habari

Edward Lowassa Atangaza kuhama CHADEMA na kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM)

on

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Jana Machi Mosi 2019.
Lowassa ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati kuu CHADEMA alihama CCM na kujiunga CHADEMA, Julai 2015 ambapo aligombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho.

Amepokelewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli  katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam

Akizungumza kwa kifupi wakati wa hafla hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema, “Kama alivyosema Waziri Mkuu Mstaafu, Lowassa, amerudi nyumbani. Kwa hiyo tunaanza kazi ya kujenga taifa letu, na kulinda uhuru wetu.”

Advert

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *