kumi wa ndege hiyo.

Ndege hii aina ya Iliouchine IL-76 imeanguka katika shamba moja karibu na uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufarik, ambapo miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni askari na familia zao.

Ndege hiyo ilikua ikielekea uwanja wa ndege wa kijeshi wa Tindouf, kwenye mpaka na Sahara Magharibi. Vyanzo vya Usalama, vilivyonukuliwa na gazeti la kila siku la Ennahar, vinabaini kwamba wajumbe 26 wa Polisario walikuwa katika ndege hiyo.

Mamlaka inajaribu kutafuta mabaki ya waliouawa. Picha kutoka eneo hilo zinaonyesha moshi ukifuka kutoka kwa vifusi vya mabaki ya ndege hiyo.

 Naibu waziri wa Ulinzi, pia Mkuu wa majeshi ya Algeria, Jenerali Ahmed Gaid Salaha amezuru eneo la ajali, na pia tume ya uchunguzi imeundwa ili kujua sababu ya ajali hiyo.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *