We have 427 guests and no members online

kujiepusha na vihatarishi vya ugonjwa wa kisukari

Displaying 01.JPG

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Displaying 02.JPG

Mwandishi wa habari wa Redio Adhana Harith Subeit akitaka ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani kwenye mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.

Displaying 03.JPG

 Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Mohd Dahoma akijibu maswali ya waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari katika mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.(Martha Magessa)

Displaying 04.JPG

Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari Waziri Said Othman akitoa taarifa ya Jumuiya hiyo katika mkutano wa waandishi wa Habari uliofanyika Wizara ya Afya Zanzibar.

Displaying 05.JPG

Mkuu wa Kitengo cha ugonjwa wa Kisukari Zanzibar Dkt. Faiza Kassim Suleiman akitoa ufafanuzi wa masuali ya waandishi wa habari kuhusu hali halisi ya ugonjwa huo katika mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

RAMADHANI ALI/HABARI MAELEZO ZANZIBAR 

Wananchi wameshauriwa kujiepusha na vihatarishi vinavyoweza kupelekea kupata ugonjwa wa kisukari na kujenga tabia ya kupima afya zao ili kujuwa matatizo yanayowakabili.

Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mnazimmoja katika kuadhimisha siku ya kisukari Duniani.

Alisema tatizo la ugonjwa wa kisukari na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo limekuwa kubwa na inakisiwa zaidi ya watu milioni 346 duniani wanasumbuliwa na ugonjwa huo.

Alisema ongezeko kisukari katika nchi nyingi linasababishwa na watu kubadili mfumo wao wa maisha na mabadiliko ya kijamii na kiutamaduni.

Naibu Waziri ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2011 hapa Zanzibar, unaonyesha kiwango cha ugonjwa wa kisukari ni asilimia 3.7 ambayo ni sawa na watu 50,000.

Ali

sema kwa mujibu wa takwimu zinazokusanywa katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja pekee kunawastani wa wagonjwa wapya wa kisukari 300 kila mwaka na zaidi ya watu 180,000 wapo hatarini kupata maradhi hayo kutokana na uzito uliokithiri.

Amewakumbusha wananchi kuwa ugonjwa wa kisukari hauponi na mtu akishaupata hulazimika kutumia dawa katika uhai wake wote na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

"Jambo la msingi ninalosisitiza ni kwamba ugonjwa wa kisukari hauponi, mtu anapothibitika kuwa nao inamaana ataendelea kuwa nao katika maisha yake yote na atalazimika kutumia dawa ama sindano katika uhai wake wote," alieleza Naibu Waziri.

Katika kujikinga na ugonjwa huo Naibu Waziri amewasisitiza wananchi kufanya mazoezi, kujiepusha na matumizi ya pombe na matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku pamoja na kuzingatia umuhimu wa lishe bora.

Amewashauri wananchi kuweka umuhimu wa kuchunguza afya zao kama ni njia moja wapo ya kinga kwani inakadiriwa kuna zaidi ya asilimia 50 ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ambao hawajijui.

Akizungumzia kadhia ya kisukari Mkuu wa Kitengo cha ugonjwa wa kisukari Dkt. Faiza Kassim Suleiman alisema tatizo kubwa linalowapata wenye maradhi hayo ni ganzi, kupoteza nuru ya macho na kupungua nguvu za kiume.

Hata hivyo amesema bado hakujawa na mikakati imara iliyoandaliwa kukabiliana na ongezeko kubwa la ugonjwa huo licha ya kuwepo dawa katika Hospitali na vituo vya Afya.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari Zanzibar Waziri Said Othman amesema dawa za ugonjwa huo zinapatikana lakini tatizo linalowakabili ni dawa za maradhi mengine ambayo yanaenda sambamba na kisukari ikiwemo sinikizo la damu.

Amewashauri madaktari kuongeza juhudi katika kuwashughulikia wagonjwa wa kisukari wenye vidonda kwani tiba yake huchukua muda mrefu kabla mgonjwa kupona.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA