michezo

Gabriel Jesus Asaini Mkataba Mpya ndani ya Man City

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea club ya Man City ya England Gabriel Jesus jana August 3 2018 ametangaza kuongeza mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kusalia Etihad akiitumikia club hiyo ya jiji la Manchester.

Gabriel Jesus amesaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia Man City hivyo kutokana na mkataba wake wa awali Man City ulikuwa umesalia miaka miwili, sasa atakuwa Man City hadi mwaka 2023, hivyo atakuwa akilipwa mshahara wa pound 100000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 290.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Gabriel Jesus alijiunga naMan City mwaka 2015 akitokea club ya Palmeiras ya kwao Brazil kwa dau la pound milioni 27, mkataba wake wa awali alikuwa akilipwa pound 70000 kwa wiki ambao ni zaidi ya Tsh milioni 200, Jesus ameifungia Man City magoli 24.

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *