michezo

AWESO CUP 2018 Yazinduliwa Kwa Kishindo, Simba Wailaza Yanga Pangani.

on

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akizindua mashindano ya Kombe la Aweso (AWESO CUP 2018) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iyopita mjini Pangani, Tanga. Pembeni ni Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (mwenye kofia nyeusi) ambaye ndiye mwaandaaji wa kombe hilo, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja (mwenye traki suti bluu), Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza na msemaji wa Simba, Haji Manara na Jerry Muro.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amefungua mashindano ya kombe la Aweso katika uwanja Kumba wilaya Pangani na kuwataka viongozi wa halmashauri ya Pangani kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vya kuchezea.
Katika kufanikisha ufunguzi wa kombe la Aweso wasanii wa filamu wanaunda kundi la Uzalendo Kwanza walishiriki ili kuhamasisha vijana kupenda michezo na sanaa.
Akifungua mashindano hayo Naibu Waziri Juliana Shonza akatoa agizo kwa viongozi wa halmashauri kukarabati viwanja huku mkuu wa wilaya wa Pangani, Zainab Abdallah Issa amesema kuanzisha kwa kombe la Aweso kuanarudisha ari ya michezo wilayani humo.
Kwa upande wake Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ambaye ndiye mwaandaaji wa kombe hilo amesema katika mashindano hayo watapatikana vijana wenye vipaji.
Nae mwenyekiti wa uzalendo kwanza Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ amesema ushiriki wao unasaidia vijana kupenda michezo na sanaa.
“Tumekuja kuwaamsha vijana wenzetu ili watambue umuhimu wa kuwa Wazalendo na kujikwamua na watambue vipaji vyao, maana vijana wengi wamepoteza matumaini ya kuishi kutokana na kujiona wametengwa na jamii” amesema.
Jumla ya timu 20 zinashiriki michuano ya kombe la uweso ambapo timu shiriki zikabidhiwa vifaa vya michezo na naibu waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo.
Katika ufunguzi wa kombe hilo uchezwa mchezo wa mashabiki Simba na Yanga ambapo timu ya Simba ikiongozwa na Msemaji Haji Manara waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Yanga na wakapata maziwa ya Asas na fedha laki tano huku Yanga wakipata laki tatu na maziwa ya Asas. Huku zikishuhudiwa na Naibu Waziri wa Habari Michezo, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mkuu wa wilaya Pangani, Zainabu Issa, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja.

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *