michezo

Giggs: Ni Wakati Wa Kumuombea Fergurson Na Kuamini Kuwa Atapona.

on

Meneja wa Wales Ryan Giggs amesema anaamini na anaomba meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson aweze kupona tatizo lake la uvujaji wa damu ubongoni.

Meneja huyo wa zamani alimruhusu Giggs wakati huo akiwana miaka 17 kucheza kwa mara ya kwanza katika timu ya Manchester United mnamo 1991 na alikuwa katika kikosi cha kwanza cha mechi 13 za Ferguson na kushinda mataji ya Premier League.

Giggs ameliambia shirika la habari la BBC Wales, kwamba Sasa ni wakati wa kumuombea na kutamaini kuwa atapona kikamilifu.

“Amekuwa na ushawishi mkubwa katika kazi yangu ndani na hata nje ya uwanja. Najua upasuaji ulikuwana ufanisi – lakini yeye ni mponaji na hilo ndilo linalonifanya nikafikiria kuwa ataweza kupona.”

Ferguson, mwenye umri wa miaka 76, bado yupo katika hali mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura siku ya Jumamosi.

Meneja wa sasa wa Manchester United na mlinzi wa timu ya taifa ya England Phil Jones, pia ametuma ujumbe kama wa Giggs kwamba anamuombea Ferguson na amemtaja kama babake.

Jones alisajiliwa kutoka Blackburn na Ferguson akiwa na umri wa miaka 19 mnamo Juni 2011 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda cha mechi yake ya mwisho kabla astaafu mnamo Mei 2013 baada ya kushinda mataji 38 katika muda aliyohudumu wa miaka 28 katika klabu hiyo.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *