habari

Bwawa La Umeme Labomoka, Watu 20 Wapoteza Maisha.

on

Watu 20 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya bwawa la umeme kubomoka katika mji wa Solai, karibu kilomita 200 kaskazini-magharibi mwa Nairobi nchini Kenya, afisa wa serikali amesema leo Alhamisi.

Gavana wa mkoa wa Nakuru amesema kiwango cha uharibifu kinaendelea kutathminiwa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limetangaza kwenye Twitter kwamba limewaokoa watu 39.

Kupasuka kwa bwawa hili kumesababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha mashariki mwa Afrika kwa miezi miwili sasa.

Tangu mwezi Machi, mvua hizo zimeua watu 132 na kusababisha zaidi ya watu 220,000 kuyahama makazi yao katika kaunti 32, serikali ya Kenya imesema.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *