michezo

COCA-COLA Bonite Yazidi Kuleta Raha Ya Mzuka Wa Soka Na Coka Kanda Ya Kaskazini

on

Mmoja wa  washindi wa fedha taslimu akipokea zawadi yake
Wakati mashindano ya kombe la Dunia 2018 yanakaribia, kampuni ya Coca-Cola Bonite Bottlers Limited  ya mjini Moshi inazidi kumwaga zawadi za pikipiki,luninga za kisasa na fedha taslimu  kwa wakazi wa Kanda ya Kaskazini kupitia promosheni ya Mzuka wa Soka na Coka inayoendelea.
Akiongea katika  hafla ya  kukabidhi zawadi kwa washindi  16 wa wiki liyopita, Meneja Mauzo wa Bonite, mkoa wa Arusha Bw. Boniphace Mwasi, alisema zaidi ya wateja 50 wamejishindia zawadi na zawadi bado ziko nyingi. “Bado tunazo zawadi nyingi hivyo natoa wito kwa wakazi wote wa kanda ya kaskazini kuchangamkia kunywa soda za Coca-Cola, ili waweze kujishindia zawadi”.
Wakiongea  muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa kuleta furaha kwa jamii hususani kwa kuwakwamua kiuchumi.

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *