habari

CCM Yalalamika Siri za Serikali Kuvuja

on

Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Dk. Antony Dialo amesema miongoni mwa matatizo ambayo watumishi wengi wanaostaafu au kuondolewa katika nafasi wanazoteuliwa na Rais ni kukiuka kiapo chao cha kutunza siri.
Dk. Dialo alisema wapo watumishi wengi hususan wa kuteuliwa wakiwamo  mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala na wengine  wamekuwa wakitoa siri  walizopata wakati wakitumikia nafasi zao kitendo ambacho kinakiuka kiapo chake.
Kauli hiyo aliitoa  hivi karibuni alipozungumza na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mwanza walioteuliwa  Julai 28, mwaka huu na Rais Dk. John Magufuli  huku akiwataka   waliostaafu kwa umri   na walioondolewa katika nafasi zao kuendelea kutunza siri za Serikali.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *