We have 431 guests and no members online

ACACIA KUKUSANYA DOLA 200,000

Kundi la watu 21, wakiwemo, wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro Juni 22, 2015

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (katikati), akiwa na Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo, (kushoto), akizungumza muda mfupi kabla ya kuongoza timu ya wapanda mlima Kilimanjaro kwa nia ya kukjsuanya fedha hizo

Brad, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Necta Pendaeli Foya (katikati)

KAMPUNI ya ACACIA inayojishughulisha na uchimbaji na utafutaji madini, imezindua kampeni ya kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, leo Jumatatu Juni 22, 2015, ambapo fedha hizo zitakwenda kusaidia sekta ya elimu kwenye maeneo yanayozunguka migodi mitatu inayomilikiwa na kampouni hiyo ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwenye lango la Machame,iliyo shirikisha watu 21, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Brad Gordon, alisema, kampuni yake ilianzisha mpango ujulkikanao kama “CAN EDUCATE”, ikimaanisha tunaweza kujieleimisha, imeamua kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, ili kusaidia elimu na kampuni inimekuwa ikifanya hivyo kila mwaka.

“Lengo ni kukusanya dola za Kimarekani 200,000, zitakazosaidia jamii inayokaa kuzunguka maeneo ya migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo” alisema Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa Kmapuni, Asa Mwaipopo.

Na kuongeza kuwa kuna watoto wengi wanashindwa kendelea na elimu ya sekondari na ile ya chuo kikuu, sio kwa sababu za uwezo mdogo wa kimasomo, bali ni ukosefu wa fedha za kuendelea na elimu.

Acacia imeamua kushiriki katika kuwasaidia watoto hawa ili watimize ndoto zao. Alimaliza Mwaipopo. Pichani, Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya ACACIA, Brad Gordon, (Wapili kushoto), akiongoza timu ya watu 21 wakiwemo wafanyakazi, marafiki na familia za wafanyakazi wa kampuni hiyo ,kupanda Mlima Kilimanjaro kwenye lango la Machame mkoani Kilimajaro Jumatatu Juni 22, 2015, kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini.(Habarin na K-VIS MEDIA, picha na Dixon Busagaga)(Muro)

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA