We have 151 guests and no members online

FAINALI za shindano hilo zinatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa Oktoba 9 Mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomon uliopo eneo la Namanga Kinondoni jijini Dar es Salaam. Siku hiyo pia kutakuwa na burudani za nguvu kutoka kwa msanii Run Town wa Nigeria ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Gallardo.

“Ukiachia mbali msanii huyo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa Christian Bella, Yamoto Bendi, Nevy Kenzo ambao watakamua sambamba na wasanii mahiri ambao ni zao la BSS kama Peter Msechu na Kala Jeremiah. Viingilio siku hiyo vitakuwa 25,000/=, ambapo nafasi za VIP zitakuwa 50,000/= na viti maalum vitalipiwa 100,000/=. Nawaomba mashabiki waje kwa wingi maana fainali ya mwaka huu ni ya kipekee kabisa,” alisema Madam Ritha.(P.T)

Posted On Thursday, 08 October 2015 08:36

Posted On Thursday, 08 October 2015 08:31

Posted On Monday, 05 October 2015 12:25

Mwenyekiti wa Tamasha la Kuombea Amani, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 4 kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Hamisi Pembe. (Picha na Francis Dande)

Na Mwandishi Wetu

WAIMBAJI watakaoshiriki katika tamasha la kuombea Amani Uchaguzi Mkuu 2015 wanaanza kuwasili Ijumaa Oktoba 3.

Aklizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 100 huku waimbaji kutoka nje ya nchi wanatarajiwa kuwasili kuanza Ijumaa.

Aliwataja waimbaji hao kuwa ni Sipho Makhabane, Solly Mahalangu (Afrika Kusini), Ephraim Sekereti (Zambia), Solomon Mukubwa (DR Congo), Sarah K (Kenya).

Aidha kutakuwa na waimbaji wadhawa akiwemo malkia wa muziki wa injili Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca BM, Bonny Mwaitege, Christopher Mwangira, John Lissu.

Kwa upande wa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, Kweaya ya AIC Chang'ombe na Kwaya ya St. Adrew Aglikana ya Dodoma.

Wakati huohuo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limeipongeza Kampuni ya Msama Promotions kwa kuwa wabunifu wa kuinua vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili Tanzania ambao wanapata nafasi ya kutambulika kimataifa.

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, alisema kuwa ufanikishaji huo wa kazi za waimbaji inayofanywa na Msama ni baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo ufuatiliaji wa vibali vya kufanikisha tukio hilo la kuombea amani Oktoba 4.

Mngereza alisema tamasha hilo ni lenye maana kubwa kutokana na maudhui yake, hasa ikizingatiwa nchi inakabiliwa na Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 25.

Alisema tamasha hilo linasisitiza kuwa amani ni kitu cha msingi hasa kwa masuala ya kisiasa na kiuchumi, ambavyo havitapata mwelekeo wake iwapo amani hiyo ikikosekana.

“Kama hakuna amani vitu vyote havifanyiki, tamasha hilo limekuja wakati muafaka kwamba sisi ni wamoja, Watanzania tuzingatie misingi ya amani.

“Tumekuwa ndugu bila kubaguana kwa hali yoyote, amani tuliyopewa na Mungu, tuileee na kuitunza tunu hiyo kwa sababu ndiyo chachu ya maendeleo yetu na taifa kwa ujumla,” alisema.

Mkurugenzi wa Msama Prmotions, Alex Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yamekamilika kwa kiasi kikubwa, hivyo alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.

“Nawasihi wapenzi na mashabiki wa muziki wa Injili na wengine wenye mapenzi mema kwa nchi yao, wajitokeze kwa wingi katika Uwanja wa Taifa katika tamasha la kuombea amani Uchaguzi Mkuu,” alisema Msama.

Aidha, ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kukubali kubeba jahazi la tamasha hilo, kwa kukubali kuwa mgeni rasmi ambapo atatumia tukio hilo kuwaaga mashabiki wa muziki wa Injili.(P.T)

Posted On Friday, 02 October 2015 05:24

Zetrida Ezekiel ni mwanamuziki mahiri wa muziki wa injili aishiye mkoani Kigoma, amekuwa mwanamuziki wa nyimbo za injili ambaye ni mwana kwaya wa  kikundi maarufu na kikongwe cha nyimbo za injili cha MKE MWEMA cha mjni Kigoma. Zetrida ameolewa na ni mama wa watoto wanne, wa kike wawili na wa kiume wawili.

Lakini baada ya kupata rai nyingi na kwa muda mrefu toka kwa wachungaji wake na watu mbali mbali kuwa atengeneze albamu yake kama mwanamuziki wa kujitegemea,hatimae mwezi wa August mwaka huu Zetrida alikuja Dar es Salaam na kuanza kazi ya kutengeneza albam yake binafsi.

Zetrida Ezekiel akiwa katika pozi.

Album yake inayoitwa Ringa na Yesu ina nyimbo nane na nyimbo zote amezifanyia Tika records chini ya mtayarisha muziki maarufu nchini aitwaye Ephraim Kameta ambapo nyimbo sita katika albam yake hiyo zilitengenezwa na Kameta na mbili zikitengenezwa mtayarisha muziki machachari PG zote katika studio za Tika records pia. Katika albam hiyo kuna nyimbo kama Ringa na yesu liyobeba jina la albam Malaika, waombee maadui zako na nyingine nyingi zenye kiwango cha hali ya juu.(P.T)

Posted On Thursday, 01 October 2015 07:21

Joh-makini

Staa wa Hip Hop Bongo anayewakilisha Kundi la Weusi, John Simon ‘Joh Makini’

wpid-davido-his-hkn-crew-fly-private-jet-to-kenya-in-style-31

Staa wa muziki kutoka Nigeria, David Adeleke ‘Davido’

STAA wa Hip Hop Bongo anayewakilisha Kundi la Weusi, John Simon ‘Joh Makini’ ametoboa siri ya kolabo yake na staa wa muziki kutoka Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ kuwa Davido ndiye alikuwa na shauku ya kufanya naye kolabo na kumtafuta kwenye mitandao ya kijamii.

Akichonga na Showbiz, Joh Makini alisema, kupitia ukurasa wake wa Instagram, alitumiwa ujumbe mfupi na Davido na kuelezwa kuwa amekuwa shabiki wake mkubwa na angependa wafanye naye kazi.

“Kiukweli nilishangaa sana maana sijawahi kukutana mahali popote na Davido, so lilikuwa jambo la kushtukiza kwangu lakini nikagundua siri ambayo wasanii wengi hawaijui ni kwamba muziki ni lugha inayoweza kuwaunganisha wasanii kutoka kona yoyote ile duniani,” alisema Joh.(P.T)

Posted On Wednesday, 30 September 2015 04:45

Msanii mkongwe wa muziki wa reggae na Mkurugenzi wa Reggae Production House Innocent Nganyagwa akiongea na wadau wa muziki huo mapema wiki hii kwenye programu maalum ya kujadili hatma ya muziki wa reggae iliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kufanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Sanaa kutoka BASATA, Augustino Makame na Katibu wa chama cha waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli .

Katibu wa chama cha waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wa muziki wa reggae (hawako pichani) kwenye programu maalum ya kujadili hatma ya muziki huo. Kushoto kwake ni Msanii mkongwe wa Reggae Innocent Nganyagwa 

Ras Bumijah Zinyongwa ambaye pia ni kiongozi wa Tanzania Rastafarai Movement (TARAMO) akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyoibuka kwenye programu hiyo.

Msanii mkongwe wa muziki wa Band John Kitime akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) kuhusu umuhimu wa Wasanii kujiunga na Shirika la Bima la Taifa (NHIF) ili kujihakikishia matibabu na kuepuka kuombaomba wakati wanapougua. (P.T)

Posted On Wednesday, 30 September 2015 04:43

Mwanamuziki maarufu wa Nigeria, David Adeleke.

MWANAMUZIKI maarufu kijana wa Nigeria, David Adeleke ajulikanaye zaidi kama Davido, amesema hana haraka ya kuoa hivi sasa ambapo nadhari yake ameielekeza kwenye tasnia ya muziki ambayo ndiyo inampa riziki yake na kwamba hataki kujifungia katika ‘sanduku’ na ndoa.

Davido aliyesema hayo hivi karibuni katika mahojiano na gazeti la Punch ambapo aliweka wazi kwamba bado hajaamua kumuoa mama wa mtoto wake, licha ya upendo wake mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha kwa mtoto wake.

Msanii huyo aliyeimba wimbo maarufu wa 'Skelewu' alisema: “Ni jambo jema sana kuitwa baba, lakini sifikirii kuoa sasa kwani kipaumbele changu hivi sasa ni muziki. "Hivyo, wapenzi wa mwanamuziki huyo watabidi wasubiri na kuona ni lini atafunga ‘pingu za maisha’.GPL(P.T)

Posted On Tuesday, 29 September 2015 04:03

Posted On Sunday, 27 September 2015 04:45

uzo aduba emmy awards 2015 speech

Muigizaji ambaye ni mzaliwa kutoka Nollywood, mkazi wa Hollywood, Uzo Aduba akionesha tuzo aliyoshinda.

uzzo

MUIGIZAJI mwenye vituko ambaye ni mzaliwa kutoka Nollywood na mkazi wa Hollywood, Uzo Aduba ameshinda kwa mara ya pili Tuzo za Emmy.

Staa huyo alishinda tuzo hiyo kupitia mchezo wa kuigiza ujulikanao kama Orange is the New Black katika kipingele cha Best Supporting Actress. Sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilifanyika hivi karibuni, Los Angeles, Marekani. Mwaka jana pia staa huyo alichukuwa tuzo hizo za Emmy.(P.T)

Posted On Saturday, 26 September 2015 18:56
Page 6 of 54

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu