habari

Baada Ya Kashfa, Facebook Yadaiwa Kushuka Thamani.

on

Mtandao huo wa kijamii wa Facebook ambao hivi karibuni ulikabiliwa na hisia kali kutoka kwa wanasiasa, wawekezaji na wateja wake kufuatia kashfa ya data na hivyo kupelekea mmiliki wake Mark Zuckerbag kuomba msamaha kwa ukiukaji wa sheria ya data ulioathiri zaidi ya watu milioni 50, hata hivyo Msamaha huo, haukuwazuia wawekezaji kutouza hisa zao huku wengi wakishangazwa ni kiwango cha uharibifu huo utakavyoathiri mtandao huo wa kijamii.

Katika mtandao huo wa kijamii, hisa zilishuka kutoka $176.80 siku ya Jumatatu hadi $159.30 siku ya Ijumaa jioni.

Awali inaelezwa kuwa, hisa za facebook ziliuzwa kwa $38 kila moja na hivyobasi kuipatia kampuni hiyo thamani ya kibiashara ya $104b, lakini kufuatia ukuwaji thabiti na utawala katika matangazo ya kidijitali, hisa za facebook zilipanda hadi $190 kufikia Februari mwaka huu.

Mchanganuzi mkuu katika kampuni ya utafiti ya Pivital, Brian Wieser alisema kuwa alipata matokeo mabaya ya hisa za facebook .

”Nilikuwa nikilenga $152 katika facebook mwaka 2018 na hiyo ilikuwa kabla ya kisa cha kashfa iliotokea wiki hii”.

Bwana Wieser anasema kuwa kushuka kwa bei ya hisa kulionyesha kuwa wawekezaji waliogopa kuongezeka kwa udhibiti mbali na wateja kuondoka katika mtandao huo lakini kulikuwa na hatari chache kwa wamiliki wa matangazo kuondoka facebook.

Mojawapo ya siri na ufanisi wa Facebook inayoelezwa, ni kiwango cha wateja wanaojiunga na facebook kinazidi kuwapendeza wateja wake. Lakini cha kushangaza ni kwamba ni wembe huohuo unaoinyoa facebook wakati inapopoteza idadi kuu ya watumiaji wake kutokana kashfa hiyo.

Na BBC.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *