We have 142 guests and no members online

Chungu Cha Tatu

kizungumza na gazeti la Mtanzania hivi karibuni , JB alisema akiisema gharama ya filamu hiyo TRA watataka kujua pesa hizo amezipata wapi.

“Nikisema nitaje gharama iliyotumika na niliyowalipa wasanii nadhani TRA itawafuata, lakini nimetumia gharama kubwa mno naweza kuthubutu kusema imezidi gharama za filamu zangu zote chini ya Jerusalem,” alisema JB.

Alisema licha ya gharama hizo lakini filamu hiyo inatoa somo kwa wanandoa wengi ambao wana tabia mbalimbali zinazokera hivyo wajifunze na wabadilike kwani kuna mambo ambayo yanachangia kuvunja ndoa.

Filamu hiyo iliyoingia sokoni hivi karibuni ina mastaa, Jacob Stephan aka JB , Wema Sepetu, Pacho Mwamba, Mau pamoja na mastaa wengine.

Posted On Tuesday, 15 December 2015 06:27

Posted On Tuesday, 15 December 2015 03:00

 

Posted On Monday, 14 December 2015 15:17

 

Posted On Monday, 14 December 2015 15:15

Mwanamuziki na mtangazaji wa redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana , kuhusu onyesho lake atakalolifanya leo katika fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam na kesho ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani Dodoma katika Tamasha la Instagram Party Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba ambao wamemleta msanii huyo hapa nchini kwa kushirikiana na Kampuni ya C&G Solutions na kulia ni Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.

Meneja Mawasiliano wa Freconic Ideaz, Krantz Mwantepele (kushoto), akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kampuni yao itaendelea kuleta wanamuziki wengine kutoka pande mbalimbali za dunia kama walivyofanya kwa Robarto Amarula.

Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia (kulia), akizungumza na wanahabari.

Mwanamuziki na mtangazaji wa Redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia, akifanya vitu vyake mbele ya wanahabari.(VICTOR)

Posted On Saturday, 12 December 2015 07:03

4K0A5075

Mjasiriamali na mbunifu wa mavazi nchini, Khadija Mwanamboka amesema ubunifu anaoutumia kwenye mavazi, aliuhamishia kwenye biashara yake ya mgahawa wa vyakula ‘VVK’ ndio maana mwezi huu unatimiza mwaka mmoja ukiwa na mafanikio makubwa.

Khadija ameeleza kuwa kupitia mgahawa huo wa VVK ambacho ni kirefu cha Vitu Vya Khadija uliopo Block 41 Kinondani, jijini Dar es salaam, amesema dani ya mwaka mmoja ameweza kuvuka matarajio ya kuwafikia wateja wengi zaidi.

“Nimeamua kuwa serious kwenye hii restaurant kwa sababu wateja wetu wamekubali huduma zetu. Mimi kama mbunifu wa mavazi kuingia kwenye sekta ya chakula haikuwa ngeni. Mimi ni mbunifu wa mavazi kwahiyo nilihamisha ule ubunifu wangu kwenye upande wa chakula,” amesema.
Basicaly hata chakula ninachouza ni chakula ambacho hata mimi nakipenda. Ni chakula ambacho mimi najua kukipika,” ameongeza.

Khadija anasema baada ya kuweza kuwafikia wateja wao wengi ndani ya mwaka mmoja, sasa wamejipanga kutoa ofa nyingi kwa wafanyakazi wa maofisini.

“Tuna plan kubwa sana ya kuboresha huduma,” anasema.

“Tunataka kuwa na ofisi ambazo zitakuwa VVK members. Kwa mfano labda kwenye ofisini kuna watu 15 wamejisajiri, watu hao watapata chakula kwa nusu ya bei, kama mfano biriani ni shilingi 10,000, wao watapata kwa shilingi 5,000 kila siku. Mungu akipenda utaratibu huu utaanza mwezi wa pili lakini kwa kipindi hiki wanaweza kuendelea kupata huduma zetu za kila siku na baadaye tutawatangania kwa kutumia mitandao yetu ya kijamii pamoja na tovuti yetu.”

Pia Khadija amesema wanatoa huduma za chakula kwenye sherehe mbalimbali pamoja na kutoa ushauri.

Posted On Saturday, 12 December 2015 04:54

 

Posted On Saturday, 12 December 2015 04:49

 

Posted On Friday, 11 December 2015 16:56

 

Posted On Thursday, 10 December 2015 16:43

Posted On Saturday, 05 December 2015 03:34

fl1

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akielezea namna sekta ya Filamu ilivyo piga hatua hapa nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Genofeva Matemu na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Fatma Salum.

fl2

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo uliokuwa unahusu ukuaji wa sekta ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHVUM

Na Jovina Bujulu-MAELEZO

Sekta ya filamu imekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa jumla ya ajira 732,681ikiwa ni mchango wake katika kutatua tatizo la ajira nchini kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Joyce Fissoo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Fissoo alifafanua kuwa idadi hiyo ya ajira zilizotolewa inajumuisha wataalamu wa filamu 944 na wadau wengine wasio wataalamu 731,737 ikilinganishwa na takwimu zilizotolewa na Shirika la Milki Bunifu Ulimwengini liliripoti kuwa mwaka 2007 tasnia ya filamu iliajiri watu 36.

‘Katika kipindi cha miaka ya 2000 utengenezaji wa filamu umebadilika kutoka ule wa awali wa kuburudisha na kuelimisha na kuwa biashara inayoingiza kipato na kutoa ajira katika jamii hivyo kuongeza kipato cha Taifa letu”. Alisema Fissoo

Aidha, kuanzia miaka ya 2000 sekta binafsi ilianza kutengeneza filamu hivyo filamu zilianza kufadhiliwa, kutengenezwa, kumilikiwa na kusambazwa kwa kiasi kikubwa na wadau na makampuni binafsi hivyo kupelekea ongezeko kubwa la makampuni ya uzalishaji na usambazaji kutoka kampuni 1 miaka ya 2000 hadi kufikia makampuni 250 mwaka 2015.

Tasnia hiyo imechangia kukuza uchumi wa nchi na ule wa mtu binafsi ambapo kwa mujibu wa Shirika la Milki Bunifu Ulimwenguni (WIPO) kwa mwaka wa 2007 ilichangia shilingi 2,134,860 na kufikia mwaka 2010 ilichangia shilingi 11,398,440, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 433.9.

Akizungumzia ukuaji huo wa tasnia ya filamu, Fissoo alisema kuwa ukuaji wa teknolojia umepelekea utumiaji wa vifaa vyenye teknolojia ya hali ya juu vilivyowekezwa na baadhi ya wadau vinavyopatikana kirahisi kama vile kamera za kisasa, na mashine za kufungashia kazi za filamu hivyo kupunguza gharama za uzalishaji wa filamu nchini.

Aidha, kumekua na uuzaji wa filamu kwa njia ya mtandao suala linalopanua wigo wa masoko na kuitangaza nchi kwa wepesi zaidi hivyo kupelekea umahususi wa mandhari ya Tanzania kutumika na watengenezaji wa ndani na makampuni ya nje yapatayo 169 kutengeneza filamu mbalimbali.

Tasnia ya filamu nchini imeendelea kukua na kushamiri kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo na wadau wa ndani ya nchi ikiwemo kuandaa, kuratibu na kuendesha matamasha na Tuzo za Filamu za Tanzania (TAFA),Tamasha la Filamu la Bara la Ulaya, Tamasha la Filamu la Misri, Tamasha la Filamu la India, Tamasha la Filamu la Bara la Asia, Tamasha la Filamu la Brazil na Arusha African Film Festival(P.T)

Posted On Wednesday, 02 December 2015 15:09

Posted On Sunday, 29 November 2015 03:59
Page 3 of 54

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart