We have 180 guests and no members online

 

Posted On Friday, 18 December 2015 23:16

Posted On Friday, 18 December 2015 19:47

 

 

Posted On Friday, 18 December 2015 19:42

 

Posted On Friday, 18 December 2015 19:39

Bob Junior Sharobaro

Muimbaji na mtayarishaji wa muziki wa Sharobaro Records, Bob Junior amesema tayari kolabo yake na Diamond imekamilika.

Ameutaja wimbo huo kuwa unaitwa ‘I Am Praying for You.

Bob amefunguka kuwa kazi hiyo imechukua muda mrefu kukamilika kutokana na wawili hao kuwa busy.

“Naomba Mungu kazi itoke mwaka huu kwa sababu itakavyozidi kuchelewa itakuwa ni issue nyingine. Kazi imekamilika kwa kiasi chake ndio maana nasema itatoka mwaka huu,” amesema.

Bob Junior pia amewataka mashabiki wake kuwa na subira licha ya kuwaahidi mara kadhaa kuachia kazi mpya.

Posted On Friday, 18 December 2015 19:37

 

Posted On Friday, 18 December 2015 19:14

Posted On Thursday, 17 December 2015 15:01

 

Posted On Thursday, 17 December 2015 14:57

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya marekebisho ya kanuni za usajili ambapo sasa mchezaji ambaye usajili wake utakuwa umepita kwenye mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS) atapewa leseni na kuitumikia moja kwa moja timu yake mpya.

TFF itatoa leseni ya usajili wa mchezaji ambaye amethibitishwa kupitia mtandao wa TMS baada ya kuwepo nyaraka zote; mkataba uliomalizika, barua ya kuvunja mkataba, barua ya kuachwa (release letter), mkataba mpya na uthibitisho wa makubaliano kati ya klabu zinazohusika.

Licha ya mchezaji kupata leseni, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji bado itakuwa na mamlaka ya kushughulia upungufu, malalamiko ya kiusajili, pingamizi na uhalali wa kimkataba kati ya pande mbili (mchezaji na klabu).

Wachezaji wote wa kigeni waliosajiliwa kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) wanapaswa kulipiwa dola za kimarekani U$ 2,000 kwa kila mmoja kabla ya kupatiwa leseni na kuanza kuzitumikia klabu zao katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.

Pia TFF kupitia kamati ya sheria na hadhi za wachezaji inaweza kumruhusu kwa kipindi maalum mchezaji mwenye dosari acheze kwa leseni ya muda (provisional license) hadi dosari hizo kati ya klabu na klabu zitakapomalizwa. Iwapo dosari hizo hazitakuwa zimemalizwa, mchezaji anaweza kuzuiwa kucheza na klabu husika kuadhibiwa.

Timu zote za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zinatakiwa kufuatilia TFF kujua wachezaji ambao hawana pingamizi na leseni za wachezaji waliopitishwa wanaweza kuanza kutumika kuanzia kesho tarehe 18/12/2015 na kwenye michezo ya kombe la Shirikisho (FA Cup) kama hawakuwa wamecheza raundi ya kwanza kwenye vilabu vya zamani.

Posted On Thursday, 17 December 2015 14:46

adele na dela

Dela ni muimbaji kutoka Kenya aliyeingia kwenye orodha ya wasanii wengi duniani waliofanya cover ya hit song ya muimbaji wa Uingereza, Adele-Hello, lakini yeye akiwa ameifanya kwa lugha ya Kiswahili.

Cover hiyo ya Kiswahili imesifiwa na watu wengi ikiwa ni pamoja na mtandao mkubwa wa Marekani, Perez Hilton waliodiriki kusema kuwa ni kali kuliko original version ya Adele.

Kupitia mtandao wao wameandika:

“Dela Maranga is a singer from Nairobi, Kenya, and her Swahili version of the 25classic may actually be better than the original. Her voice is powerful like Adele’s, but she also has this soulful tone that makes the lyrics even more painful — in the best way possible.”

Baadhi ya watu mwenye mitandao ya kijamii wameonekana kuikubali sana na kumshauri afanye video kama walivyofanya wasanii wengine waliofanya cover ya wimbo huo.

Kwa wasiomfahamu vizuri Dela, ni yule aliyewahi kushirikishwa kwenye wimbo wa AY – ‘Asante’.

Usikilize hapa

Posted On Thursday, 17 December 2015 09:34

YounG KILLER

Young Killer Msodoki ni msanii kutoka Rock City, Mwanza aliyeibuliwa kwenye shindano la Fiesta Super Nyota la mwaka 2012, na hadi mwaka huu anafikisha miaka mitatu kwenye muziki.

Rapper huyo ameshare mafanikio aliyoyapata toka alivyoingia rasmi kwenye muziki miaka mitatu iliyopita.

“Mafanikio ambayo nimeyapata kwanza ni kujuana na watu ambao nilikuwa naamini wanaweza wakaja kuwa watu muhimu katika maisha yangu na nilikuwa nikipenda nije kukutana nao,” alisema Young Killer.

“Kitu cha pili nimeweza kumsaidia nyumbani bi mkubwa, nimemjengea nyumba na sasa hivi iko katika finishing lakini nyumba ishasimama na mama yangu anauweza kuishi yaani iko tayari lakaini kuna viurembo urembo tu vya kumalizia.”Alieleza Young Killer.

“Pia naishi vizuri kupitia muizki wangu, naishi kwangu nagari yangu ya kutembelea matembezi yangu madogo madogo.”

Baada ya kufanikiwa kupata show za kampeni mwaka huu, rapper huyo amesema sehemu ya pesa aliyolipwa amenunua kiwanja maeneo ya Chamanzi.

“Pia kitu kikubwa ambacho nimeweza kufanikiwa pia siku za karibuni hapa nimechukua kiwanja ambacho naamini katika kumalizia nyumba ya bi mkubwa wangu nitaanza na mimi kuporomosha dude langu ambalo nahisi ndio litakuwa linanipa ubize sana katika hela zangu pia ambazo nitakuwa nazipata kidogo kidogo” alimaliza Young Killer.

Posted On Thursday, 17 December 2015 09:32

12301398_1675226496024383_418418585_n

Diamond na mchumba wake Zari The Bosslady wataiteka Kampala, Uganda wikiendi hii.

Wote watakuwa na show tofauti.

Zari atakuwa na All White Party Alhamis hii kwenye kiota cha Guvnor huku Diamond Ijumaa hii akitumbuiza kwenye uwanja wa cricket wa Lugogo akiwa na msanii wa Nigeria, Patoranking kwenye show ya Born 2 Win.

Tayari Zari ameshawasili nchini humo huku Diamond akitarajiwa kuwasili leo au kesho.

Posted On Thursday, 17 December 2015 09:28
Page 2 of 54

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli