habari

CCM CHAWAKUMBUSHA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM) KUENDELEA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA VIJANA WENZAO NA TAIFA KWA UJUMLA

on

index

Katika semina maalum ya mafunzo kwa Viongozi na Watumishi wa Umoja wa Vijana wa CCM ambayo imeandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndg. Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM amesema Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) lazima waendelee kutimiza wajibu wao kwa vijana wenzao na Taifa kwa ujumla.

Akifafanua suala hilo Ndg. Polepole amesema UVCCM ni taasisi muhimu sana kwa Chama na Vijana wote wa Tanzania, hivyo wanawajibu wa kujizatiti katika kuonesha njia ya maendeleo ya Vijana wa Tanzania na kuwaeleza, kuwahimiza na kuwasisitiza Vijana wenzao juu ya fursa zilizopo kwenye serikali yao.

1

“Mnakazi kubwa ya kuonesha muelekeo wa Vijana kwenye nchi hii, napenda muendelee kuizungumzia Tanzania ya viwanda imetengeneza ajira kiasi gani kwa vijana, mikopo kwa vijana imetolewa kiasi gani na miradi gani ni muhimu katika kukuza ajira kwa vijana” amesisitiza Ndg. Polepole

Aidha Ndg. Polepole amewakumbusha UVCCM kuhusu Imani, Itikadi na Sera za CCM ambazo zinahimiza utu, haki, usawa, umoja, udugu na demokrasia na amewataka Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuendelea kujifunza, kupeana maarifa na taarifa ili waendelee kuwa bora na imara zaidi.

Huu ni muendelezo wa madarasa ya mafunzo ya Chama na Jumuiya zake katika kuimarisha ufanisi na utendaji wa CCM katika kuwahudumia wananchi.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *