We have 82 guests and no members online

Displaying Ngoma Africa Band show dancers on action.JPG

Displaying Ngoma Africa band (1) (1).jpg

Displaying Great Ngoma Africa Band based in Germany.JPG

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni yenye makao nchini Ujerumani ,itatumbuiza mjini Bremen,Ujerumani

siku ya jumamosi 7 November 2015,katika ukumbi wa Weserterrasse, uliopo

mtaa wa Osterdeich 70b, D- 28205 Bremen kuanzia saa usiku, onyesho hilo limeandaliwa na Pan-African Org tawi la Bremen ambalo linasherekea miaka 10 ya kuanziswa kwake. bendi ya Ngoma Africa band kwa sasa wanatamba na CD yao mpya La Mgambo na pia song lao jipya waliloliachia juzi tu

"Mapenzi ya Pesa" nyimbo zote hizo zinapasua anga ya kimataifa

unaweza pia kusikiliza at www.ngoma-africa.com(P.T)

Posted On Wednesday, 04 November 2015 13:06

Diamond (wa tatu kutoka kushoto), akiwaongoza wenzake kwa kumuimbia wimbo wa birthday dada yake.

Queen Darleen akimshukuru kwa zawadi ya gari Diamond.

Queen Darleen akimlisha keki Diamond.

Meneja wa Diamond,  Babu Tale (kulia), akimmwagia maji Queen Darleen.

Msanii wa Bongo Fleva, Mwasiti Alimasi na wenzake awakimtaabisha Queen Darleen kwa kumpakaa keki.(P.T)

Posted On Wednesday, 04 November 2015 12:23

Unamkumbuka yule dogo aliyeanzisha redio stesheni yake nyumbani kwao? Bila shaka umewahi kusoma story yake kwenye kijarida cha kila mwezi kiitwacho SHUJAAZ ambacho husambazwa na gazeti la Mwanaspoti na vibanda vya Coca Cola. Sasa hivi, dogo ana habari mpya na njema kwa vijana na wote wanaomfuatilia. Nyota imeanza kung’ara upande wake na sasa redio kubwa Tanzania EAST AFRICA RADIO imeamua kumpa nafasi aweze kusikika hewani na show yake mpya iitwayo SHUJAAZ.

“Show yangu itahusika na lifestyle ya vijana kwa ujumla, bila kusahau burudani kali, story za wana mbali mbali wanaojituma na kutoboa katika kufikia malengo yao maishani. Pia, utawasikia vijana mbali mbali wakijadiliana kuhusu ishu zinazowahusu, mfano PESA, MAPENZI, KAZI, MICHEZO, UJASIRIAMALI n.k, ni lazima tupeane mashavu kama vijana.” Alisema DJ Tee.

Show hiyo itakayoanza rasmi JUMAMOSI hii (07/11/2015) saa TISA alasiri, inatarajiwa kuvuta hisia za vijana wengi hasa wajasiriamali kwa kuwa itahusika na ishu zote ambazo zinawahusu vijana kama DJ TEE mwenyewe alivyoelezea.

Unaweza kupata maelezo zaidi kutoka kwake mwenyewe kwa kujiunga naye kupitia Facebook jina ni DJ Tee (http://on.fb.me/1FUl1hX), Twitter (http://bit.ly/1LLGEpK) na Instagram (http://bit.ly/1Hn07t4)(P.T)

Posted On Wednesday, 04 November 2015 07:38

IMG-20151102-WA0031

Na Modewjiblog, team

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi katika tasnia ya muziki Bongo, Fredrick Kalala ama jina la usanii akijulikana zaidi, Fred Swagg ameachia wimbo mpya mtandaoni ‘NIMEWAKA’ au ‘Nimelewa’.

Akizungumza na Modewjiblog kwa njia ya simu kutoka jijini Mwanza, Fred Swagg mkali wa vibao vya Maandishi alichowashirikisha Younf Killer na Kad Go. Ameeleza kuwa katika wimbo wake huo mpya wa Nimewaka, upo katika mahadhi ya rap, ni maalum kwa watu wa rika zote hasa sehemu za starehe ikiwemo Club.

“Wimbo huu mpya wa Nimewaka ni wa ku-Party’ ndani yake kuna komediani ikielezea watu wanavyotumia pesa na kulewa pombe za aina mbalimbali.. hivyo fans wakae mkao wa kula kuanzia sasa itakuwa mtandaoni ikiwemo mkito.com “ ameleza Fred Swagg.

Fred Swagg anabainisha video ya wimbo huo zinatarajia kuanza muda wowote kuanzia mwezi ujao huku kwa sasa akiendelea na promo za nyimbo zake zingine zinazofanya vyema kwenye vituo vya radio mbalimbali za ndani na nje wimbo wa ‘Kikomo’ aliomshirikisha Msanii, Da Prince na wimbo wa Maandishi aliowashirikisha Young Killer na Kad-Go.

Posted On Tuesday, 03 November 2015 06:58

Posted On Monday, 02 November 2015 04:49

Muimbaji kutoka nchiniUganda Jose Chameleone akiimba kwenye stage ya bendi ya Skylight mara baada ya kupanda kwenye stage hiyo na kuwaacha mashabiki awa bendi hiyo wakitoa shangwe ya nguvu.

DSC_0048

Muimbaji wa nchini Uganda Jose Chameleone (katikati) akiimba kwa hisia moja ya nyimbo yake uku akisindikizwa na waimbaji wa bendi ya Skylight kushoto ni Suzy pamoja na Kasongo Junior (kulia).

Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani akisindikizwa na waimbaji wenzake katika kiota cha Escape One Mikocheni.

Waimbaji wa Bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani ya nguvu kwenye kiota cha Escape One.(P.T)

Posted On Monday, 02 November 2015 03:58

Phil Collins

Collins ni mmoja wa wanamuziki waliofanikiwa zaidi duniani

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Uingereza Phil Collins ametangaza kwamba atarejelea uimbaji na kusema hata anapanga ziara ya mataifa mbalimbali duniani.

Kwenye mahojiano na jarida la Rolling Stone, mwanamuziki huyo amesema: “Siko tena katika maisha ya kustaafu. Farasi achatoka nje sasa na yuko tayari kwa mbio.”

Msanii huyo wa umri wa miaka 64, aliyekuwa wakati mmoja kwenye bendi ya Genesis, alitangaza 2011 kwamba alikuwa ameachana na muziki ili kuweza kuwalea na kuwatunza wanawe wawili wa kiume.

Amesema kutokana na mpango uliopo wa kutoa upya nyimbo zake, haitakuwa busara kwake kutotoa nyimbo mpya

Collins hajatoa albamu yoyote ya nyimbo mpya tangu ile ya Testify aliyoitoa mwaka 2002 ingawa aliongoza kwenye chati za muziki mwaka 2010 kwa mkusanyiko wa nyimbo za Motown kwa jina Going Back.

Mwaka 2007, aliumia kwenye ziara ya pamoja ya wanabendi wa Genesis, na kumfanya asiweze kucheza ngoma tena.

Ameambia Rolling Stone kwamba atahamishia studio Miami, Florida na huenda akaanza kurekodi nyimbo mpya mwezi ujao.

Amesema angelipenda sana kutumbuiza katika kumbu Australia na Mashariki ya Mbali.

Collins ni mmoja wa wasanii waliofanikiwa sana, na ni miongoni mwa wanamuziki tatu, pamoja na Paul McCartney na Michael Jackson, waliouza zaidi ya albamu 100 milioni duniani wakiwa kivyao na pia kwenye bendi.

Nyimbo zake maarufu ni pamoja na A Groovy Kind of Love na Against All Odds.

Collins ameshinda tuzo saba za Grammy, sita za Brit, moja ya Oscar na mbili za Golden Globes.

Posted On Sunday, 01 November 2015 05:24

Staa anayesumbua kwa sasa na Kibao cha Shauri Zao, Abedinego Damian ‘Belle 9’.

Boniphace NgumijeNGUMIJE
STAA anayesumbua kwa sasa na Kibao cha Shauri Zao, Abedinego Damian ‘Belle 9’ amefunguka kuwa kufuatia wimbo wake huo kuanza kufanya vizuri kimataifa ikiwa ni pamoja na kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya televisheni ikiwemo Trace Urban kumemfanya apate mzuka wa kuandaa kazi nyingine kali ambayo anategemea itamfikisha kimataifa zaidi ya hapo alipo.

Akichonga na Centre Spread, Belle alisema hatua hiyo aliyopiga kwa sasa anadhani ndiyo ambayo mashabiki wake walikuwa wanaililia aifikie na kwa kuwaheshimu mchango wao atahakikisha ana washa moto ambao hauzimiki ili kufika mbali zaidi.

“Kila mara nilikuwa napenda kusema kuwa wakati wangu haujafika lakini sasa nathubutu kusema it’s my time to shine na moto ninaokwenda kuuwasha kwa kazi zinazofuata hakuna wa kuuzima,mashabiki zangu wategemee vitu vikubwa sana,” alimaliza Belle.GPL(P.T)

Posted On Friday, 30 October 2015 04:32

Adele

Adele amepanga kuzindua albamu mpya mwezi ujao

Wimbo mpya wa mwanamuziki Adele umeendelea kuvunja rekodi, siku chache baada ya kuzinduliwa.

Wimbo huo kwa jina Hello, ambao unarejesha Adele kwenye chati za muziki, uliza nakala 165,000 siku tatu za kwanza.

Mnamo Ijumaa, wimbo huo unatarajiwa kuongoza chati za vibao vya pekee vya muziki Uingereza.

Nyota huyo pia anatarajiwa kuvuma sana Marekani, wimbo huo ukitarajiwa kuwa nambari moja kwenye chati baada ya kupakuliwa mara 450,000 mtandaoni masaa 48 ya kwanza tangu kutolewa kwake.

Video ya wimbo huo, ambayo imeelekezwa na mtengenezaji filamu kutoka Canada Xavier Dolan, kadhalika imevunja rekodi iliyowekwa na Taylor Swift kwa kutazamwa mara nyingi zaidi kwenye mtandao wa Vevo siku yake ya kwanza.

Video ya Hello ilitazamwa mara 27,717,681 Ijumaa iliyopita, na kupita mara wimbo wa Bad Blood wake Swift ambao ulitazamwa mara 20.1 milioni siku ya kwanza baada ya kuzinduliwa mapema mwaka huu.

Video hiyo yake Adele kufikia sasa imetazamwa mara 107 milioni kwenye YouTube.

Mwanamuziki huyo anatarajiwa kuzindua albamu yake kwa jina ‘25’ mnamo Novemba 20.

Adele, ambaye jina lake kamili ni Adele Laurie Blue Adkins ameolewa na ana mtoto mmoja.BBC

Posted On Wednesday, 28 October 2015 16:45

dimaond

 Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na tuzo yake kutoka MTV EMA.

STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ jana ametwaa tuzo ya MTV EMA katika kipengele cha ‘Best Worldwide Act: Africa/India’ akimgalagaza Miss World 2000, Priyanka Chopra. Diamond alikuwa akichuana na muigizaji wa filamu na aliyekuwa Mrembo wa Dunia (Miss World 2000), Priyanka Chopra katika tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA) kwenye kipengele hicho. 

Priyanka-Chopra-2

Miss World 2000, Priyanka Chopra.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Diamond amewashukuru sana mashabiki wake, wasanii wenzake, uongozi wake pamoja na familia yake huku akisema kutokana na zoezi la uchaguzi mkuu hapatakuwepo na mapokezi makubwa ila itaandaliwa siku maalum kwa ajili ya kupiga picha na tuzo hiyo. Hivi ndivyo Diamond alivyoandika:

 diamond 

Tuzo hizo zilitolewa jana Oktoba 25, 2015 jijini Milan, Italia.(P.T)

Posted On Monday, 26 October 2015 06:42

Na Hamida Hassan-GPL

HALIMA Yahya ‘Davina’ amehamasika na mambo ya kisiasa hivyo, kujiandaa kwa kujifua vyema kwa ajili ya msimu ujao wa uchaguzi (2020).

Halima Yahya ‘Davina’ .

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Davina ambaye ni msanii wa filamu Bongo, alisema kufuatia kupata fursa ya kushiriki kampeni kwa nafasi yake, maeneo mbalimbali ya nchi, amejikuta akishawishika kuwa kiongozi na kwamba baada ya miaka mitano, endapo Mungu atamjaalia uzima, atagombea nafasi ya ubunge, mkoani Iringa.

“Sikuwa na mzuka na mambo ya siasa kabisa lakini kushiriki kwangu kampeni za kumnadi Magufuli maeneo mbalimbali nchini, nimeingiwa na ujasiri wa kujiingiza huko na naamini nitamudu nikijipanga, kikubwa tuombe uzima,” alisema Davina.(P.T)

Posted On Friday, 23 October 2015 08:49

Hakika ilikuwa ni Furasa isiyo na Kifani kwa Wanafunzi wa Awali kutoka Shule ya Msingi Green View English Medium ya Jijini Mwanza baada ya kufika katika mandhari iliyopo ndani ya Mamiz Grand Resort Mkolani Jijini Mwanza kwa ajili ya ziara yao ya Kimasomo (Study Tour) siku ya juzi Octoba 16,2015.

Na:George Binagi-GB Pazzo

Wanafunzi hao walifurahia michezo ya aina mbalimbali inayopatikana Mamiz Grand Resort kama ambavyo Kamera ya BMG (Binagi Media Group) ilivyonasa matukio ya hapa na pale. Hakika Watoto sasa wamepata pahala pa kufurahia utoto wao ndani ya Jiji la Mwanza.

Mmoja wa Wanafunzi wa Green View English medium akifurahia Michezo ya Chopa ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza 

Mmoja wa Wanafunzi wa Green View English Medium akifurahia Michezo ya Chopa ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza 

Mmoja wa Wanafunzi wa Green View English Medium akifurahia Michezo ya Chopa ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza (P.T)

Posted On Sunday, 18 October 2015 06:37
Page 5 of 54

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi