habari

BENKI KUU YA TANZANIA YAPONGEZA UBUNIFU WA BENKI YA NMB KATIKA KURAHISHA HUDUMA ZA KIBENKI NCHINI

on

proxy?url=http%3A%2F%2Ffullshangweblog.com%2Fhome%2Fwp-content%2Fuploads%2F2018%2F08%2F2-35
Bi. Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Hyyat jijini Dar es salaam.proxy?url=http%3A%2F%2Ffullshangweblog.com%2Fhome%2Fwp-content%2Fuploads%2F2018%2F08%2F3-36
Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Dk.Benard Kibese akiwa amekaa pamoja na wageni mbalimbali waalikwa na viongozi wa benk ia NMB wakati wa hafla ya uzinduzi huo.proxy?url=http%3A%2F%2Ffullshangweblog.com%2Fhome%2Fwp-content%2Fuploads%2F2018%2F08%2F4-26
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo mbalimbali Benki ya NMB wakiwa katika hafla hiyo.proxy?url=http%3A%2F%2Ffullshangweblog.com%2Fhome%2Fwp-content%2Fuploads%2F2018%2F08%2F5-25proxy?url=http%3A%2F%2Ffullshangweblog.com%2Fhome%2Fwp-content%2Fuploads%2F2018%2F08%2F6-16
Bi. Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB akiwa pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo katika uzinduzi huo.proxy?url=http%3A%2F%2Ffullshangweblog.com%2Fhome%2Fwp-content%2Fuploads%2F2018%2F08%2F7-13
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi huo.proxy?url=http%3A%2F%2Ffullshangweblog.com%2Fhome%2Fwp-content%2Fuploads%2F2018%2F08%2F8-10proxy?url=http%3A%2F%2Ffullshangweblog.com%2Fhome%2Fwp-content%2Fuploads%2F2018%2F08%2F9-10
Bi. Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB pamoja na Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.

*Yazindua huduma ya Klik App NMB inayowezesha kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeipongeza Benki ya NMB kwa uamuzi wake wa kuzindua huduma ya kufungua akaunti kwa kutumia mtandao wa simu ya mkononi.

Imesema hatua hiyo imethibitisha namna benki hiyo inavyotumia ubunifu na kukua kwa teknelojia ya mawasiliano kwa kurahisisha huduma za kibenki nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Dk.Benard Kibese wakati akizindua Klik App ya NMB inayowezesha mteja kufungua akaunti kupitia simu ya kiganjani.

Amesema kuwa ubunifu huo ambao umefanywa na benki ya NMB utarahisha watanzania wengi kufungua akaunti za benki hiyo kupitia simu zao na kwamba hivi sasa watumiaji wa simu za mkononi ni wengi na hivyo huduma hiyo ya NMB imekuja wakati sahihi.

“Tunaipongeza NMB kwa ubunifu huu ambao wamekuja nao wa kuhakikisha wanatumia teknolojia iliyopo kuanzisha huduma za kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi na kizuri zaidi hata wenye simu za tochi bado wanaweza kufungua akaunti kupitia huduma hiyo,”amesema Dk.Kibese.

Amefafanua kuwa kama mnavyofahamu idadi kubwa ya Watanzania wanapotaka kununua bidhaa wanakwenda na fedha mkononi na hiyo imekuwa changamoto kubwa hasa ya usalama wa fedha.Lakini sasa NMB mbali ya kuja na huduma ya kukuwezesha kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi pia wanayo huduma nyingine ambayo inakuwezesha kununua bidhaa kwa kutumia simu.

“Kuna kifaa ambacho unatumia kupitisha kwenye simu yako na kupata huduma ambayo pia hata kwenye simu ya tochi bado atapata huduma.Kwa mazingira ya aina hii lazima tutoe pongezi kwa NMB kwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu kwa kutumia teknolojia iliyopo kurahisha huduma za kibenki nchini,”amesisitiza.

Ameleezea namna ambavyo huko nyuma yametokea mambo mengi ya uporaji wa fedha na wakati mwingine yamesababisha baadhi ya watu kuuawa kwasababu ya fedha ambazo wameshika mkononi lakini sasa NMB wamekuja na huduma ambayo inaweka usalama wa fedha kwani hakuna sababu ya kutembea na fedha mkononi.“Kuna kijana siku za nyuma alivamiwa na kuporwa Sh.milioni 10 na kibaya zaidi aliuawa .Hivyo kama kungekuwa na huduma kama hii ambayo NMB yangeendelea kuwa hai,”amesema.

Dk.Kibese amesema kwa sasa Watanzania wengi wanamiliki simu na kikubwa ni matumizi ya huduma za mtandao yaongezeke na kwamba wanachokifanya NMB ni kutimiza ndoto ya usalama zaidi wa fedha.Pia amesema NMB wanayo huduma ambayo inamuwezesha mtu kufanya miamala mbalimbali na kwamba benki hiyo wamekuja na App inayomuwezesha mtanzania kukopa kupitia simu.

“Bot inao wajibu wa kuangalia usalama wa fedha za mteja na pia kuhakikisha ubunifu katika nchi hii unapewa kipaumbele.Hivyo kwetu sisi tunayo sababu ya kuipongeza NMB kwa ubunifu huu ambao wamekuja nao,”amesema.

Ameongeza kitendo cha kutumia simu kufanya miamala mbalimbali ya kibenki maana yake inatoa nafasi ya fedha kuwa salama na ndicho ambacho BoT wanasimamia kuhakikisha kunakuwa na mifumo imara ya usimamizi wa fedha.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *