habari

Barcelona: Malefu Waandamana Kupinga Kukamatwa Viongozi Wa Catalonia.

on

Maelfu ya watu wameandamana mjini Barcelona Jumapili hii kupinga kuwekwa kizuizini viongozi tisa wanaogombania kujitenga kwa jimbo la Catalonia, ambao wanakabiliwa na kesi ya mashtaka ya uasi.

Maandamano hayo yamekuja siku kumi baada ya mahakama ya Ujerumani kutupilia mbali ombi la Uhispania la kumtaka Carles Puigdemont kiongozi wa zamani wa Catalonia anayeongoza vuguvugu hilo la kutaka kujitenga arejeshwe nyumbani kwa mashitaka ya uasi na badala yake mahakama hiyo ilimuachilia huru kwa dhamana.

Jimbo la Catalonia limekuwa katika mkwamo wa kisiasa tokea serikali kuu ya kihafidhina ya Uhispania kuchukua udhibiti wa moja kwa moja wa jimbo hilo baada ya kujitangazia uhuru mwezi Oktoba. Chaguzi nyingine za majimbo zitaitishwa iwapo kiongozi mpya wa jimbo hilo hatochaguliwa hadi ifikapo Mei 22.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *