We have 434 guests and no members online

Neno Fupi La Usiku Huu; Ya Bwana Yesu Na Ufupi Wa Zakayo!

Photo: Neno Fupi La Usiku Huu; Ya Bwana Yesu Na Ufupi Wa Zakayo!
" Yule Zakayo ni mtu mfupi, alitaka kumuona Yesu,
Alipanda juu, juu ya mkuyu
Yesu akamwiita, Zakayoo Njoo
Zakaayo Njoo, Shuka juu ya mti...!"
Ndugu zangu,
Wimbo huo wa kwaya niliusikia utotoni mwangu. Nilijiuliza sana kuhusu kisa cha Zakayo na Bwana Yesu. 
Hakika kinahusu hesabu pia, kama  tulivyoona utata wa ushahidi wa Kalumekenge na Bwana Njau juu ya urefu wa mtuhumiwa. Njau alimwona mtuhumiwa mfupi kwa vile yeye ni mrefu, na Kalumekenge alimwona mtuhumiwa mrefu kwa vile yeye ni mfupi.
Kwenye Biblia inaandikwa, kuwa Zakayo alikuwa mkusanya kodi. Alikuwa dhalimu kwa watu. Aliwanyanyasa katika kukusanya kwake kodi.
Siku Bwana Yesu alipofika kwenye mji wao, umati wa watu ulikusanyika. Zakayo naye alitaka kumwona Yesu. Kwa vile alikuwa mfupi, alipanda juu ya mti wa Mkuyu.
Yesu akamwona. Akamwita; Ewe Zakayo, shuka juu ya mti...!
Yesu akaenda hadi nyumbani kwa Zakayo. Tendo hilo lilimstaajabisha Zakayo. Wanazuoni wa Kikristo huenda wanaweza kukifafanua zaidi kisa hiki .
Lakini, tukirudi kwenye lile la hesabu. Yumkini Zakayo alipokuwa juu ya mti kwake Yesu alikuwa ni mtu mfupi. Na mara Yesu alipomsogelea Zakayo, bai, Yesu akawa mrefu!
Ni Neno Fupi La Usiku Huu.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
<a href=

http://mjengwablog.co.tz/

HEADER

Guest
0Guest2013-10-14 19:57#1
Suala la zakayo ni refu zaidi kwa kua alisema anataka kuona yesu ni mtu wa namna gaini alisikia kuzaliwa kwake ni kwa uwezza wa Roho mtakatifu pia herode aliua watoto wengi sana huko bethlehemu na alisikia Kua alitembea juu ya maji akajiuliza huyu ni wa namnagani
Mnukuu
Guest
-1Guest2013-10-16 13:45#2
Je wewe ni mfupi kama zakayo isiwesababu yakushindwa kumuona YESU ufupi ni sawa namatendo mabaya urefu ni matendo mema ndg
Mnukuu
Guest
0Guest2014-02-16 13:23#3
la hasa urefu ni matendo mabaya ufupi ni matendo mema kwa mfano njia pana ni ya wenye dhambi na njia nyembamba ni ya wenye kutenda mema
Mnukuu

Tuma Maoni

Security code

Anzisha upya

Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA