We have 185 guests and no members online

Ajali ya pikipiki imesababisha Diamond hasara ya zaidi ya shilingi milioni 9

Posted On Saturday, 12 March 2016 11:58 Written by
Rate this item
(0 votes)

Diamond alilazimika kutoa $4,500 za ziada (ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 9 za Tanzania) kugharamia hasara iliyopatikana baada ya Harmonize kupata ajali akiwa model kwenye utengenezaji wa video ya wimbo Bado.

Harmonize ametoa taarifa hiyo wakati akiongea Jumamosi hii kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM. Amedai kuwa wakati wanataka kufanya scene hiyo ya pikipiki, muongozaji alitaka wavutwe na kamba na gari maalum ili kuonesha kama akiendesha kweli, lakini Harmonize alidai kuwa wabongo wangeshtukia hivyo ni bora angeendesha kweli kwakuwa anafahamu.

“Wakati tunashoot, tunapaki, yule demu wakati nampakiza kwenye pikipiki haamini kabisa kama naweza kuendesha na yeye pia, yule video queen, kwahiyo akawa ameng’ang’ania kwamba tukianguka tuanguke wote,” amesema muimbaji huyo.

“Sasa wakati tunapaki akataka kuruka, halafu bahati mbaya akaruka kulia, yaani unajua ile nimesimama, yeye anataka ashukie kulia. Alivyoshukia kulia akadondoka, halafu ile pikipiki ikanizidi uzito, ikaenda hadi chini hivi kwasababu ni BMW ni kubwa sana,” ameongeza.

“Kwahiyo ilivyofika chini ikavunjika indicator halafu katika exhaust ikakwanguka hivi. Sasa zile tu exhaust kukwanguka vile na indicator ikatugharimu kama dola 4,500 hivi yaani kama milioni 9 hivi za Kitanzania. Halafu pia demu akaleta mashauzi siku kama tatu hivi anajiuguza tukawa tunambembeleza tukalipia tena apartment kama siku tatu mbele ikatucost. Lakini mwisho wa siku tukamaliza salama tukarudi hapa nyumbani.”

Read 2921 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart