We have 151 guests and no members online

index

MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini, Rebecca Malope, amepongeza wazo la kuwepo Tamasha la Amani linalotarajiwa kufanyika Dar es Salaam Oktoba 4 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema tayari wasanii mbalimbali wa kimataifa wameguswa na uwepo wa tamasha hilo.
“Tumepanga kuwa na tamasha la amani Oktoba 4, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na baadaye mikoa mbalimbali nchini.
“Wasanii wa Injili wa ndani na nje wamepongeza wazo hilo na wameonekana kuguswa kwa kiasi kikubwa akiwemo Malope.
“Amenijulisha kwamba tukimuhitaji yupo tayari wakati wowote kufanya naye kazi kwenye tamasha hilo. Bado tunajipanga na mambo yakiwa mazuri tutamualika,” alisema Msama.
Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

Posted On Monday, 24 August 2015 02:51

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Paul Makonda akiongea na wasanii (hawako pichani) wakati akizindua semina ya siku moja kuhusu Umuhimu wa waanii kuwa na Bima ya Afya iliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Shirika la Taifa la Bima (NHIF) na kufanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Msanii Kimela Bila, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Joyce Fisoo.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza akisisitiza jambo wakati akiongea na Wasanii waliohudhuria semina ya Umuhimu wa Wasanii kujiwekea Bima ya Afya iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ndugu Paul Makonda.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mifuko ya Afya ya shirika hilo Ndugu Eugen Mikongoti akiongea na wasanii juu ya madhumuni ya semina hiyo ya wasanii. (P.T)

Posted On Sunday, 23 August 2015 06:20

Mshumaa wa wiki ni kipengele kinachozungumzia kuhusu msanii ama kundi la muziki wa zamani katika kipindi cha Mishumaa ya Kale

Kipindi hiki hukujia kila Ijumaa kuanzia saa 11 jioni mpaka 1 usiku kwa saa za Marekani ya Mashariki

Kinatayarishwa na kurushwa na Vijimambo Radio na Kwanza Production, kwa ushirikiano na NesiWangu Media

Posted On Sunday, 23 August 2015 04:12

11373888_852445964863527_348235188_n

Diamond akiwa studio jijini Johannesburg kuandika na kurekodi sehemu ya wimbo huo

Mafikizolo tayari wameshaingiza sauti zao na aliyekuwa anakisubiriwa ni Diamond ambaye huenda leo akamaliza sehemu yake.

Studio Joburg South Africa Muda huu nikirecord nyimbo kwajili ya kutokomeza Umasikini Africa.... #TellEveryone #SustainableDevelopment @TheGlobalGoals,” ameandika Diamond kwenye picha aliyoweka Instagram.

Fresh kutoka kurekodi wimbo na Ne-Yo, Diamond Platnumz amekwea pipa kutoka Nairobi kwenda nchini Afrika Kusini kuungana na Mafikizolo kurekodi wimbo uitwao ‘Tell Every One’ ambao ni sehemu ya kampeni ya dunia ya kutokomeza umaskini, maradhi, njaa na matatizo mengine, The Global Goals.

 

Posted On Saturday, 22 August 2015 04:42

 Rapper wa muziki kutoka Marekani Future ameachia video yake mpya ya wimbo unaoitwa “Where Ya At” akiwa maemshirikisha Drake.

Posted On Saturday, 22 August 2015 04:27

 

Jaji Mkuu wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Roy Sarungi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo Katika ofisi za Proin Promotions Ltd juu ya mchakato mzima wa fainali ya TMT itakayofanyika tarehe 22 August 2015 Katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta kwa kiingilio cha Shilingi Elfu Hamsini (50000) kwa viti maalumu na shilingi elfu thelathini (30000) kwa viti vya Kawaida.Mshindi katika fainali hiyo itaondoka na kitita cha Shilingi milioni hamsini (50,000,000) za Kitanzania.(P.T)

Posted On Thursday, 20 August 2015 03:12

 

IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON

Posted On Wednesday, 19 August 2015 16:51

Mkazi wa Mwembeyanga Bi. Sikudhani Idd (katikati) akipokea zawadi yake ya bia za bure, mfuko pamoja na Tisheti alivyopewa wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Kisuma ya Mwembeyanga Tandika mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker toka kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habbash na (kulia) ni balozi wa bia hiyo Bi. Veronica Mbilinyi

Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash akielezea utaratibu wa utoaji zawadi kwa wapenzi wa bia ya Tusker waliofika katika baa ya Kisuma wakati wa kuipongeza baa hiyo iliyopo Tandika jijini Dar es salaam. Baa hiyo ilibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker lengo likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli pale wanapotoa huduma kwa wateja.(VICTOR)

Posted On Tuesday, 18 August 2015 14:59

pic-ludenga_783c7.jpg

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limelifungulia shindano la urembo la Miss Tanzania baada ya mwandaaji wake Kampuni ya LINO International Agency Limited kufuata taratibu, kuomba radhi na kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.

Itakumbukwa kuwa mnano tarehe 22/12/2014 BASATA liliwaandikia barua LINO International Agency Limited ya kulisimamisha shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili (Mwaka 2015 na 2016) na kuwaagiza kujipanga upya na kurekebisha kasoro ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.

Mapungufu yaliyobainishwa ni pamoja na; mosi, kutokufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji matukio ya Sanaa nchini, pili kutokuwasilisha nyaraka mbalimbali za shindano lake hususan mikataba ya washiriki. Tatu kutumia mawakala wasiosajiliwa na kupewa vibali vya BASATA.(P.T)

Posted On Monday, 17 August 2015 11:27

flaviana ndoa (1)

Mwanamitindo Flaviana Matata na Deogratius Massawe baada ya kufunga pingu za maisha juzi.

flaviana ndoa (2)

Massawe akimbusu mkewe.

flaviana ndoa (3)

Mwanamitindo Flaviana Matata akiwa katika pozi na mumewe Deogratius Massawe.(P.T)

Posted On Monday, 17 August 2015 03:33

Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la Wasanii, Simon Mwakifamba.

Mshindi kwa upande wa wachekeshaji, Nurdin Bakari 'Balotelli' akitoa kichekesho mbele ya Rais KIikwete.

Mmoja wa washiriki akiimba.

Mpoki (wa pili kutoka kulia) akiwa na washindi wa Kinondoni Talent Search. (P.T)

Posted On Monday, 17 August 2015 03:27

diamond p

Diamond Platnumz anaendelea kupata nominations za tuzo mbalimbali ndani na nje ya Afrika, ambapo hivi sasa amechaguliwa kuwania tuzo mbili za International Reggae and World Music Awards (IRAWMA) 2015 za Marekani.

Baba Tiffah amechaguliwa kuwania kipengele cha ‘Best African Song’ kupitia wimbo wake ‘Nana’ aliomshirikisha Flavour wa Nigeria, pamoja na ‘Best African Entertainer’.

“Alhamdulilah… ndugu zangu kijana wenu nimechaguliwa tena kwa tunzo za IRAWMA za Nchini Marekani…kama Mburudishaji bora wa Africa na nyimbo ya #NANA kama Nyimbo Bora ya Africa…kama mnakumbukumbu nzuri mwaka jana tuliweza kuishinda Tunzo hii… ambapo #MdogoMdogo ilishinda kama Nyimbo bora ya Kiafrica na mimi kama Mburudishaji bora wa Africa… InshaAllah, Naamini na mwaka Huu pia itakuja Nyumbani #JonsWeekend.” Ameandika Diamond Instagram.

Nyimbo nyingine zinazoshindanishwa katika kipengele hicho ni “Enemy Solo”ya Awilo Longomba aliowashirikisha P-Square, “Original” ya Fally Ipupa, “Dance 4 Me Remix” ya J.Martins ft. Koffi Olomide na “Garlie O Remix” ya Patoranking ft. Tiwa Savage.

Tuzo hizo zitatolewa October 4,2015 huko Florida, Marekan

Kilonge

Posted On Friday, 14 August 2015 11:07
Page 10 of 54

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu