habari

FBI Wafanya Upekuzi Ofisi Za Wakili Wa Rais Trump.

on

Maafisa kutoka Idara ya Upelelezi ya Marekani – FBI wamefanya upekuzi katika ofisi za wakili wa muda mrefu wa Rais Donald Trump, Michael Cohen. Wakili wa Cohen Stephen Ryan amesema upekuzi huo umetokana kwa sehemu na maelekezo ya Robert Mueller, mwanasheria maalum anayeongoza uchunguzi kuhusiana na madai ya kula njama kati ya timu ya kampeni za Trump na Urusi wakati wa uchaguzi wa rais nchini Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Trump amelaani vikali uvamizi huo na kusema kuwa uchunguzi wa Mueller ni shambulizi dhidi ya Marekani. Michael Cohen amekuwa kwenye vichwa vya habari katika wiki za karibuni tangu ilipofichuliwa kuwa alilipa dola 130,000 kwa mcheza filamu za ngono Stormy Daniels kabla ya uchaguzi wa rais wa mwaka wa 2016, ambazo alisema yalikuwa malipo ya kumfanya kusalia kimya kuhusu madai ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Trump.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *