michezo

Barcelona habari: Antoine Griezmann Hajafanya Uamuzi Juu ya Uhamisho Wake Kwa Msimu Ujao.

on

Antoine Griezmann hajui ataichezea timu ipi msimu ujao, Kulingana na maneno ya Diego Godin kutoka Atletico Madrid.

 

Mchezaji huyo wakifaransa anahusishwa kwa kiwango kikubwa juu ya kuhamia katika timu ya Barcelona kwa miezi ya hivi karibuni baada ya kukataliwa ofa hiyo msimu uliopita.

Griezmann amekataa kuongelea kuhusu kubaki clabuni hapo mpaka mwisho wa msimu huu.

Lakini watu wengi wanatarajia kuwa mchezaji huyo atafanikisha uhamisho huo kwenda Nou Camp msimu ujao kwa donge nono la fedha.

Kwa hali yoyote Godin amesisitiza kuwa Griezmann bado hajafanya maamuzi juu ya wakati ujao na kusisitiza kuwa hakuna mtu anaejua juu ya hilo na pia hawadhani kama yeye pia anajua juu ya uhamisho wake kwa msimu ujao.

Na

-Innocent Chambi-

 

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *