We have 439 guests and no members online

Picha ya Fred Matuja

Kwa muda nilikuwa kimya kutokana na kubanwa na majukumu ya “Kaisari” hata hivyo muda wote huu nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu kujua nini kiko katika akili za baadhi ya Watanzania. Ni kwa namna Watanzania wengin wanafikiria changamoto zinapotokea.

Katika muktadha wa leo, nitajikita kwa viongozi wa kisiasa na waandishi wa habari kama watu wenye nafasi ya kuwasilisha kile kinachozungumzwa katika majukwaa ya kisiasa na kukileta kwa wananchi kupitia magazeti, radio, television, mitandao za kijamii na vyanzo vingine vyovyote vile kwa lengo la kuhabarisha.

Katika majuma kadhaa kumekuwa na mijadala wa “uwepo wa njaa” Mjadala huu umechagizwa kutokana na sababu ya kupanda kwa bei ya nafaka hususani mahindi. Unga wa sembe na dona kupanda bei kumekuwa gumzo. Isipokuwa mchele hakua kwenye mjadala licha ya bei yake kuwa chini kwa nyakati hizi ukilinganisha na bei ya mchele kwa miaka miwili iliyopita.

Pamoja na wingi wa mijadala na hotuba majukwaani hata kwa wale wanaolaumu au kulalamika kuna njaa, ni wachache sana waliokwenda mbele kwa kufungua akili zao kuona suluhisho na kulileta katika mjadala ili Watanzania waweze kupata fikra mbadala ambayo inaweza kuleta mwitiko mbadala kwa kuchukua hatua tofauti ya namna ya kufanya kilimo chetu.

Tukijikumbusha hadithi ya kweli ya Viktor Frankl mtu aliekuwa katikati ya mateso chini ya udikteta wa Hitler, yeye alianza kuifundisha akili yake kuona maisha baada ya kifungo. Pamoja na kufiwa na watu wake wa karibu kwa sababu ya mateso waliyopata akiwemo baba, mama, na mke, bado Frankl hakukata tamaa ya kuona kifo chake kimefika. Hakutaka kuwa na fikra ya kuishi chini ya ushawishi wa hali ngumu ya mateso. Bali alijenga fikra mbadala ambayo baadae ilimpa matokeo kwa kiwango cha namna alifikiria.

Nilitegemea na ninategemea kuona kila kiongozi wa kisiasa au mwanahabari kutokulaumu au kulalamikia hali ya kupanda bei chakula, hali ya kutokuwa na uhakika wa mvua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, bali kutuletea maandiko na habari zenye fikra mbadala za kuwasaidia Watanzania kujipanga upya na kufanya maamuzi ya kuendelea kufanya kilimo bila kutegemea mvua. Kilimo bado tunakitegemea sana ili kupata chakula, mali ghafi za mazao ya kilimo kama alizeti, pamba, ufuta hali kadhalika wafugaji wanatakiwa kupata elimu mbadala ya namna bora za kuwa na malisho mbadala ya wanyama pasi kutegemea kuhama toka upande mmoja wa Tanzania kwenda kwingine kutafuta malisho.

Kulalamikia uongozi kwa kuwa mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira si rafiki ni mfumo wa kutokuwajibika kama kiongozi. Wajibu wa kwanza kwa kiongozi yeyote ni kuja na njia mbadala na kuihamasisha jamii kupitia elimu kupitia vyanzo mbalimbali vya habari ili Watanzania tujione tuna akili za kuidhibiti “dunia” yetu kwa kijihakikishia uhakika wa chakula.

Kuna jukumu kubwa la kuja na elimu mbadala, ambao itabadili namna ya kufikiri kwa Watanzania. Waziri wa habari yeye kama mdau mwenye dhamana ya kusimamia Wizara ya habari na utamaduni, ana jukumu la kukaa na wadau ili kusaidia jamii ipate habari zenye kufundisha akili zetu Watanzania namna mpya ya kufikiri na kutenda pale changamoto zinapotokea katika jamii zetu.

Mwanamke wa kwanza kuanzisha jina la cheo cha mke wa Rais (First Lady) Eleanor Roosevelt aliwahi kusema, hakuna mtu au kitu kinaweza kukuumiza bila kukiruhusu.

Watanzania tunajukumu la kubadili namna ya kupata habari pamoja na uhuru huu wa habari. Kuna habari zingine ziko sawa kuzifahamu, ila kama hazitupi suluhisho la namna gani ya kutoka hapo na kuiacha jamii kwenye “suspense” hizo habari zaweza kuwa sumu.

Tegemeo letu ni kuwa kwenye karne ya 21 ambapo inajulikana wenzetu duniani wanafanya nini kukabili matatizo kama ya hapa kwetu, basi wanahabari ambao wanabeba jukumu la uongozi wa kuhabarisha kusimama kutuoesha uongozi, vinginevyo wataweka habari ambazo si kila msomaji amekomaa kuweza kuzisoma na kujua nini afanye kutoka hapo alipo.

Naomba kunukuu moja ya kauli ya Rais aliemaliza muda wake wa uongozi nchini Marekani alipohutubia kwa mara ya mwisho kama rais pale Chicago. Iliwaomba Wamerekani waamini. Si kumwamini uwezo wake yeye kuleta mabadiliko ila wajiamini wao.

Tukiamua kwa pamoja na kwa nia moja kutafuta mabadilko katika namna ya kufanya kilimo chetu kwa kutumia teknolojia ya umwagilaji kwa lengo jema la kazalisha kwa wingi ili kupata ziada. Nina imani hakuna mtu mwenye nia ya kutatua tatizo la chakula akija na mpango-mkakati wa kulima kwa kumwagilia bila kuathiri mazingira ili kupata chakula cha kulisha ndani na ziada kuuza nje ya nchi atapingwa. Tunawajibika kuijenga Tanzania mpya kwa mfumo huu.

Watanzania tuna jukumu la kukumbuka kuwa, tabia ya kulalamika ikiendelea mara kwa mara itazaa mwenendo wa kulalamika tu na kulaumu. Watu wengi wakiwa na mwenendo wa kulalamika na kulaumu tutakiua kizazi cha kesho.

Natamani kila mtu anaendika habari ajione ana jukumu la kuonesha kiwango cha uzalendo kwa hali ya juu. Pale mwanahabari au mwanasiasa anapotoa taarifa ya tatatizo anajione pia anawajibika kutuonesha suluhisho la tatizo ambalo kalionesha kwa kuliandika, kupiga picha au kuliweka katika makundi mbalimbali kama mjadala kwenye mitandao ya kijamii.

Wimbo wa taifa letu una ujumbe wa kuomba Mungu adumishe uhuru na umoja wetu. Pengine kuna jukumu la kutafakari kwa kina, kama kila tunachokifanya kinadumisha uhuru wetu na umoja au inakuwa kinyume chake.

Mungu ibariki Tanzania. Tuna jukumu la pamoja kuijenga nchi yetu.

Fredrick Matuja
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.(P.T)

MJO

 Rais Dkt. John Pombe Joseph magufuli akisalimiana na Mwakilishi kutoka Uturuki  Bw, Ziya Karahan wakati wa chakula cha jioni alichomwandalia Rais huyo jana jijin Dar es Salaam. Mwenye tai nyekundu ni Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

MJO 1

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akipeana mkono na Mke wa Rais Dkt. Magufuli Mama Janeth Magufuli jana jijini Dar es Salaam.

MJO 2

 Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Rais Dkt. John Pombe Joseph magufuli na Mama Janeth Magufuli wakigonga cheers wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa mahususi kwa ajili ya Rais huyo wa Uturuki jana jijin Dar es Salaam.

MJO 3

Baadhi ya wageni waalikwa katika dhifa ya chakula cha jioni  kwa ajili ya kumuaga Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan jana jijini Dar es Salaam.

MJO 5

Rais Dkt. John Pombe Joseph magufuli akipiga ngoma baada ya kufurahishwa na burudani kutoka kwa Bendi ya Mrisho Mpoto na Banabana wakati wa chakula cha jioni alichomwandalia Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan jana jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija – MAELEZO.(P.T)

Ttcl 1

Baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Simu  Tanzania TTCL katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule za Sekondari ya Tabora Wavulana na Wasichana nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tabora baada ya hafla fupi ya  TTCL kukabidhi msaada wa vifaa vya Maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari za mkoa wa Tabora.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry akipokea msaada wa vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kutoka kwa Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi,vifaa hivyo vinathamani ya shilingi milioni saba.

Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akisoma taarifa fupi ya kukabidhi msaada huo wa vifaa vya maabara vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni saba.

Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akikabidhi taarifa aliyoisoma wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Tabora Wasichana wakiwa wamebeba masanduku ya vifaa vya maabara vilivyotolewa msaada na Kampuni ya Simu Tanzania TTCL

Baadhi ya maafisa wa TTCL wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya maabara ya sayansi vilivyokabidhiwa na Kampuni hiyo ya simu Tanzania.(P.T)

Rais wa Marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amefanya kile alichokiita siku yake ya kwanza kuanza kazi katika utawala wake, kutokana na uamuzi alioufanya wa nchi yake kujiondoa katika mpango wa Ushirikiano wa kiuchumi wa nchi zinazounganishwa na bahari ya Pasifiki.

Ameonya pia kuyapa adhabu makampuni ya nchi hiyo yanayopeleka kazi nje ya nchi.

Makubaliano ya Mpango wa Ushirikianio wa Kibiashara wa nchi zinazounganishwa na Bahari ya Pacific TPP, yalijadiliwa na utawala wa Rais Barack Obama.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer anasema hatua hiyo ni dalili ya kuanza kwa enzi mpya ya sera za biashara za Marekani.

''...Kama alivyokuwa akisema Rais mara nyingi, hii ni aina ya makubaliano ya mataifa mengi na si kwa maslahi mazuri kwetu, na amekua akienda haraka kuboresha sera za kibiashara ambazo zitaongeza ushindani wa wafanyakazi wa Marekani na uzalishaji...'' Alisema Sean Spicer

Amesema amri hiyo ya Rais inaongoza katika enzi mpya ya sera za biashara ya Marekani, ambayo utawala wa Trump utapata fursa ya kufanya biashara na washirika wake duniani kote.

Lakini si hatua hiyo tu aliyoichukua Rais Trump, katika wiki yake ya kwanza ofisini, Rais Trump pia amerejesha amri ya kupiga marufuku utoaji wa fedha za serikali kwa makundi ya kimataifa ambayo yanazitumia katika kushughulikia ama kujadili utoaji mimba kama njia moja wapo ya uzazi wa mpango.

Uamuzi huo ni taarifa ya kwanza ya utawala mpya wa Marekani kutoa kuhusiana na misaada inayotoa kimataifa.

Utawala unaongozwa na chama cha Republican nchini Marekani mara zote umekuwa ukipiga marufuku msaada wa serikali kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa ambayo yanatoa huduma za utoaji mimba.

Wakati huohuo Baraza la Senete nchini Marekani limemthibitisha Mike Pompeo kuwa mkurugenzi mpya wa Shirika la Ujasusi nchini humo CIA.

Waandishi wa habari wanasema kazi yake ya kwanza itakuwa kurejesha uhusiano mzuri katui ya shirika hilo na Rais Donald Trump, ambaye amekuwa akilikosoa kwa kile ilichosema kwamba Urusi ilimsaidia wakati wa uchaguzi.BBC

media

Nkosazana Dlamini Zuma, Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Viongozi wa mataifa ya Afrika, watakutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia mwishoni mwa wiki hii kujadili maswala mbalimbali yanayoligusa bara la Afrika hususan kuhusu usalama na uchumi.

Hata hivyo, viongozi hao watakuwa na kazi kubwa ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja huo kuchukua nafasi ya Nkosazana Dlamini-Zuma kutoka Afrika Kusini.

Wagombea watano wanawania wadhifa huu akiwemo Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohammed.

Amina Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, aliyependekezwa na Rais Uhuru Kenyatta, kuwania kiti cha uenyekiti wa AU.

Serikali ya Kenya inasema ina imani kubwa kuwa mgombea wake atashinda, kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Fred Matiang'i ambaye amekuwa akiongoza Kamati Maluum ya kumpigia debe Waziri Amina.

Itafahamika kwamba Afrika Mashariki itawakilishwa na Fowsiyo Yusuf Haji Adan, waziri wa zamani wa kigeni nchini Somalia, na Waziri wa sasa wa mambo ya Nje wa Kenya Amina Mohammed, ambaye anapigiwa debe na Rais wake, Uhuru Kenyatta, na kuungwa mkono na rais wa Uganda Yoweri Museveni. Moussa Faki Mahamat, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, ambaye alitangaza kuwania katika kinyang'anyiro hicho katika dakika ya mwisho, ni miongoni mwa wagombea hao.RFI

WODO

Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akimueleza jambo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli Ikulu Leo Jijini Dar es Salaam.

WODO 1

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan Ofisini Kwake Leo Jijini Dar es Salaam.

WODO 2

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan wakifurahi na kinamama waliowalaki wakati anawasilini ofisini kwa Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.

WODO 3

 Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan baada ya kusaini kitabu cha wageni Ofisini Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli.

WODO 4

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan.

WODO 6

Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akiongea na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ambapo amemuahidi kuendelea kushirikiana katika kuwasaidia watoto na wanawake.(P.T)

Read more...

FULL

 Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe wakipokea mashada ya maua kutoka kwa watoto walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 kwa mapokezi rasmi na mazungumzo na mwenyeji wao Rais Dkt John Pombe Magufuli.

FULL 1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwalaki Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 kwa mazungumzo

FULL 2

FULL 3

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan wakipiga ngoma Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017

FULL 4

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwazawadia Kinyago cha Umoja na Mchoro wa Mlima Kilimanjaro Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 

FULL 5

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mama  Emine Erdogan wakipeana mikono baada ya maongezi  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 

FULL 7

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na akiongea katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam  leo Januari  23, 2017.(P.T)

Read more...

1

Msafara wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan ukiwasili katika viwanja vya Ikulu leo wakati alipopokelewa na mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli leo katika Ikulu ya Magogoni  jijini Dar es salaam , Rais huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.PICHA NA (JOHN BUKUKU FULLSHANGWE-IKULU DAR ES SALAAM)

022

Msafara wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerari Davis Mwamunyange  katika viwanja vya Ikulu leo wakati alipopokelewa na mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli leo.

3

Msafara wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan aki mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli leo wakati alipopokelewa kwenye viwanja vya ikulu jijini Dar es salaam.

4

Msafara wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan  na mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli leo wakipokea heshima kwa kupigiwa nyimbo za mataifa haya mawili na mizinga,

5

Msafara wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan akikagua gwaride  katika viwanja vya Ikulu leo wakati alipopokelewa na mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli leo.

1213

Msafara wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan aki na mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano leomara baada ya kuwasili Ikulu..

14

Msafara wa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan akipiga mgoma  katika viwanja vya Ikulu leo wakati alipopokelewa na mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli.

7

Wakuu wa vikosi vya iulinzi na usalama wakisubiri kupokelewa kwa Rais wa Uturuki Mh. Recept Tyyip Erdogan

8

Rais Dk. John Pombe Magufuli leo akizungumza na wakuu wa vyomboo vya ulinzi na usalama wakati akisubiri kuwasili kwa rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan.

9

Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa wakati wa mapokezi hayo.

10

Baadhi ya mawaziri na watendaji wa serikali ya Uturuki wakiwa wamekaa katika viwanja vya Ikulu

11 

Waziri wa Sheria na Katiba Dk. Harrison Mwakyembe kulia akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mapokezi ya Rais wa Uturuki Mh. Recept Tayyip Erdogan.

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uturuki zimesaini mikataba tisa ya makubaliano ya kiuchumi inayolenga katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa maendeleo baina ya nchi hizo.

Mikataba hiyo inahusisha sekta za uchukuzi, mawasiliano, habari, elimu, utalii, utafiti, viwanda, afya na ulinzi.

Akizungumza mara baada ya kusaini kwa mikataba hiyo  leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alisema ujio wa Rais wa Uturuki na ujumbe wake ni kielelezo cha ukuaji wa mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki katika nyanja ya biashara na kimaendeleo baina nchini hizo.

Rais Magufuli alisema katika mazungumzo yake aliyofanya na Rais Recep Erdogan kuhusu ujenzi wa Reli ya Standard Gauge nchini, alimjulisha kiongozi huyo kuwa miongoni mwa wakandarasi walioomba zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kuwa ni kampuni kutoka Uturuki, hivyo endapo itashinda zabuni hiyo itasaidia kukuza uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa, Serikali ya Tanzania inatarajia kuomba  mkopo kupitia Benki ya Exim ya Uturuki katika kujenga sehemu ya kipande cha ujenzi wa reli hiyo.

Rais magufuli alisema Tanzania inaendelea kunufaika na uwepo wa Shirika la Ndege la Uturuki kwa kufanya safari zake za moja wka moja kutoka nchini Uturuki, kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo.

Kwa upande wake Rais wa Uturuki, Recep Erdogan alisema kuwa uwepo wa mikataba hiyo baina ya Tanzania na Uturuki itasaidia kupata matokeo mazuri ya uhusiano pamoja na fursa mbalimbali za ushirikiano katika nyanja ya Kilimo, Utalii, Ulinzi, Reli ambazo zitawezesha kukuza uchumi wa mataifa hayo.

Rais Erdogan alisema kuwa Uturuki imelenga kukuza ushirikiano uliopo baina yake na  Tanzania kupitia makongamano ya wafanyabiashara yenye malengo ya kukuza uchumi, kuongeza ajira pamoja na kukuza ujasiriamali baina ya Tanzania na Uturuki.

“Kiwango cha Biashara ya uwekezaji katika nchi ya Uturuki ni Dola za kimarekani 150 ambapo lengo letu ni kufika Dola za kimarekani 500” alisema Rais huyo.

Aidha Rais Erdogan alisisitiza kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia nchi hizi kusonga mbele na kufanikiwa katika nyanja mbalimbali.

Nae Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa makubaliano ya mkataba baina ya Tanzania na Uturuki katika Sekta ya Utalii yatasaidia katika kutangaza vivutio vilivyopo nchini, kubadilishana wataalamu, kubadilishana taarifa na kuongeza idadi ya watalii nchini.

Prof. Magembe aliongeza kuwa makubaliano hayo yatakuza sekta ya utalii katika kuvutia uwekezaji wa katika maeneo ya hoteli, fukwe na mbuga za wanyama zilizopo nchini. (P.T) 

RTKAAA

 Baadhi ya wakazi wa Njombe Mjini wamiwa wanamsikiliza waziri Mkuu Kassm Majaliwa katika maeneo ya Wikichi Mjini Njombe

 Waziri mkuu Majaliwa akizungumza na wakazi wa njombe Maeneo ya Hospitali ya Mkoa wa njombe Mtaa wa Wikichi Njombe Mjini.

Wziriri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha chai cha Kibena 

Na Mwandishi wetu

WAZIRI  Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa ameahirisha ziara yake mkoani Njombe ambapo ameelekea jijini Dar es salaam ambako anatarajia kumpokea Rais wa Uturuki ambaye anakuja hapa nchini kwa ziara ya kikazi Ziara yake inatarajiwa kuendelea januari 25 kwa siku tatu.

Waziri mkuu amekuwa mkoani Njombe kwa siku tatu ambapo amepita katika halmashauri tatu za mkoa huo kabla ya kuahirisha ziara hiyo na kurejea jijini Dar es Salaam kwa majukumu mengine ya kiutendaji ziara yake mkoani Njombe ilikuwa ya siku sita na kuzitembelea halmashauri zote za mkoa huo.

Waziri mkuu Juzi aliwaaga viongozi wa mkoa wa Njombe na kuelekea jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya ndege mkoani Iringa huku akitarajia kulejea tena mkoani humo Januari 25 na kumaliza ziara yake baada ya siku tatu.

Akirejea Njombe atatembelea halmashauri ya wilaya ya Njombe na kutembelea kiwanda cha chai na kuzungumza na wakulimqa wa zao hilo, kasha kuzungumza na wakazi wa Mji wa Njombe baadaye kwenda wilayani Ludewa ambako pia atakutaa na wakazi wa Mundini na Liganga kutako tarajiwa kuwa na migodo ya makaa yam awe na Chuma.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka akizungumza na Nipashe kuhusiana na kuahirishwa kwa ziara hiyo alisema kuwa waziri mkuu alikuwa mkoani humo kwa siku tatu ambapo ameahilisha kuendelea na ziara na kasha kulejea tena Januari 25.

Alisema kuwa waziri mkuu anaelekea jijini Dar es Salaam kwa kuwa nchi itakuwa ikipokea ugeni wa Rais wa Uturuki ambaye anafanya ziara yake hapa nchini ambapo baada ya ziara ya Rais Huyo Waziri mkuu watalejea Mkoani Njombe.

Mwishoni mwa wiki jana Waziri mkuu alikuwa mkoani Njombe na kuzungumza na wakazi wa maeneo mbalimbali ya halmashauri za wilaya Makete, Wangingombe, na mji wa Makambako ambako ndio alianzia ziara yake.

Akiwa Wangingombe alifungua jingo la Halimashauri ya Wangingombe na kuzungumza na wananchi wa Mjia huo kasha kuwataka watumishi wa halmashauri na wilaya kuhamia halmashauri hiyo ifikapo mwezi februari.

Waziri hakusika kuwaeleza wananchi adhima ya serikali kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kumaliza matatizo ya maji na kufanya wafanye shughuli za kimaendeleo bila Bughuza.(P.T)

TUMAI

 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Tumaini mwaka wa tatu wakiwa katika picha ya pamoja chuoni hapo. 

Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Sinza Palestina, Aliho Ngerageza (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa wanafunzi wa Shahada ya Mawasiliano ya Umma mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Tumaini Tawi la Dar  es Salaam (Tudarco), kwa ajili ya wanawake na watoto waliolazwa hospitalini hapo anaekabidhi ni Enock Bwigane  na katikati ni Mhadhiri wa somo hilo chuoni hapo, Mary Kafyome 

 Mhadhiri wa somo la Public Relations chuoni hapo, Mary Kafyome akizungumza na vyombo vya habari.(P.T)

Read more...

RAIS WA UTURUKI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Published in Jamii

WQA

 Rais wa  Uturuki,  Mheshimiwa  , Recep Tayyip Erdogan akiongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa ziara rasmi Januari 21, 2017.Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WQQQ

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan aliyefuatana na  mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo  kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 21, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.

Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat  Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak

Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.(P.T)

EVO

Na.Mwandishi Wetu

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amepongeza jitihada zinazofanywa na muwekezaji wa kampuni TwyFord Tanzania Cereramics,kwa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae “Tiles” katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Waziri Mwijage, amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo, litakalojengwa kiwanda hicho cha kutengeneza vigae “Tiles” kitakachotoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfu mbili katika mfumo rasmi,na ajira elfu nne zisizo rasmi.

“kiwanda hiki kikikamilika kitasidia sio tu kutoa ajira lakini pia kitasidia kwa watanzania kununua na kuuza bidhaa zinazotengenezwa nyumani na sio  kuangiza kila kitu kutoa nje”alisema Mwijage.

Waziri Mwijage aliongeza kuwa,” bidhaa hizi pia zitauzwa katika nchi majirani kama Zambia,Malawi, DRC,Rwanda, Burundi,Uganda na Jamhuri ya watu wa Afrika Kati na kusafirishwa nje ya bara.

Aidha Waziri Mwijage alisema kuwa  kiwanda hicho kitumike vizuri na kutoa wito kwa watanzania kutumia fursa zitakazo patikana katika mradi huo zitumike kwa faida ya kila mmoja, “Serikali ya kijiji itambue maeneo yake ili kusaidia kuharakisha maendeleo ya eneo hili ambapo kiwanda kinafanya shughuli zake”alisema Mwijage.

Kwa upande Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, alisema kuwa ujenzi  wa kiwanda hicho kipo katika hatua ya mwanzo ya Ujenzi na kinataraji kukamilika Mwezi wa Saba na kufunguliwa Rasmi mwezi wa Nane mwaka huu.

 Ridhiwani alisema kuwa kiwanda hicho kitasaidia kufungua mji wa Chalinze na kufanya mji wa viwanda na biashara na hivyo kufungua fursa za kiuchumi na kupanua mji huo,katika sekta ya viawanda inayosimamia vyema na serikali ya awamu ya tano.

 “ujenzi wa kiwanda hiki ni Alama Chanya ya jinsi serikali ya awamu ya Tano ilivyojidhatiti kufungua fursa za viwanda katika Nchi yetu.Wananchi wa Chalinze na Pwani wameaswa kuendelea kujipanga kwa viwanda na fursa nyingi zaidi.”alisema ridhiwani

Ridhiwani aliongeza kwa kunshukuru muwekezaji huyo pia  kwa kukubali kusaidia kumalizia ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Pera na kituo cha afya katika kata hiyo.

“licha ya kukubali kusaidia  ujenzi wa huo lakini pia fursa nyingine watu watapata  nafasi ya kuuza mali ghafi zinazotumika kutengeza  vigae hivyo ambapo tunatarajia asilimia 90 malighafi hizo zitatoka hapa kwetu katika  mikoa ya jirani”.alisema Ridhiwani.(P.T)

Yahya Jammeh aondoka Gambia, nakuacha hazina tupu

Yahya Jammeh aondoka Gambia, nakuacha hazina tupuMshauri maalumu wa Rais wa Gambia Adama Barrow amesema zaidi ya dola za Kimarekani milioni 11 zinaaminika kutoweka katika hazina ya serikali, kufuatia kuondoka madarakani kwa mtawala wa muda mrefu Yahya Jammeh.

Mia Ahmad Fatty amewaambia Waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar kwamba wataalamu wa masuala ya fedha wanatathmini kujua ni kiasi gani kwa sasa kimepotea.

Amesema Gambia kwa sasa ina tatizo kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu.

Kwa sasa Rais Barrow amekuwa akifanya kazi na timu ya wataalamu wa masuala ya fedha na wengine kutoka Benki kuu ya nchi hiyo kupata kiasi halisi kilichopo.

Habari zinasema magari ya kifahari na mali nyingine zilionekana zikipakiwa katika ndege ya mizigo ya Chad kwa niaba ya Rais Jammeh siku alipoondoka nchini humo.

Maelfu ya watu walikusanyika katika Ikulu ya nchi hiyo jana jioni wakiyaangalia majeshi ya Senegal yakiingia kwa ajili ya kuweka usalama kabla ya kurejea nchini kwa Adama Barrow.

Adama Barrow akiwa Dakar, Senegal Januari 20, 2017

Adama Barrow, (katikati), amesema anapanga kuchunguza tuhuma za ukiukaji wa haki za kibinadamu zilizotekelezwa wakati wa utawala wa Jammeh

Rais Barrow yupo nchini Senegal na bado haijulikani ni lini hasa atarudi Gambia na kuingia ofisini.

Alisema atarejea tu baada ya kuhakikishiwa usalama wake.

Wanajeshi wa Senegal wakishika doria karibu na ikulu ya rais mjini Banjul Jumapili

Wanajeshi wa Senegal wakishika doria karibu na ikulu ya rais mjini Banjul Jumapili.  BBC

Karibu Mjengwablog

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

Smartads