simulizi

Bongo Hapo Zamani: Nyerere Alitoa Hadhi Maalum Kwa Rastafarians.

on

Ndugu zangu, Si wengi wenye kufahamu hoja ya diaspora na hadhi maalum. Ina historia yake Tanzania.

Disemba 12, 1985 Ofisi ya Rais, Ikulu ya Dar es Salaam ilitoa barua rasmi kuhusiana na ‘Waafrika walio ughaibuni’ hususani Nchi za Magharibi. Barua ilieleza kuwa Rais..”agreed with principal of black Africans returning to Africa” Kwamba amekubaliana na waafrika weusi warudi Afrika. Barua hiyo iliwalenga hususani Wajamaika. (Rastafarians).

Barua hiyo ilisainiwa na Ndugu Mizengo Kayanza Pinda aliyekuwa  msaidizi wa katibu wa Rais Ndugu Joseph Butiku.

Hilo likawa jibu rasmi la serikali kwa maombi ya Rastafarians yaliyoanzia na mkutano wa Mwalimu Julius Nyerere na kiongozi wa Rastafarians Jah Mkhululi Mwaka 1979.

Taarifa hizi za kitafiti zimeandikwa na mwandishi mwanamama Monique Bedasse (Jah Kingdom, Rastafarians, Tanzania, And Pan Africanism In The Rise Of Decolonization).

By Maggid Mjengwa.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *