We have 183 guests and no members online

BONNY MWAITEGE:TAMASHA LA PASAKA TULIPE UZITO WAKE

Posted On Thursday, 28 January 2016 21:24 Written by
Rate this item
(0 votes)

MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injil, Bonny Mwaitege ametoa wito kwa Watanzania kuilipa uzito wa aina yake Tamasha la Pasaka kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria tukio hilo adhimu duniani.Mwaitege alisema Tamasha la Pasaka lina ujumbe wa Mungu hivyo Watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi na kumkimbilia Mungu katika tamasha hilo
.“Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka, hivyo kuna kuna ujumbe mkubwa kutoka kwa Mungu ambao utawaokoa Watanzania wote,” alisema Mwaitege.Mwaitege alisema kupitia tamasha hilo jamii inaondokana na machafu ambayo yanamchukiza Mungu.Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema tamasha la mwaka huu wamejipanga vilivyo kufanikisha matakwa ya jamii kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili na viongozi wa dini watakaohudhuria tamasha hilo.
Msama alisema tamasha la mwaka huu wamepanga litaanza Machi 26 hadi 28 hapa nchini, hivyo Watanzania wajiandae na tamasha hilo.“Watanzania watarajie tamasha bora ambalo litafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii, hivyo wajiandae,” alisema Msama.(VICTOR)

Read 1052 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart