We have 431 guests and no members online

Neno La Leo: Ujamaa Ni Imani

Ndugu zangu,

Kuna wajumbe walioniuliza nini hasa maana ya itikadi? Ni nini maana ya mrengo wa Kushoto na Kulia. Nimepata kuzungumzia hili huko nyuma. Nitarudia tena.

Kusimama kwenye Ujamaa ni kusimama Kushoto kiitikadi. Kuna tuliozaliwa kwenye Ujamaa, tumekulia kwenye Ujamaa, na tutakufa Wajamaa.Itikadi ni Imani pia. Ndio maana ya kusemwa, kuwa Ujamaa ni Imani. Kuyumba kiitikadi ni jambo baya. Na kwa kiongozi humaanisha kutojitambua. Hupelekea anguko la kisiasa.

Na kwenye siasa, unapozungumzia Kushoto na Kulia ina maana ya political distiction. Kwenye lugha ya kiimani na hususan Ukristo, Kulia ni Nzuri na Kushoto ni Mbaya.

Inasemwa, kuwa Bwana alimweka kondoo Kulia kwake, na mbuzi Kushoto kwake. Kondoo ameahidiwa nchi takatifu, wakati mbuzi mahali pake ni kwenye moto usiokoma.

Na Yesu alikaa kulia kwa Mungu, kama ilivyo kwa Malaika wa Mungu, nao walikaa kulia mwa altani yenye kufuka moshi.

Lakini, kwenye lugha ya siasa, tangu zama za Mapinduzi ya Ufaransa, hali hiyo ni kinyume. Kushoto, kwa maana walio kwenye mrengo wa kushoto, wao, kwenye Bunge la Taifa, walikaa Kushoto kwa Spika wa Bunge.

Kwa ufupi kabisa, kinachotofautisha Kulia na Kushoto kwenye itikadi ni mtazamo juu ya Usawa. Tulio kwenye mrengo wa Kushoto tunaamini, kuwa Kutokuwepo kwa Usawa katika jamii ni jambo lenye kudhalilisha na lisilopaswa kuwepo. Walio kwenye mrengo wa Kulia wanaamini, kuwa kutokuwepo kwa Usawa katika Jamii ni jambo lisiloepukika.

Walio kwenye mrengo wa kulia wanahofia sana mrengo wa Kushoto, wakati, tulio kwenye mrengo wa Kushoto tunaamini, kuwa tuko kwenye njia sahihi katika kuipata jamii yenye Usawa. Maana, Amani na utulivu haviwezi kupatikana kwenye jamii isiyo na Haki na Usawa. Hivyo, kutokuwepo kwa Maendeleo.

Na kwa vile, kwenye jamii kama ya kwetu, pengo la walio nacho na wasio nacho linazidi kupanuka, basi, itikadi ya mrengo wa Kushoto inahitajika kuliko wakati mwingine wowote. Hivyo basi, uwepo wa misingi thabiti ya itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea uliofanyiwa mabadiliko ya kimsingi.

Ni Neno La Leo.

Nassor Barsheba Nimekuelewa vzr sana comrade .je wananchi wana wajibu gani wa kuyaleta hayo .na kwa njiya IPI?

5 mins · Like

John Kalla Asante mwenyekiti kwa ufafanuzi...inatuongezea ujuzi wa mambo ..

2 mins · Like

HEADER

Boaz Lunyungu
0Boaz Lunyungu2015-03-26 04:26#1
Tatizo kubwa tunadhani bila usaw kutakuwepo na amani mtu hawezi kuwa na amani wKati hana uhakika wa kula , kutibiwa kulipa ada za watoto, tunahitaji kuona wale wanaohubiri kuhusu umaskini nao wanaishi maisha ya umaskini , tunahitaji kuwa na usawakatika mgawanyo wa pato la taifa , tu ahitaji kuwa na usawa katika kumilki ardhi , tunshitaji kuwa na usawKatika ulipaji kodi tunahutaji kuwa na usawzkatika elimu tunayotoa kwa watoto wetu na kila mtu aone kweli usawa upo, tunahitaji usawa katika kutoa haki kwenye vyombo vyetu vya sheria bila kujali vipato vyetu, kukiwa na usawa amani itakuwepo na maendeleo yatakuwepo.
Mnukuu

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA