We have 220 guests and no members online

Neno la Leo; Unachokitarajia Huwezi Kukijua...!

Published in Tafsiri Yangu

Photo: Neno Fupi La Usiku Huu; Unachokitarajia Huwezi Kukijua...!
Ndio maana unakitarajia. Ndio maana unakisubiri. Unachokijua unakitegemea. Kitakuja tu. Yumkini huwezi kuwa na hamu sana ya kukisubiri. 
Naam, moja ya faida ya kuwa mtu mzima ni kuacha kuyaangalia mambo kwa darubini. Unayaona kwa macho yako makavu. Unajenga uwezo wa kusoma alama za nyakati. Na wakati mwingine zinakupotea, lakini, utu uzima unakusaidia kujua kuwa zimekupotea.
Nimejifunza kutoliogopa giza, na hata kulitilia mashaka pia. Maana, giza linapokuwa giza linabaki kuwa giza. Siwezi kuligeuza mwanga.
Na hilo ni Neno Fupi La Usiku Huu.
Maggid, 
Iringa
0788 111 765


Ndio maana unakitarajia. Ndio maana unakisubiri. Unachokijua unakitegemea. Kitakuja tu. Yumkini huwezi kuwa na hamu sana ya kukisubiri.

Naam, moja ya faida ya kuwa mtu mzima ni kuacha kuyaangalia mambo kwa darubini. Unayaona kwa macho yako makavu. Unajenga uwezo wa kusoma alama za nyakati. Na wakati mwingine zinakupotea, lakini, utu uzima unakusaidia kujua kuwa zimekupotea.

Read more...

Neno La Leo: Ya Padri Mushi Na Ugumu Usiokuwepo Wa Kurudi Misri!

Published in Tafsiri Yangu

Photo: Neno La Leo: Ya Padri Mushi Na Ugumu Usiokuwepo Wa Kurudi Misri!
Ndugu zangu,
Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.
Bado, kama taifa, tuko kwenye mshtuko wa kuawa kwa Padri Mushi kule Unguja. Swali bado linaning'inia vichwani; KWANINI?
Watanzania kwa asili ni ndugu, haya ya tofauti za kidini hayajawahi kuwa tatizo kwetu. Mathalan, asubuhi hii nilikuwa naongea na ndugu yangu kijijini Mahango, Madibira, Mbeya. Anaitwa Salim Mjengwa, yeye ni Muislamu, baba yake, Raphael Mjengwa ni Mkristo. Na kwenye familia yao wamechanganyika Waislamu na Wakristo. Kamwe haijawa tatizo kwao wala kwa sisi ndugu zao.
Jana jioni niliongea na Padri Manfred Mjengwa, naye ni mdogo wangu. Alikuwa njiani kwenda msibani Unguja kumzika Padri mwenzake na rafiki yake waliofanya kazi pamoja alipokuwa Zanzibar. Ni Padri Mushi. Ukristo wa Manfred sijapata kuuona ni tatizo kwenye ukoo wetu uliochanganyika kiimani. Hata mmoja wa watoto wangu nimempa jina la baba yake mdogo, anaitwa Manfred. 
 Ndugu zangu,
Kuna tulikotoka na tumeanza kupasahau. Nimepata kuandika yafuatayo, kuwa ni vigumu leo kwa Wana wa Israel kuamua kurudi tena Misri. Hata kama, pamoja na chawa na kunguni walioaacha Misri, bado, kuna Wana wa Israel wanaokumbuka samaki na masufuria ya pilau waliyoayaacha Misri. 
Lakini, kijamii, na kwa kuingalia jamii yetu hii ilikotoka, ilipo sasa na inakoelekea, na tuone sasa, kuwa hakuna ugumu wa kurudi tena Misri. Na hapa nitazungumzia umuhimu wa sisi WaTanzania kujitambua.
 Nahofia, kuwa moja ya kiini ya haya yanayotukuta sasa ni dhambi ya Ubaguzi iliyoanza kututafuna pole pole. Taratibu tunapoteza uwezo wetu wa kujitambua. Ni ukweli sasa, kuwa Watanzania hatujitambui, na kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa na kidini wanapoonyesha wazi wazi kuwa hawajitambui.
 Maana, tumeanza sasa kuzungumza lugha za ‘ Wao Wakristo’ na ‘ Sisi Waislamu’. Tunasahau, kuwa sisi ni ndugu wa damu. Kuwa SISI ni Watanzania Kwanza. Na lililo la kwanza kwetu ni ‘ Nchi Yetu’ na maslahi yake.
Hii ni Nchi Yetu Sote. Kila Mtanzania kwa nafasi yake ana lazima ya kupigania Usalama wa Taifa letu. Usalama wa Nchi Yetu tuliyozaliwa. Hatuwezi kuilinda na kuijenga Nchi Yetu kwenye mazingira ya kubaguana. Kwenye mazingira ya kugawanyika kwa misingi ya udini, ukabila na rangi. Na hapa nitamrejea tena Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na dhana ya Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa.
Ni Mwalimu Nyerere aliyeuanzisha na kuusimamia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa, hata hivyo, tunaona sasa unavyoporomoka na kuliacha taifa letu mashakani. Ndio, Mwalimu alijenga misingi imara ya Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ( Nation Building).
 Kuijenga jamii ya Watanzania yenye kuamini kwenye ukweli kuwa sisi sote ni ndugu. Kwamba Nchi yetu haina dini. Yenye kupiga vita ubaguzi wa aina zote, iwe wa rangi, kabila au dini. Ilimchukua Mwalimu na taifa letu miaka mingi sana kuijenga misingi hiyo iliyowawezesha pia Watanzania kuwa na mioyo ya uzalendo kwa Taifa lao.
 Tunaona sasa, kazi hiyo iliyochukua miaka mingi, kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka ya baadhi ya wanasiasa wetu, wanapelekea kubomoka kwa misingi hiyo na kuliacha taifa letu kwenye hatari ya kuangamia.
Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu. Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao. Kuna Watanzania wengi sasa wanaopoteza mioyo ya uzalendo kwa nchi yao.
 Kuna hata wenye kufikia kutamka; ‘Nchi hii ina wenyewe’. Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali. Hizi si dalili njema kwa taifa. Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa.
Ukiuliza utajibiwa; “Ah! Nchi ina wenyewe!”. Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao.
 Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili.
Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya ‘kila mtu na lwake’. Idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.
 Ndugu zangu, Hakuna ugumu wa kurudi Misri. Tuna lazima ya kupanga safari ya kurudi tena Misri. Inawezekana.
 Na hilo ni Neno la Leo.
Maggid Mjengwa,
 Iringa,
0788 111 765, 0754 678 252
<a href=


Ndugu zangu,

Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.

Bado, kama taifa, tuko kwenye mshtuko wa kuawa kwa Padri Mushi kule Unguja. Swali bado linaning'inia vichwani; KWANINI?

Read more...

Neno La Leo: “ I AM SORRY!”

Published in Tafsiri Yangu

Photo: Neno La Leo: “ I AM SORRY!”
Ndugu zangu,
Neno ‘ Nisamehe’ ni neno fupi sana. Kutamka hilo kwa kimombo ni kusema; “ I ‘m sorry!”
Hata hivyo, neno hilo ni moja ya maneno magumu sana katika lugha nyingi za walimwengu. Neno hilo lina maana kubwa kwa mwanadamu. Laweza kufanya miujiza ya kuwaunganisha watu waliotengana na hata kufikia kuchinjana. Ni pale tu linapotamkwa na mtu mwuungwana na mwenye dhamira ya dhati.
Katika dhambi anazoweza kufanya mwanadamu hapa ulimwenguni, dhambi ya ubaguzi ni moja ya dhambi mbaya kabisa.
Mwalimu Nyerere alipata kutamka; “ Dhambi ya ubaguzi ni sawa na dhambi ya kula nyama ya mtu, ukishaanza kuila tu, basi, hutaacha!” 
Na katika dunia hii ubaguzi hujengwa katika mifumo. Afrika Kusini enzi za Ubaguzi wa rangi walijenga misingi ya ubaguzi. 
Ni kwa kupitia sheria za kibaguzi zilizopitishwa na Bunge. Kati ya sheria hizo ni pamoja na marufuku ya weusi kukutana, kufanya mikutano na maandamano, marufuku ya kupata habari na hata kuchapisha habari na mengineyo. 
Lakini, katika dunia hii, himaya zote huporomoka, hata Roma pia iliporomoka. Na himaya ya utawala wa kibaguzi ikafikia hatima yake.
Na kikubwa kabisa kilichowafanya weupe kwa weusi wa Afrika Kusini kuacha ya nyuma na kwenda mbele kwa pamoja ni neno fupi la ‘ I’m sorry!”- Samahani.
Aliyekuwa kiongozi wa kibaguzi wa Afrika Kusini , De Klerk alisimama mbele ya wanahabari wa dunia na kutamka; “ I am sorry!”. Kwa yote waliyotenda huko nyuma, ikiwamo aliyotenda yeye kama kiongozi. 
Naam, hata hapa kwetu, dhambi ya ubaguzi inaendelea kututafuna. Ni nani mwenye ujasiri wa kusimama mbele ya umma na kutamka; “ I’m sorry!”?
Ndio, huko nyuma TANU na baadae CCM viliamini kuwa
asiyefikiri kama wao basi si mwenzao. Ni mpinzani, ni adui wa maendeleo.
Ni adui wa umma. Ni msaliti. Si mwenzao na alibaguliwa. Alitengwa na pengine kuishia kifungo cha ndani au cha nje. Ni kwa kurudishwa kijijini alikozaliwa au asikozaliwa.
Huko Mtanzania huyo aliyebaguliwa kisiasa. Alifikia kuambiwa kuwa kila siku awe anaripoti kwa Balozi wa Nyumba Kumi. Na kutoka kijijini kwake kwenda kijiji kingine ni sharti aombe ruhusa ya uongozi wa kijiji!
 Na kutoka nje ya wilaya ni sharti apate kibali cha DC! Hii nayo ni historia yetu. Ili tuelewe tulipo na tunakokwenda tuna lazima ya kuipitia
historia yetu.
Ubaguzi wa kisiasa ni jambo baya sana. Migoro mingine inayoibuka kwenye jamii kama hii ya kidini yaweza pia kuwa chanzo chake ni ubaguzi wa kisiasa. Kwamba kuna wanaonyimwa nafasi za kushiriki siasa na kuamua kutumia majukwaa ya kidini kutimiza malengo yao.
Kwamba kuna wanaojiona wao wana haki zaidi kuliko wenzao katika nchi hiyo hiyo ambayo wenzao pia wanaiiita nchi waliyozaliwa. Hivyo, wanawakandamiza wenzao.
 Kwamba wanajiona wana uwezo wa kuwafanya Watanzania wenzao waishi maisha magumu kwa vile tu wanatofautiana au wanapingana kifikra na walio kwenye mamlaka ya dola au Chama kilicho madarakani. 
Ubaguzi wa kisiasa huzaa chuki ya kisiasa. Na mara zote, uvumilivu wa wanaobaguliwa na kukandamizwa hufikia kikomo. Na yanapolipuka, basi, huwa kama nusu ya kiyama. Moto huwaka. Hakukaliki.
Kule Misri vijana wengi wanajua sasa ni kwanini wazazi wao walihangaika sana kutafuta ajira lakini hawakupata. Waliishia kuishi maisha magumu.
Wanajua sasa ni kwanini baadhi yao ( Vijana) hawakupata scholarship au ajira baada ya kufuzu masomo yao. 
Wanajua sasa, kuwa Idara ya Usalama wa Taifa chini ya Hosni Mubarak, familia yake na jamaa zake wa karibu walikuwa na faili maalumu yenye orodha ya majina ya WaMisri, vijana kwa watu wazima, ambao walionekana kuwa ni wenye fikra za kipinzani. 
Kuna waliochunguzwa tangu wakiwa kwenye mijadala ya vyuo vikuu. Na ambaye jina lake limeingizwa kwenye faili hilo, basi, ataandika kurasa kwa maelfu za barua za maombi ya
kazi, na atasaga lami sana hadi soli za viatu ziishe akitafuta ajira bila mafanikio. 
Serikali ya Hosni Mubarak ilikuwa na mikono mirefu, na miguu pia. Tatizo lilikuwa kwenye ‘kichwa cha Serikali’. Kilikuwa kidogo sana, maana hatma ya yaliyomfika Hosni Mubarak ingepaswa kuepukwa na mtu mwenye kichwa kinachofikiri. Kwa vile kilichotokea kingetokea, ilikuwa ni suala la wakati tu.
Ndio, Usalama wa Taifa ( Zaidi Usalama wa Hosni Mubarak na Chama chake) ulihakikisha Mmisri ambaye jina lake limo kwenye kitabu chao hapati kazi yeyote ile, labda iwe ya kubeba zege ili hali ana digrii ya chuo Kikuu. 
Ndugu zangu,
Moja ya faida ya kuwa mtu mzima ni ukweli kuwa huhitaji kuliangalia kila jambo kupitia darubini. Mengine utayaona kwa kutumia uzoefu tu.
Ndio, tunajenga nyumba moja, lakini tunagombania fito. Ni hulka za ubinafsi. Na tunaweza kwenda mbele kama taifa, kwa kuyaongea kwa uwazi ya nyuma. Kuyabaini mapungufu yetu, na kuwa na ujasiri wa kutamka; “ I’m sorry!”
Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa,
0788 111 765
<a href=

Ndugu zangu,

Neno ‘ Nisamehe’ ni neno fupi sana. Kutamka hilo kwa kimombo ni kusema; “ I ‘m sorry!”

Hata hivyo, neno hilo ni moja ya maneno magumu sana katika lugha nyingi za walimwengu. Neno hilo lina maana kubwa kwa mwanadamu. Laweza kufanya miujiza ya kuwaunganisha watu waliotengana na hata kufikia kuchinjana. Ni pale tu linapotamkwa na mtu mwuungwana na mwenye dhamira ya dhati.

Read more...

Neno La Leo- Padri hauawi, hata Sheikh pia...

Published in Tafsiri Yangu

pedre 65d50

Padre Ambrose,aliyepigwa risasi hivi karibuni

One Does Not Kill A Priest, Not A Sheikh Either!


Ndugu zangu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuuawa kwa Padri Mushi wa Kanisa la Minara Miwili huko Zanzibar asubuhi ya leo.

Tumelelewa tukiamini, kuwa hakuna atakayethubutu kumpiga risasi Padri au Sheikh.

Read more...

Photo: Neno Fupi La Usiku Huu: Ukimya Wa Marafiki Unaumiza Zaidi Kuliko Kelele Za Maadui...!
Ndugu zangu, 
Maneno hayo juu yalipatwa kutamkwa na Martin Luther King ( Jr) alipokuwa gerezani.
Mwanadamu unapokuwa kwenye matatizo unawahitaji zaidi wanadamu wenzako, na hususan marafiki.
Moja ya hotuba bora kabisa kupatwa kutolewa na Julius Nyerere ni ile ya mwezi Oktoba mwaka 1978. Ni pale alipotangaza vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda. 
Nilikuwa na miaka 12 tu. Nakumbuka niliisikiliza hotuba ile kutoka mwanzo hadi mwisho; neno kwa neno. Nikiri, kuwa Julius Nyerere alikuwa hodari sana kwenye rhetoric- sanaa ya kuzungumza.
Kwa mtawala, kuamrisha vikosi vya nchi yako kwenda vitani ni moja ya maamuzi magumu sana. Na wakati mwingine, hotuba ya kuamrisha vita yaweza kuamua hatma ya vita. 
Kwenye hotuba ile, Julius Nyerere aliweka vema msingi wa hoja, ya kwanini, sisi , kama taifa, tulilazimika kwenda vitani.
Na akatamka yafuatayo yaliyosisimua na kuhamasisha vikosi na taifa kwa ujumla. Kwamba;
- Uwezo wa kumpiga Amin tunao...
- Sababu ya kumpiga Amin tunayo..
- Na nia ya kumpiga Amin tunayo...
Kisha akatoka nje ya mipaka yetu akitamka; 
" Tunataka dunia ituelewe hivyo". Akaonyesha pia kuwa taifa lina marafiki kwa kutamka;
" Marafiki zetu kwanza tuacheni, tumwonyeshe mshenzi huyu!"
Naam, katika maisha, mwanadamu kuna wakati unalazimika kuingia vitani. Unalazimika kupambana kudai haki yako na kulinda hadhi yako. Hayo ni mapambano ya haki. Na vita ya kudai haki ni vita ya lazima kupiganwa.
Hapo mwanadamu anakuwa kwenye matatizo. Katika hali hiyo, anachohitaji mwanadamu ni kuungwa mkono na marafiki zake. 
Katika hilo, kama alivyotamka Martini Luther King Jr, kwamba ukimya wa marafiki unaumiza zaidi kuliko kelele za maadui.
Na hilo ni Neno Fupi la Usiku Huu.
Maggid Mjengwa,
Iringa.


Ndugu zangu,

Maneno hayo juu yalipatwa kutamkwa na Martin Luther King ( Jr) alipokuwa gerezani.

Mwanadamu unapokuwa kwenye matatizo unawahitaji zaidi wanadamu wenzako, na hususan marafiki.

Moja ya hotuba bora kabisa kupatwa kutolewa na Julius Nyerere ni ile ya mwezi Oktoba mwaka 1978. Ni pale alipotangaza vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda. 

Read more...

makala yangu raia mwema

Published in Tafsiri Yangu

IMG-20130213-00858 01c4a

makala yangu raia mwema

Published in Tafsiri Yangu

Uchambuzi Wa Habari: Je, Tumejiandaa Na ' Uvamizi Wa WaChina?'

Published in Tafsiri Yangu

wachina f9197


Ndugu zangu,
Jeshi la Wachina linakuja, wako wengi. Kwenye moja ya picha za magazetini hii leo, inamwonyesha Rais wetu akiwa amezungukwa na Wachina.

Rais amevalia ' Kijamaa', lakini Wachina wamevalia ' Kibepari'.

Naam, China ni taifa kubwa kiuchumi. Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa, ni uchumi wa Kibepari.

Read more...

Neno La Leo: Mkurugenzi Anaporudisha Fedha Hazina...

Published in Tafsiri Yangu

urambo 46aceNdugu zangu,
Wanazuoni wa Kiislamu ni wenye kufahamu zaidi juu ya kisa kifuatacho nilichokipokea miaka mingi iliyopita. Hivyo, wanaweza kukiboresha zaidi.

Inasimuliwa, kuwa katika wakati wake, Mtume Muhammad (S. A. W) alipata kupokea makusanyo ya zakka kutoka kwa mjumbe wake.

Mjumbe yule katika kupita kwake na kukusanya zakka, huko alipewa pia zawadi mbali mbali. Basi, alipofika kwa Mtume na kukabidhi zakka, akaweka kando zile zawadi alizopewa na waja wa Mwenyezi Mungu. Akakabidhi tu kile alichoambiwa akusanye kama zakka.

Read more...

wateule wanapotofautiana katiba mpya...!

Published in Tafsiri Yangu

neno 03622

 Ndugu zangu,

Miongoni mwa viongozi waliopata kuongoza dola ya Kiislam, hususan baada ya Mtume Muhammad (SAW) , na baada ya masahaba, ni Amir Muuminina Khalifa Umar bin Abdulaziz.

Wanazuoni wa Kiislam wanatwambia, kuwa utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz ulijaa uadilifu. Si kwa viongozi tu, hata kwa raia wake.

Read more...

makala yangu raia mwema

Published in Tafsiri Yangu

Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA