michezo

Chama Cha Soka Ghana Chavunjwa Baada Ya Rais Wake Kupokea Rushwa.

on

Chama cha soka nchini Ghana kimevunjiliwa mbali na serikali ya nchi hiyo baada ya rais wa chama hicho kunaswa katika video akionekana akipokea rushwa.

Rais huyo Kwesi Nyantakyi alipigwa picha akipokea $65,000 kutoka kwa mwandishi habari mpekuzi aliyejifanya kuwa mfanyibiashara aliye na hamu kubwa kuwekeza katika soka nchini Ghana.

Mtandao wa GhanaWeb umeripoti kuwa waziri wa michezo Isaac Asiama amesema chama hicho kimevunjiliwa mbali mara moja, ambapo taarifa zinasema Mpaka sasa rais huyo hajasema chochote kuhusu tuhuma hizo..

Waandishi wanasema uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi habari anayekumbwa na mzozo Anas Aremayaw Anas umezusha maswali kuhusu soka barani Afrika.

Katika makala hiyo ndefu, iliopewa jina ‘wakati ulafi na rushwa zinapokuwa kawaida’, ilikabidhiwa kwa maafisa wa serikali mwezi uliopita na kuonyeshwa wazi mbele ya umma kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano.

Waziri wa habari Ghana Mustapha Abdul-Hamid, amesema serikali imeamua kuchukua hatua za mara moja kukivunja chama cha soka Ghana GFA, akitaja kuenea kwa muozo unoaonekana.

Amesema hatua za muda za kuongoza soka Ghana zitatangazwa hivi karibuni, wakati kukisubiriwa kuundwa chama kipya.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *