We have 429 guests and no members online

Neno La Leo: Mengine Tuyafanyayo Hupelekea Maanguko Yetu!

Photo: Neno La Leo: Mengine Tuyafanyayo Hupelekea Maanguko Yetu!
Ndugu zangu, 
Kupitia kitabu chake ’ Kusadikika’, mwanafasihi Shaaban Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.
Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali.  Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.
Hapo, mchwa hukabiriwa na  hatari kubwa.  Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu.  Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa  anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.
Naam, mengine tuyafanyayo hupelekea maanguko yetu. Hata kama mwanzoni huonekana kutupaisha juu angani.
” Nafikiri, ndio maana naishi”- Anasema mwanafalsafa Rene Descartes.
Na maarifa ya Sayansi  yanatusaidia kuyabaini mahusiano kati ya dunia tunayoishi na mazingira yanayotuzunguka. Hiyo ni falsafa ya kivitendo. Ndio iliyo bora kuliko ile dhanifu- Speculative.
Iweje basi tumekuwa ni  watu wa  kuishi kwa  dhahnia na hata kusambaza uvumi?
Tusisahau, kuwa kiu ya mwanadamu siku zote ni kutaka kuujua ukweli. Ukweli mzima.
Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
<a href=
Ndugu zangu,

Kupitia kitabu chake ’ Kusadikika’, mwanafasihi Shaaban Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.

Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali. Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.

Hapo, mchwa hukabiriwa na hatari kubwa. Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu. Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.Naam, mengine tuyafanyayo hupelekea maanguko yetu. Hata kama mwanzoni huonekana kutupaisha juu angani.

” Nafikiri, ndio maana naishi”- Anasema mwanafalsafa Rene Descartes.

Na maarifa ya Sayansi yanatusaidia kuyabaini mahusiano kati ya dunia tunayoishi na mazingira yanayotuzunguka. Hiyo ni falsafa ya kivitendo. Ndio iliyo bora kuliko ile dhanifu- Speculative.

Iweje basi tumekuwa ni watu wa kuishi kwa dhahnia na hata kusambaza uvumi?

Tusisahau, kuwa kiu ya mwanadamu siku zote ni kutaka kuujua ukweli. Ukweli mzima.
Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz/

Tuma Maoni

Security code

Anzisha upya

Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA