habari

Dk.Ndugulile Ahidi kutoa Bilioni Moja kuanza Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya

on

Kurushwa hewani:

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akikagua stoo kuu ya kuhifadhi dawa katika hospitali ya Rufaa ya Haydom

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile  amefanya ziara ya kikazi Mkoani Manyara na kutembelea halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ili kujionea shughuli mbalimbali  katika  Hospitali ya Rufaa ya Haydom na Kituo cha Afya cha Dongobesh, akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Haydom  aliweza kupokea taarifa ya hospitali na kisha kutembelea sehemu mbalimbali ndani ya hospitali kujionea huduma zitolewazo.

Mganga Mkuu wa Hospitali Dokta Emanuel Nuwasi akisoma taarifa ya utendaji ya hospitali ya rufaa ya Haydom

Akisoma taarifa ya Hospitali ya Rufaa ya Haydom,Mganga Mkuu wa Hospitali Dokta Emanuel Nuwasi aliweza kueleza changamoto mbalimbali zinawazowakabili ikiwa ni pamoja na changamoto ya ufinyu wa bajeti,changamoto ya bajeti ndogo ya dawa tofauti na mahitaji, vitendanishi tiba kutoka bohari ya dawa(MSD), Kuharibika kwa Mashine ya CT SCAN, kukatwa kodi kwa Call Allowance,changamoto kwa Watumishi wanaolipwa kwa Ruzuku( Salary Grant),kucheleweshwa kusainiwa kwa makubaliano maalum juu ya utoaji huduma (MOU),kuondokewa kwa Watumishi kutokana na mazingira

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akikagua chumba cha kuhifadhi damu salama.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akifurahi mara baada yakukuta taarifa za wagonjwa zikiingizwa katika mfumo.

Mara baada ya kupokea taarifa ya Hospitali Dokta Faustine alihaidi kwenda kushughulikia changamoto hizo zinazowakabili kutokana na hospitali hiyo kuwa kwenye mchakato wa kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya Rufaa ya Kanda,aidha Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine alitoa ushauri kwa uongozi kuweza kutekeleza maagizo waliyopewa na kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu ili hospitali hiyo iweze kupandishwa hadhi mapema.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akiongea na baadhi ya wananchi walikuja kutembelea wagonjwa katika wodi la wazazi

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akiwa katika wodi la wanaume akikagua taarifa za mgonjwa mmojawapo

Sambamba na maagizo hayo Dkt. Faustine ameendelea kuhimiza kusimikwa kwa Mfumo wa Afya (GoTHOMIS) ili kuweka kumbukumbu sahihi za Wagonjwa,Madawa yanayotoka na na kuingia pamoja na kudhibiti Mapato yanayokusanywa ,pia alipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa sasa kutokuwa na kituo cha Afya/Zahanati yoyote yenye hadhi ya nyota 0 na hatimaye kuweza kukabidhi cheti cha hadhi ya nyota 2 kwa zahanati ya Labay.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akipitia kwa makini taarifa ilikuwa inawasilishwa.

Watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Haydom wakiwa ukumbini wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile

Akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kata ya dongobesh, Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile amehaidi kuleta fedha kiasi cha Bilioni moja mwisho wa mwezi huu,hii ni kutokana na Serikali imekwisha leta kiasi cha shilingi Milioni 500 ambazo ni kwa ajili ya Ujenzi wa hospitali ya Wilaya kwa kutumia nguvu ya wananchi( force account), hivyo kuagiza fedha hizo zitakapoingia ujenzi huo uanze mara moja.

Wananchi wa kata ya Dongobesh wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya kata ili kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile

Waheshimiwa Madiwani wa Viti Maalum kata ya Dongobesh kwa tiketi ya CCM, Mhe. kipapai na Mhe. Esther wakikabidhi zawadi ya Shuka( mgoroli),Kitenge na Vitunguu Swaumu Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile

Akihitimisha ziara yake Wilayani Mbulu,Dokta Faustine amehimiza kuanza mkakati mapema wa kutoa elimu juu ya lishe bora na kuandaa mpango mkakati wa matumizi ya vyoo bora.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akipata maelezo zaidi juu ya ujenzi wa chumba cha kuhifadhi Maiti kutoka kwa Mhandisi wa Halmashauri mwenye shati jeupe Mhandisi Bundala.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *