We have 458 guests and no members online

BENKI KUU YAKANUSHA UVUMI POTOFU KWAMBA SARAFU YA SHILINGI 500 INA MADINI NA NI MALI

Benki Kuu imekanusha vikali kwamba sarafu ya shilingi 500 ina madini ndani yake hivyo ni mali inayoweza kutumika kutengenezea vito, kufuatia uvumi potovu ulioenea kila pembe ambao unawafanya wananchi wengine wanunue sarafu hiyo kwa bei mara tano hadi kumi y thamani yake.

Akiongea na Globu ya Jamii jijini Dar es salaam leo, Meneja wa vituo vya Utunzaji wa Benki Kuu Bw. Abdul Dollah, amesema kwamba uvumi huo si kweli na kwamba katika sarafu ya shilingi 500 kuna madini machache mno ya nickel ambayo hayafai hata chembe kutengenezea vidani.

Amesema sio kweli kwamb sarafu za shilingi 500 hazipo katika mzunguko kutokana na kuhodhiwa na hao wenye kuvumisha na wanaotaka faida ya haraka haraka, na kwamba zinapatikana kwa wingi katika vituo vyake vyote.

Amesema huenda wananchi wanachanganya sarafu hiyo ya 500 na sarafu maalumu iliyotolewa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ambayo alikiri kwamba ina madini na thamani yake ni shilingi 50,000/-.(Muro)

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA