simulizi

Bongo Hapo Zamani: Hii Ndio Nyumba Namba Moja Iringa!

on

Ni ‘ Ikulu Ndogo’ Aliyoishi RC Dr Kleruu Aliyeuawa Na Mkulima Said Mwanwindi

Ndugu zangu, 

Ikulu Ndogo ya zamani ya Iringa, kwa maana ya makazi ya RC, imejengwa na Mjerumani mwaka 1906. Ndivyo inavyoonekana mpaka leo.

Ina master-bedroom. Bedroom tatu. Chumba cha kusomea , sebule kubwa, jiko na stoo. Style yake haijabadilishwa tangu Dr Kleruu aiache; madirisha, milango, ukuta na paa ni ile ile. 

Baada ya kuuawa kwa Dr Kleruu ma- Rc waliofuata ni kama walikuwa na woga nayo. 

Inasimuliwa, kuwa enzi za RC Dr Kleruu, alikuwa akisimama hapo mbele ya nyumba yake na kuongea na wananchi. Nyumba iko mlimani na mji wa Iringa unauona ukiwa kwenye baraza ya Ikulu Ndogo.

Kwanini nyumba hii inaogopewa?

Ni abrakadabra, si kitu kingine. Mfano, Serikali imegharakia kujenga nyumba ya DC Iringa wakati hiyo hapo pichani DC angeweza kukaa. 

Shida ukimweka DC au RC hapo, usishangae DC mzima akaamka asubuhi moja kutaka kuhama nyumba au kuhamishwa mkoa kabisa, kisa?  Atakwambia usiku amemwona Mkulima Mwamwindi anamjia na bunduki yake mkononi!

Naam, ingawa hivyo, kwa nyakati tofauti nyumba hiyo imetumiwa na jeshi. Si wengi Iringa wenye hata kujua ilipo nyumba hii muhimu iliyokuwa ya Serikali na yenye kumbukumbu muhimu ya kihistoria. 

Nami nimeipiga picha hiyo kuhifadhi kumbukumbu hiyo, maana siku hizi majengo kama haya ambayo ni hazina kwa taifa hayakawii kuvunjwa na kujengwa maghorofa.

Maggid Mjengwa

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *