We have 144 guests and no members online

Jux n vee-1

Mapenzi ya mwimbaji wa R&B Juma Jux na Vanessa Mdee a.k.a Vee Money sasa yamefikia kwenye ‘climax’. Licha ya kukiri hadharani kuhusu uhusiano wao lakini sasa kila mmoja wao amekuwa tayari kuelezea jinsi anavyompenda mwenzie hadharani ikiwa ni ishara ya kuwa mahaba yako kileleni.

Jux katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ambayo ilikuwa ni Sept 1, aliamua kuifanya kuwa siku maalum kumuandikia barua ya mapenzi Vanessa, lakini haikuwa barua ya kawaida kama tulivyozoea bali ni barua ya moyo wake kumzungumzia jinsi alivyobadili maisha yake toka wamekuwa wapenzi.

“Tomorrow is my birthday nitaifanya maalum kwa msichana aliye badilisha maisha yangu. Nitaiweka wazi barua ya moyo wangu ambayo huwa naisoma kila siku kwenye nafsi yangu.” Aliandika Jux Instagram siku moja kabla ya birthday yake.

Kupitia kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Jux akiwa na Vanessa walipata nafasi ya kuzungumzia mengi kuhusu uhusiano wao, na ndipo Jux alipewa nafasi na Diva kuisoma ile barua yake ya moyo kuhusu Vanessa.

Yafuatayo ni mambo sita ambayo Jux aliyasema kuhusu jinsi Vanessa alivyobadilisha maisha yake toka wawe couple.

1. Cha kwanza Jux alisema kuwa toka amekuwa na Vanesa Mdee mwaka 1 na miezi 8 sasa hajawahi kumcheat na msichana mwingine yeyote.

“Vanessa ni msichana wangu ambaye, huu ni ukweli naongea…ni mahusiano yangu ambayo nimekuwa na Vanessa halafu sijawahi kuwa na msichana mwingine yeyote, samahani kwa ma ex wangu nilikuwa nao lakini nilikuwa na maside chicks..Ni msichana ambaye nimekuwa nae na sijawahi kuwa na mwanamke mwingine yeyote kwa muda wa mwaka mmoja na miezi karibia nane.” – Jux

2.Kitu cha pili Jux alisema kuwa Vanessa amekuwa msaada mkubwa sana kwenye muziki wake kiasi ambacho hadi sasa kuna hatua kubwa ambayo ameipiga kutokana na miongozo yake.

Posted On Wednesday, 02 September 2015 11:04

11820548_1683409475227962_1535485925_n

Kupitia akaunti yake ya Instagram Lulu ameandika:

Nimeulizwa na Wengi na pengine yanasemwa mengi kuhusu ni Chama kipi cha Siasa nina support Kama ilivyoonekana Kwa Wasanii Wenzangu wengine..! Kwa kifupi nitajaribu kufafanua machache Kwa huu uwezo mdogo wa kufikiri nilijaaliwa na Mwenyezi Mungu..! Kwanza,kila binadamu/mwananchi ana uhuru wa kuchagua na ku support anachokipenda…kwahyo sitangaa wala kuchukia Flani ku support upande flani

Pili,Mimi Kama mm(binafsi)hii ni Mara yangu ya kwanza kupiga kura kwahyo nimeamua kuitumia Kwa busara na kuifanya iwe na kwanza isiyo na majuto Kwa kutofuata mkumbo wowote wa ndugu,jamaa,marafiki au watu walionizunguka..! Tatu,Nimependa kuitumia NAFASI hii zaidi Kwa UHUSIKA wa ELIZABETH na sio LULU nikimaanisha ikiwa kila kura ya mwananchi wa wakawaida ni ya siri na kuuridhisha moyo wake basi na mm nitakuwa mwananchi wa kawaida kbsa katika hili..! Nne,natoa pongezi Kwa wasanii wenzangu waloweza kushiriki Kwa namna moja au nyingine ktk ku support upande mmoja au mwingine kwani wameonyesha ujasiri na mapenzi ya kweli kwa vyama wanavyo support ila tu mabishano ya hoja ni mazuri zaidi na yanaweza kuepusha ugomvi au kuvunja mahusiano yetu ambayo yalikuwepo kabla ya uchaguzi na yatatakiwa kuendelea kuwepo baada ya uchaguzi..! tano,nawatakia kila la kheri wagombea wote na natumaini uchaguzi utakuwa wa sawa na haki..!

Posted On Wednesday, 02 September 2015 10:57

Posted On Wednesday, 02 September 2015 06:47

MWANAMKE: Ujasiri Katika Uamuzi Ndiyo Umenifikisha Hapa

Katika tamaduni za kimagharibi mtoto ana uhuru wa kuchagua afanye nini au ajikite kwenye taaluma gani ambayo anaona inafaa au kumvutia.

Wazazi nao huwa mstari wa mbele kumsaidia mtoto kwa kumuewekea mazingira rafiki ili aweze kutimiza azma au ndoto yake.

Tofauti na ilivyo katika tamaduni za Kiafrika ambapo wazazi ndiyo hutoa muongozo wa kile wanachotaka watoto wao wafanye katika maisha.

Inapotokea mtoto au kijana akachagua kufanya kitu tofauti na matakwa ya wazazi wake huonekana mkaidi na anayejitafutia kuwa na maisha mabaya.

Pamoja na kuwapo kwa kasumba hiyo wapo watoto ambao wanasimamia kile wanachokiamini na kukiweza hivyo kujikuta wakifanikiwa na kuwashangaza wazazi.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mwigizaji Godliver Gordian nyota wa tamthilia ya ‘Siri ya Mtungi’ anayefahamika zaidi kama Cheusi.

Wengi walimfahamu Cheusi kupitia tamthilia hii iliyovuta hisia za watazamaji wa vipindi vya runinga alipocheza kama mke wa mhusika mkuu Cheche.(P.T)

Posted On Monday, 31 August 2015 05:02

01_55558.jpg

 Makamu wa Rais wa Star Times Group kutoka Beijing China Michael Dearharm akitoa hotuba ya uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachokuwa kinarushwa na Televisheni ya Star Times katika nchi za Afrika Mashariki wakati wa hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es salaam.

02_5dd3c.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Star Times Group nchini Langtang Liao akimkaribisha Makamu wa Rais wa Star Times Group kutoka Beijing China Michael Dearharm wakati wa hafla ya uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachokuwa kinarushwa na Televisheni ya Star Times.

03_efd74.jpg

Mtayarishaji wa Kipindi cha Mashariki Max kitakachokuwa kinarushwa na Televisheni ya Star Times katika nchi za Afrika Mashariki Roby Bresson akiwatambulisha watangazaji wa kipindi cha Mashariki Max kitakachokuwa kinarushwa na Televisheni ya Star Times Jokate Mwegelo na Sarah Hassan (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kipindi hicho jijini Dar es salaam.

04_50270.jpg

Watangazaji wa kipindi cha Mashariki Max kitakachorushwa na Televisheni ya Star Times wakati wa uzinduzi wa kipindi hicho jijini Dar es salaam. Kulia ni Jokate Mwegelo na Sarah Hassan (kushoto).(P.T)

Posted On Monday, 31 August 2015 04:31

Wasanii wa Kundi la The W.D kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% 2015 lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oystebay Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.

Vijana wanaunda kundi la Timu Makorokoro wa wilaya ya Temeke jijijini Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la robof wa shininali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.

Vijana wanaaunda kundi la timu ya Shamba kutoka Temeke wakionyesha umahiri wa kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay jijini Dar es Salaam ,mwishoni mwa wiki.Shindano hilo iliandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania. Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.(P.T)

Posted On Sunday, 30 August 2015 12:25

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa matamasha mbalimbali kama lile la Krismas na Pasaka, Alex Msama (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana asubuhi kuhusu uzinduzi wa Tamasha la kuliombea Taifa kuelekea ucahguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu utakaofanyika Oktoba 4, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Benno Chilele (kushoto), akizungumza katika tamasha hilo. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa Tamasha la Krismas na Pasaka, Alex Msama.

Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.(VICTOR)

Posted On Sunday, 30 August 2015 06:44

NI maisha ya nguli wa filamu Bongo, Jacob Stephen Mbura ‘JB’. Anasimulia kila kitu alichopitia maishani mwake tangu kuzaliwa hadi sasa alipo. Hakika ni simulizi ambayo imejaa kila aina ya mafunzo kuhusu maisha na changamoto zake.

Kikubwa katika simulizi hii, ni kuwatia moyo watu wenye ndoto kama zake au nyingine, kutokata tamaa pindi wanapokumbana na matatizo wakati wa kufuatilia ndoto zao. Kujaribu kupandikiza na kufufua mbegu za ushindi miongoni mwa watu wenye malengo na ndoto kubwa.

Simulizi ya maisha yake imejaa dhoruba kubwa, vimbwanga na vichekesho vingi kwa baadhi ya mapito yake katika kusaka mafanikio maishani. Wiki iliyopita, aliishia kueleza namna na jinsi ambavyo walianza kufanya kazi na muigizaji mwenzake, Single Mtambalike ‘Richie’ na baadaye kutengana na Richie kuanzisha kampuni yake ya kuzalisha filamu ya Bulls Entertainment.
Je, nini kitafuata? Yumbayumba nayo hapa chini.

“Kwa hiyo Richie akawa ameondoka, hata hivyo kama nilivyosema hapo awali, niliumia sana lakini kamwe sikukata tamaa kabisa, nikaamua kumtafuta mtu mmoja aitwaye Adam Philip Kuambiana (marehemu),” anasema JB huku akipunguza sauti kwa chini sana.(P.T)

Posted On Saturday, 29 August 2015 08:55

Posted On Friday, 28 August 2015 09:33

Neno moja huweza kubadilisha maisha ya mtu, hayo yamemkuta msanii wa muziki nchini Tanzania

Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Abubakar Shaaban Katwila almaarufu Q Chillah aliyekuwa ameathiriwa na dawa za kulevya kiasi cha kushindwa kuendelea kuiburudisha hadhira, ameamua kuitoa siri yake kwa BBC namna alivyoweza kuachana na uraibu, sababu kubwa ni neno aliloguswa kutoka kwa bintiye.

Sikiliza mahojiano yake na Anord Kayanda.BBC

 

Posted On Friday, 28 August 2015 09:30

KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’.

KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ amefungukia ujio wake wa sasa wa Ngoma ya Amerudi aliyoizindua mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa hatoi wimbo mpya ili apate tuzo.

Staa huyo anayebamba na Ngoma ya Nashindwa, aliwaambia mashabiki wa muziki wa Dansi waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar katika uzinduzi wa wimbo wake huo wa audio na video kuwa anashangazwa na wasanii wanaokimbilia kutoa wimbo mpya ili wapate tuzo.

“Kila siku nikilala nawaza mashabiki wangu nifanye nini muendelee kunipenda nisije kufulia. Nawaandalia ngoma kali na zinazodumu mwaka hadi mwaka.

“Malaika Music ina miaka miwili sasa lakini ina wimbo mmoja tu uliofanya vizuri wa Nakuhitaji na wimbo huo una zaidi ya mwaka mpaka leo ukipigwa ni kama mpya. Leo (Ijumaa) tunazindua Amerudi na yenyewe itadumu miaka na miaka.
“Wengi wanafikiria kutoa wimbo mpya ili wapate tuzo, sisi kwetu hatupo hivyo na hata mimi sipo kwa ajili hiyo,” alisema Bella.GPL(P.T)

Posted On Friday, 28 August 2015 09:24

 

Posted On Monday, 24 August 2015 05:17
Page 9 of 54

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart