michezo

Barcelona Yamsajili Mwingine Kutoka Brazil.

on

Winga wa Brazil Malcom amekamilisha uhamisho wa kitita cha £36.5m kwa kujiunga na Barcelona kutoka Bordeaux.

Mkataba huo ulitangazwa mara ya kwanza siku ya Jumanne baada ya mabingwa hao wa Uhispania kuwashinda Roma katika kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21aliyefunga magoli 20 na kuandaa mengine 13 katika mechi 84 za Bordeaux

Ni mchezaji wa pili wa Brazil kusajiliwa na klabu hiyo msimu huu baada kiungo wa kati Arthur kujiunga kutoka Gremio kwa dau la £35.5m.

Barcelona pia imemsajili beki wa kati wa Sevilla Clement Lenglet kwa kitita cha Yuro milioni 35.9 (£32m).

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *