habari

Cuba Yatangaza Maombolezo Baada Ya Ajali Ya Ndege Iliyosababisha Vifo.

on

Zaidi ya watu 100 wameuawa baada ya ndege aina ya Boeing 737 kuanguka muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka Havana nchini Cuba, ajali ambayo imetajwa kuwa mbaya zaidi kuikumba Cuba katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti ni watu watatu tu walionusurika katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni. Ndege hiyo ilikuwa imewabeba watu 105 na ilikuwa ikielekea mjini Holguin, mashariki mwa Cuba.Cuba imeahidi kufanya uchunguzi kubaini sababu ya ajali hiyo ya ndege.

Rais mpya wa nchi hiyo Miguel Diaz Canel aliitembelea sehemu ilikoanguka ndege hiyo na kusema matukio yote yatafanyiwa uchunguzi na ripoti itatolewa. Wahanga wengi walikuwa raia wa Cuba, lakini walikuwemo pia raia watano wa kigeni pamoja na marubani kutoka nje ya nchi. Cuba imetangaza maombolezi kuanzia leo saa sita mchana hadi kesho Jumapili.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *