We have 155 guests and no members online

 

Posted On Thursday, 24 September 2015 04:29

KUNDI  la Double M chini ya Muumin Mwinyjuma, limealikwa Msumbiji kwa mwezi mzima, na katika wakati huo kundi litashiriki katika sherehe za miaka 51 ya Vita vya Ukombozi wa nchi hiyo. Wanamuziki hawa ambao ni wanachama wa Mtandao wa Wanamuziki walipitisha barua yao ya taarifa ya kwenda huko na hivyo Mtandao ukatoa taarifa Baraza la sanaa La Taifa kama inavyostahili. Waliomo katika msafara huo ni pamoja na kiongozi wa kundi Muumin Mwinyjuma,  maarufu kwa jina la KOCHA, na wanamuziki wengine 16.

Mwinjuma Muumin Buguza- Kiongozi wa Bendi-Muimbaji, Omary Kisila- Kinanda,  Hamza S Waninga- Drums, Imma Keffa –Bass Guitar, Emmanuel Namwinga- Rhythm guitar, Amina R Juma –Muimbaji, Veronica D Buzeri –Dansa, Neema Kawambwa-Dansa, Stamili  Hamis –Dansa, Greyson Semsekwa – Rapper, Sharey Aboubakar-Muimbaji, Revina Mzinja -Dansa, Salma Shaaban –Dansa, Afande Muhamada-Fundi Mitambo, Omary Maulid –Fundi Mitambo, Saleh Kupaza-Muimbaji, Dogo Rama-Muimbaji.(P.T)

Posted On Tuesday, 22 September 2015 05:04

Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni jana.

 

Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni jana.

 

Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Usagara Tanga Mjini jana. Idadi kubwa ya wananchi walihudhuria mkutano huo hadi wengine kuzimia kutokana na msongamano.

Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni jana.

Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Kitaifa, Bi. Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi kwenye moja ya mikutano ya kampeni za CCM timu ya mgombea mweza iliyofanyika mkoani Tanga jana.(P.T)

Posted On Tuesday, 22 September 2015 04:20

Mwenyekiti wa tamasha la kuliombea Taifa Aman pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Alex Msama akifafanua jambo wakatio wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 19 kuhusu maandalizi ya tamasha hilo. Kulia ni Mratibu wa tamasha hilo, Hudson Kamoga. (Picha na Francis Dande)

Mratibu wa Tamasha la kuombea amani nchin na uchaguzi mkuu, Hudson Kamoga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo, litakalofanyika Oktoba 4 Uwanja wa Taifa jijini. Kushoto ni Mkurugenzi Msama Promotions, Alex Msama. (P.T)

Posted On Sunday, 20 September 2015 06:24

Belle 9 ameachia rasmi video yake mpya ya wimbo uitwao ‘Shauri Zao, ambayo amekuwa aki tease kwa zaidi ya wiki moja. Baadhi ya mashabiki wametoa maoni yao kuwa huenda hii ikawa ndio video kali zaidi ya Belle 9 kwa kulinganisha na zile zilizotangulia. Imeongozwa na Hanscana.

Posted On Saturday, 19 September 2015 04:59

 Ofisa Habari, Lydia Moyo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Redio EFM, Denis Ssebo  kuzungumza na wanahabari.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Redio EFM, Denis Ssebo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu shindano lililoanzishwa na redio hiyo la Kanga kupitia kipindi cha Uhondo kwa ajili ya wanawake wote wasikilizaji wa redio hiyo ambalo limeanza rasmi jana. Kulia ni Mtangazaji wa kipindi hicho, Dina Marios na Ofisa Habari, Lydia Moyo.

 Mtangazaji wa kipindi cha Uhondo, Dina Marios (kulia), akizungumzia shindano hilo.

Wapiga picha kazini katika mkutano huo 'Kazi yote  hiyo wanatafuta shibe chezea njaa wewe' 
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)(P.T)
Posted On Monday, 14 September 2015 14:42

????????????????????????????????????

Wasanii wenye vipaji vya kuimba wakihakiki majina yao kwa DJ Haazu, wa Radio 5 wakati wa mchakato wa RADIO 5 KAMATA KIPAJI uliofanyika katika viwanja vya TP SINZA Jijini Dar es salaam Septemba 12, 2015.wenye lengo la kusaka vijana wenye vipaji na kuwainua kutokana na vipaji vyao.(PICHA ZOTE NA PHILEMON ).

Katika kuonyesha kuwa wapo karibu na vijana wa Kitanzania katika kuwasaidia kuwainua kiuchumi na kiuwezo,kituo cha Radio maarufu kutoka kaskazini mwa Tanzania ARUSHA Radio 5 kimenzisha mchakato maalum wa kusaka vipaji kwa vijana wa kitanzania mchakato ambao umeanzia Jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanamuwezesha kijana mwenye kipaji kufikia malengo na ndoto zake.

3

DJ Haazu akiwajibika.

Radio 5 imekuwa na michakato mbalimbali ili kusaidia vijana katika secta tofauti tofauti zinazohusu maisha yao ya kiuchumi huku ikiwa inawaunga mkono vijana wenye shughuli mbalimbali ambao hufika radioni hapo kuomba sapoti ikiwa ni pamoja na vijana wa sarakasi, ujasiriamali na fani nyingine.

Mchakato ambao sasa unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao umezinduliwa Jijini Dar es salaam na kupewa jina la ‘RADIO 5 KAMATA KIPAJI’ katika viwanja vya TP Sinza darajani ilishuhudiwa vijana wengi wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuibuka na zawadi mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.

2

Wafanyakazi wa RADIO 5 wakishangilia wakati Wasanii mbalimbali ambao ni vijana wenye vipaji wakati wakionesha vipaji vyao jukwaaji (kulia), Mtangazaji wa Redio 5 Mwangaza Jumanne (katikati), Meneja masoko na mawasiliano Sarah Keiya na kushoto ni Meneja Vipindi, Mathew Philip.

Posted On Monday, 14 September 2015 06:32

1.

3.

Yamoto Band wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala, Zakhem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

 Wasanii wa Yamoto Band, Enock Bella (wa kwanza kushoto) akifanya yake na Aslay (kulia).(P.T)

Posted On Sunday, 13 September 2015 05:08

11375313_1660537620828116_1538688231_n

Baada ya Shikirobo tarajia ngoma zingine kali kutoka kwa Shetta. Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa ameandaa nyimbo saba mpya ambapo atachagua moja ya kutoka. Amesema muziki wa sasa unahitaji nyimbo nzuri na sio kubahatisha.

“Watu wategemee ngoma kali, sitaki kuongea sana, video kali. Kuna ngoma kama saba nimeziandaa,” amesema Shetta.

“Yeyote itatoka kwasababu muziki umekuwa unahitaji kazi nzuri ili iweze kufanya vizuri. Kwahiyo naweza nikatoa collabo pia, chochote kinaweza kutokea.”

Posted On Saturday, 12 September 2015 07:50
Page 7 of 54

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu