We have 430 guests and no members online

TBS NA TFDA WATAKIWA KUDHIBITI BIDHAA ZISIZO NA UBORA ILI KULINDA UCHUMI

Picha na maktaba

Na Woinde Shizza,Arusha

Mamlaka ya Chakula na dawa(TFDA) na Shirika la Viwango nchini(TBS), wameshauriwa kuwadhibiti zaidi wafanyabiashara wasio waaminini ambao wanaingia nchini bidhaa sizizo na ubora kwani wanaporomosha uchumi.

Meneja masoko wa kampuni ya Wrigleys (EA) Company Ltd, Emanuel Laswai, alitoa kauli hiyo juzi, katika uzinduzi wa bidhaa mpya za kampuni hiyo ya Doublemint nchini Tanzania.

Laswai alisema, uingizwaji wa bidhaa feki na zisizo na ubora zina athari za kiuchumi na kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.

“sisi kampuni yetu kwa mwaka tunalipa kodi Tsh 120 milioni, lakini inaumiza kuona kuna bidhaa zinaingizwa nchini kinyamela bila kulipiwa kodi”alisema

Alisema bidhaa zao zote kabla ya kuingia sokono lazima ziidhinishwe na vyombo vya ukaguzi wa serikali kama TBS na TFDA.

Mkaguzi wa vyakula, dawa, vipodozi ,wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA,kanda ya kaskazini, Barnabas Jacob, akizungumzia tatizo la uingizwaji bidhaa feki alisema Mamlaka hiyo, imeendelea kudhibiti na kukamata na kutekeleza bidhaa hizo.

Jakob alisema milango ya TFDA, iko wazi kwa kila mwananchi kutoa taarifa ya kuwepo kwa bidhaa hatarishi katika mazingira yeyote ili ziweze
kuchukuliwa hatua za kudhibiti bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

Kwa Upande wake, Afisa uhusiano wa shirika la viwango nchini(TBS) Roida Andusamile akizungumza na Mwananchi alisema TBS
itaendelea kudhibiti bidhaa zisizo na ubora kuingia nchini kwa kuanza kudhibiti bidhaa hizo kutoka nchi zinapotoka.

Hata hivyo, alisema ni wajibu wa wananchi pia kutoa taarifa TBS wanapobaini bidhaa zisizo na ubora katika soko au ambazo bado hazijaidhinishwa na vyombo vya serikali, ili kuweza kuchukuliwa hatua mara moja ya kuwadhibiti na kuwakamata wahusika.(Muro)

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA