We have 145 guests and no members online

 Alitanguliza audio ya wimbo huu mpya ‘Fine By Me’ siku ya jana, na sasa Chris Brown ameachia video yake.

Video hii imeongozwa na Breezy mwenyewe.

‘Fine By Me’ ni wimbo utakaopatikana kwenye album yake mpya ‘Royalty’ ambayo sasa watu wameanza kuruhusiwa kuweka oda kupitia iTunes.

Posted On Saturday, 28 November 2015 06:23

Star Female Artist, Fefe finally releases the visuals for her hit single "Make Sense". After a short spell with Capital hill Music, Fefe recently signed with Rebel Planet Management. She is preparing to release her EP titled "Mixed Feelings" which will include 9 mind blowing tracks.

Real Estate Company "Intellome" announced Fefe as the new brand ambassador for the company. 2016 seems to be a busy year for the female star.

Instagram: @kinggfefe
twitter: @kinggfefe
facebook: supadupafefe

 

Posted On Saturday, 28 November 2015 06:20

Meneja wa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kampuni hiyo kudhamini onesho la mwanamuziki Mousa Diallo kutoka nchini Mali litakalofanyika kesho katika Mgahawa wa Chakula na Vinywaji wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert na katikati ni Mwanamuziki, Moussa Diallo.

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja (kushoto), akizungumza na Mwanamuziki, Moussa Diallo (kulia). Katikati ni Mmiliki wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Carlos Bastos.

Mwanamuziki Moussa Diallo wa nchini Mali anayeishi Denmark (katikati), akiimba mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akijitambulisha ambapo leo atafanya onesho lake Ukumbi wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Slaam. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja ambao wamewezesha ujio wa mwanamuziki huyo na kushoto ni Ofisa  Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert.(P.T)

Posted On Thursday, 26 November 2015 04:16

KALLAJEREMIAH1

Staa wa muziki wa hip hop nchini, Kala Jeremiah.

Sweetbert lukonge, Dar es Salaam
STAA wa muziki wa hip hop nchini, Kala Jeremiah, ameamua kupanua wigo wa muziki wake baada ya kuanza harakati za kuhakikisha anatusua kimataifa.

Hatua hiyo inatokana na changamoto nyingi ambazo amekuwa akikumbana nazo kutoka kwa mashabiki wake ambao wamekuwa wakimsisitiza kufanya hivyo.

Kala ambaye ni zao la Bongo Star Search (BSS) aliiambia Mikito Jumatano kuwa kabla ya mwaka huu kumalizika lazima aikate kiu hiyo kwa kutoa ngoma na kichupa kikali ambacho kitachezwa kwenye runinga za kimataifa.

“Hivi sasa nipo katika harakati za kutoa wimbo mpya utakaoambatana na video kali itakayokuwa na viwango vya kimataifa ili niweze kukata kiu ya mashabiki wangu.

“Kwa sasa siwezi kuweka wazi jina la ngoma hiyo ila nina matumaini kuwa utafanya vizuri, pia video yake nitaifanyia hapa hapa nchini kwa viwango vya kimataifa, namuomba Mungu anijalie uzima ili niweze kutimiza mapema ndoto yangu hiyo,” alisema Jeremiah ambaye alitambulishwa zaidi kupitia Ngoma ya Wimbo wa Taifa aliyofanya na Nakaaya.(P.T)

Posted On Wednesday, 25 November 2015 14:08

MASHAUZI CLASSIC KUZINDUA ALBAM YA “SURA SURAMBI” NOVEMBA 26 MANGO GARDEN ...East African Melody, Cassim Mganga ndani ya nyumba

Hatimaye albam ya “Sura Surambi” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab, inazinduliwa Alhamisi hii Novemba 26.

Albam hiyo kutoka kwao Mashauzi Classic, itazinduliwa ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni huku kundi kongwe la taarab East African Melody, likisindikiza tukio hilo kubwa.

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ameuambia mtandao huu kuwa albam ya “SuraSurambi” inaundwa na nyimbo sita kali.

Ni Alhamisi ya kihistoria ambayo Isha anaitaja kuwa itapambwa na ratiba iliyokwenda shule itakayomwacha mshabiki apate uhondo mwanzo mwisho.

Isha amezitaja nyimbo hizo kuwa ni pamoja na “SuraSurambi” aliouimba yeye, “Kupendwa Bahati Yangu” uimbaji wake Abdumalick Shaaban, na “Mjinga Mpe Cheo” wa Zubeida Malick.

Nyimbo nyingine alizozitaja Ishani “Pendo la Ukakasi” wa Saida Ramadhan, “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzingana “Mapenzi Yamenivuruga” mwimbaji akiwa ni Naima Mohamed. Nyimbo zote hizo sita zimetungwa na Isha Mashauzi.

Mbali na Melody, mkali wa tungo za mapenzi wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga naye pia atasindikiza uzinduzi huo wa “Sura Surambi” ndani ya Mango Garden Alhamisi hii.(P.T)

Posted On Tuesday, 24 November 2015 08:20

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akifundishwa ngumi za kwenda kasi zilizo nyooka na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' Class anajiandaa na mpambano wake na  Twaha Kassimu 'Kiduku' Desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akielekezwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' jinsi ya kupiga ngumi za tumbo wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassim 'Kiduku' wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika uwanja wa basketboll shule ya uhuru Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS (P.T)

Posted On Sunday, 22 November 2015 06:11

1. Mshiriki miss Tanzania akichukua nafasi ya pili, 2014 Jihan Dimack akiwa kwenye red carpet iliyokuwa imeandaliwa.

Miss Tanzania aliyeshika nafasi ya pili, 2014 Jihan Dimack akiwa kwenye ‘red carpet’ iliyokuwa imeandaliwa.

2.Miss Tanzania 2014,Jihan Dimack akifanya mahojiano kwenye red carpet iliyokuwa imeandaliwa .

… Jihan  akihojiwa kwenye ‘red carpet’ iliyokuwa imeandaliwa .

3.Jihan (kushoto) akipiga picha za pozi na watu mbalimbali kwenye red carpet hiyo.

Mrembo huyo akipiga picha za pozi na mashabiki kwenye ‘red carpet’.(P.T)

Posted On Sunday, 22 November 2015 05:45

Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa pili kutoka kushoto) akishiriki katika uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania Oscar Shelukindo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli, Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, Alex Nkenyenge na Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.

Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa tatu kutoka kushoto) akishiriki katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu. --- GAPCO, kampuni ya mafuta inayoongoza Tanzania imetangaza udhamini wake wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016 kilomita 10 kwa walemavu.

Akitangaza udhamini huo jana wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi alisema GAPCO inaona fahari kudhamini mbio hizo za kilomita 10 kwa walemavu. “Tumeshuhudia mbio hizi za Kilimanjaro Marathon zikikua tangu tuanze kudhamini mwaka 2011 na pia kufurahia faida wanayopata washiriki na jamii inayozunguka maeneo ambayo mbio hizi hufanyika kila mwaka. Tunayo furaha kufanya kazi na Wild Frontiers ambao ndio waandaaji wa mashindano haya,” alisema Kakwezi.

“Kama sehemu ya kusaidia jamii ambayo tunafanya biashara, GAPCO Tanzania imeamua kusaidia wanariadha ambao ni walemavu kwa kudhamini mbio ambazo wanashiriki walemavu pekee,” alisema. Alisema udhamini wa GAPCO pia utahusisha usafiri, malazi na chakula kwa washiriki kutoka Dar es Salaam na pia zawadi za pesa kwa washindi wa mbio hizo za kilomita 10 ambazo zinafanyika pamoja na mbio nyingine za Kilimanjaro Marathon.

Kakwezi aliendelea kusema kuwa Kilimanjaro Marathon limekua tukio kubwa linalovutia washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania na hivyo limesaidia sana kutangaza vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro na pia kuwaongezea kipato wafanyabiashara wa Moshi.”. (P.T)

Posted On Thursday, 19 November 2015 03:49

Mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiongea na waandishi (hawapo pichani) wakati wa tukio la kumuaga kwa ajili ya kwenda nchini Marekani. Hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi ya Airtel Morocco jijini Dar Es Salaam. Pichani katikati ni Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde, akifatiwa na Mwalimu wa sauti Tony Joet.

Ofisa Uhusiano na Mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristed Kwizera (kushoto) akimuaga mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi. Anayeshuhudia (katikati), ni Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde.

MSHINDI wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga ameondoka nchini jana kuelekea Marekani kwa lengo la kupata mafunzo na kurekodi nyimbo yake. Nalimi Mayunga ameondoka jana usiku, kwenda kufanya kazi na nguli wa mzuki wa R&B nchini Marekani, Akon ambapo anatarajiwa kukaa huko kwa muda wa wiki moja kisha kurejea nyumbani Novemba 24, mwaka huu.

Akiongea wakati halfa ya kumuaga, Ofisa Habari Mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Aristide Kwizera alisema” Tunajisikia furaha kuona vijana wa kitanzania wakitangaza sanaa na nchi yetu duaniani kupitia muziki. Napenda kumpongeza sana mayunga kwa kupata ushindi ambao umempatia nafasi hii nono na kumwomba atumie vyema fursa hii. Sisi kama wadau wakuu wa sanaa nchini tunawapongeza sana Airtel kwa kuanzisha program zenye lengo la kukuza sanaa na muziki wa nchini kama hii ya Airtel Trace Music Stars na nyingine nyingi.

Naye mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alisema” ile siku niliyokuwa naisibiria kwa hama leo imefika na nimejipanga kuondoka kwenda kujifunza mengi na ya msingi katika maisha yangu ya muziki . Naamii safari hii itakuwa ni ya mafanikio makubwa na mwanzo wa hatua yangu ya mafanikia katika tasinia ya muziki

Napenda kuwaambia watanzania wajiandae kusikia kibao na video kali ntakayoifanya na Akon kwani nimejiandaa vya kutosha kuhakikisha nashirikiana nae vyema ili tunatoa nyimbo kali itakayowapa burdani wapenzi wa muziki pande zote duniani. Aliongeza Mayunga

Kwa upande wake Aliyekuwa jaji katika shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania na Mwalimu wa Muziki Tony Joet alisema” mayunga amekuwa akifanya mazoezi kujiandaa kwa deli hii toka alipotangazwa mshindi wa Airtel Trace Afrika. Ninaimani naye kwani ameonyesha uwezo mkubwa na nidhamu ya hali ya juu na naamini atafika mbali na namtakia kila laheri katika safari yake”

Akiongea kwa niaba ya Airtel Ofisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” mipango yote ya safari imekamilika na mayunga atakuwa marekani kwa muda wa wiki moja, tunaamini mayunga atakaporejea atakuwa tofauti kabisa na alivyokwenda na ndio hasa lengo letu sisi Airtel, kuwawezesha(P.T)

Posted On Tuesday, 17 November 2015 04:22

Msanii wa nyimbo za kizazi kipya Fid Q akitoa burudani kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Makongo jijini Dar es Salaam, wakati wa tamasha la Coke Studio lililandaliwa na Kampuni ya Coca-cola.

Msanii wa nyimbo za kizazi kipya Fid Q akiwa amemshikia kipaza sauti mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Makongo jijini Dar es Salaam, Veisi Kakobo wakatia alipokuwa akionyesha kipaji chake cha kuimba wakati wa Tamasha la Coke Studio lililofanyika shule hapo kwa ajili ya kutoa burudani na kuibua vipaji vya kuimba vya wanafunzi.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wakimlaki mwanamuziki wa nyimbo kizazi kipya Fid Q wakati alipowasili shuleni hapo kwa ajili ya kutoa burudani wakati wa Tamasha la Coke Studio lililoandaliwa na Kampuni ya Coca-cola.

Mwanamuziki wa  Bongo Fleva anayeshiriki  katika onyesho la Coke Studio msimu huu mwishoni mwa wiki alishiriki tamasha la Coke Studio liiloandaliwa na kampuni ya Coca Cola katika Sekondari ya Makongo mwishoni  mwa wiki ambapo aliwapatia  burudani murua na ushirikiana nao kucheza na kuimba ambapo baadhi ya wanafunzi walionyesha vipaji vyao vya kuimba kwa kushiriki kuimba nyimbo mbalimbali.(P.T)

Posted On Monday, 16 November 2015 04:19

Christian Bella na Ali Kiba

MUSA MATEJA

MKALI wa dansi mwenye asili ya Kongo, Christian Bella amefunguka kuwa anajivunia mafanikio makubwa waliyoyapata baada ya kufanikiwa kuingia studio na mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba kuzalisha wimbo mkali ambao umeleta ladha ya Dansi na Bongo Fleva, BongoDansi.

Mkali wa dansi mwenye asili ya Kongo, Christian Bella.

Akizungumza na gazeti hili, meneja wa Bella aliyejitambulisha kwa jina la Simple, alisema Bella na Kiba wamefanya ngoma hiyo kubwa kwenye Studio za Chedaz Record zilizopo Mikocheni jijini Dar chini ya prodyuza Abidady ukiwa ni utunzi wa Christian Bella.

Mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba

Alisema wimbo huo ambao una ladha kali kutoka kwa wasanii hao wakali wa Dansi na Bongo Fleva, tayari umeshakamilika na wameshaufanyia video ambayo wameifanyia jijini Nairobi Kenya kwa Director Enock. “Lengo ni kuleta kitu cha tofauti kwa mashabiki.

Wimbo unakwenda kwa jina la Nagha-limia, tayari umeshaingia kwenye vituo mbalimbali vya redio, utambulisho wa audio ataufanya Ali Kiba kwani Bella yuko kwao Kongo kwenye matatizo ya kifamilia. Anatarajia kurejea siku chache zijazo na akifika tu atafanya kazi ya kuachia video,” alisema Simple.(P.T)

Posted On Saturday, 14 November 2015 17:57

Posted On Monday, 09 November 2015 17:27
Page 4 of 54

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart