habari

Askofu Kakobe Afika Idara Ya Uhamiaji.

on

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amewasili leo Aprili 9, 2018 katika idara ya uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya mahojiano.
Hata hivyo, Kiongozi huyo wa kiroho hakuweza kuzungumza lolote mbele ya waandishi wa habari waliokuwapo eneo hilo.
Awali, ofisa uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Crispin Ngonyani alisema, “Tumemuita (Kakobe) kwa mahojiano; yanahusu nini hilo kama litahitajika tutawaeleza lakini kwa sasa tusubiri kwani hata kufika hajafika.”
Amesema kwa mujibu wa sheria uhamiaji inaweza kumwita mtu yeyote.
“Hakuna tatizo, kwa hiyo wananchi wasiwe na hofu sisi tunatekeleza wajibu wetu,” amesema.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *