habari

Ephraim Kibonde azikwa makaburi ya Kinondoni

on

Aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds Media Group (CMG), Ephraim Kibonde amezikwa leo Machi 9 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam majira ya saa Kumi jioni.
Amezikwa na maelfu ya watu ambao ni ndugu, jamaa na marafiki aliokuwa akifanya nao shughuli mbalimbali enzi za uhai wake na wengine waliomjua kupitia kazi yake ya utangazaji.

Kibonde amefariki dunia Machi 7 mwaka huu baada ya kuugua Presha kwa muda mfupi katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza.

Ameacha watoto watatu, wakike wawili na mmoja wakiume.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *